REAL MADRID YAINGIA KWENYE MBIO ZA KUMSAJILI ROONEY.
Taarifa kutoka jijini Madrid
zinasema mshambuliaji Wayne Rooney ameingia kwenye orodha ya washambuliaji
wanaowataka mwishoni mwa msimu.
Huku mkataba wa Rooney ukiwa umebaki
miezi 18 na inavyoelekea hana nia ya kuongeza mkataba mpya pia klabu ya Manchester Utd haipo tayari
kumuuza Rooney kwa vilabu vya England.
Kwenye orodha ya majina ya
washambuliaji wanaotakiwa na Real Madrid ukiacha jina la Rooney ni Radamel
Falcao na Kun Aguero
Sababu inayompa nafasi kubwa Rooney
kusajiliwa na Madrid ni uwezo wake kucheza nafasi mbali mbali ukiacha nafasi ya
ushambuliaji pia kocha wa sasa wa Madrid Carlo Anceletti anamfahamu vizuri
katika kipindi alichokuwa anaifundisha Chelsea.
Kama Rooney atafanikiwa kujiunga na
Madridi msimu ujao basi atajiunga tena na mshambuliaji Cristiano Ronaldo
waliyekuwa pamoja kwenye klabu ya Manchester Utd.
source:shafih dauda
OFFICIAL: TFF YAZUIA USAJILI WA EMMANUEL OKWI YANGA
USAJILI WA OKWI YANGA WAZUIWA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesimamisha usajili wa mshambuliaji
Emmanuel Okwi kutoka Uganda katika timu ya Yanga wakati likisubiri
ufafanuzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana leo (Januari 22
mwaka huu) kupitia masuala mbalimbali, imesimamisha usajili huo baada ya
kubaini kuwa Okwi aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali
maalumu kutoka FIFA.
Okwi
ambaye aliingia mgogoro na klabu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia
aliruhusiwa na FIFA kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu (provisional
permit) cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi
ya Etoile du Sahel likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.
Katika
FIFA kuna kesi tatu kuhusiana na suala la mchezaji huyo. Wakati Okwi
ameishitaki klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel
imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. Nayo Simba imeishitaki Etoile du
Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola
za Marekani 300,000.
Hivyo,
TFF imeiandikia FIFA kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza
Ligi nchini Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika
shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake.
MECHI ZA TANZANIA PRISONS YAZASOGEZWA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesogeza mbele mechi za raundi ya 14
na 15 zinazoihusu timu ya Tanzania Prisons zilizokuwa zichezwe Januari
25 na 29 mwaka huu.
Awali
Tanzania Prisons ilitakiwa kutafuta uwanja mwingine wa kuchezea mechi
hizo dhidi ya Ruvu Shooting na JKT Ruvu kutokana na Uwanja wa Kumbukumbu
ya Sokoine kutokuwa tayari kwa Ligi Kuu ya Vodacom wikiendi hii.
Mechi hizo sasa zitachezwa kati ya Februari 6 na 8 mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya Sokoine.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
BREAKING NEWS! USAJILI WA OKWI YANGA WAADUNDA..
Kwa maana hiyo Okwi hataruhusiwa kucheza raundi ya pili ya Ligi Kuu ya Vodacom mpaka sakata lake la usajili kutoka klabu ya Etoile du Sahel litakapotafutiwa ufumbuzi.
credit :shafih dauda
ALICHOKISEMA TUNDA MAN KUHUSU YEYE NA ROSE NDAUKA KATIKA MAHUSIANO

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tunda Man, amesema mpenzi wake wa
kwanza katika maisha yake ni mwanadada muigizaji wa filamu nchini Rose
Ndauka,ambaye waliachana tangu
2006.Akizungumza na XXL ya Clouds Fm Tunda amesema walikuwa wakikutana na
mwanadada huyo katika studio moja huko kariakoo hali iliyowapelekea
kuanza mahusiano yao yamapenzi.
“Kuna studio moja kariakoo,wanadada walikuwa wanakuja kuchana na yeye
anakuja studio anaangalia situation zinavyoenda, kwahiyo kuanzia hapo
ndiyo akaanza kunijua nini, nikaenda kwao kila kitu kikawa fresh kila
kitu kikawa kinaenda poa ni 2006 kitu kama hicho, yani tumeachana kabla,
hamna hata mmoja aliyekuwa star, sasa tumejikuta kila mmoja anafanya
issue zake na mimi nafanya issue zangu, mpaka sasa hivi nikikutana nae,
nasikia ameolewa peace tu ,kama na shida na yeye kwasababu na yeye sasa
hivi anapiga mapigo ya movie na mimi na movie zangu kama vipi
namdondosha halafu namlipa”, alisema Tunda
Credit:-Bongo5
HII NDO KUFURU YA PESA YA MCHEZAJI..'SAMUEL ETO’O' HAYA NDIYO MAGARI YA KIFAHARI ANAYOMILIKI NA ANAYOPENDELEA

Eto'o hivi karibuni
ameonekana kutisha sana katika kabumbu analocheza huko ulaya. Tarehe 19
mwezi huu aliweka historia kubwa katika maisha yake kwa kupiga Hat trick
kwa kuifuna Manchester united bao 3-1 na kufanikiwa kunyakuwa mpira
kama zawadi.Pia Kati ya Vitu samwel Eto'o anavyovipenda katika maisha yake ni kuwa
na Magari ya Kifahari. Hayo hapochini ni baadhi ya Magari ya kifahari
anayomiliki mchezaji huyu mkameruni. Nukuu Eto'o said: "I
like to have a few cars because it gives me choice and it doesn't hurt
anybody. To give happiness, the first thing is to be happy oneself, and I
am."
![]() |
Maybach Xenatec Coupe worth £750,000
Aston Martin V12 Zagato, worth at £450,000
Bugatti Veyron worth at £1.55m
Credit:charleslimelight.blogKAMA ULIKUWA HUJUI HUYU NDIYE MMILIKI WA YANGA ALIYEAIBUKA, ATAKA KWENDA KWA KIKWETE

ALIYEJITANGAZA kuwa mmiliki wa klabu ya Yanga, Juma Mwambelo, amesema yu tayari kukabidhi nyaraka zinazotafutwa na uongozi wa klabu hiyo kwa Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, alitangaza kwenye mkutano wa Yanga kwamba Mwambelo anashikilia hati za umiliki wa klabu ya Yanga kimakosa na anatakiwa kuzikabidhisha haraka iwezekanavyo kabla ya kuchukuliwa hatua.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwombelo alisema yupo tayari kumpa Rais Kikwete naye aukabidhi uongozi wa Yanga chini ya Yusuf Manji.
“Kweli hati hizo ninazo kwa kuwa mimi ni mmiliki wa Klabu ya Yanga, ila Rais Kikwete pekee ndiye naweza kumkabidhi, hata mwanaye Ridhwani nimewahi kumueleza kuhusiana na hili,” alisema.
“Mimi ndiye mmiliki wa Klabu ya Yanga, nina hati miliki halali ya klabu, hii hapa (anaonyesha), nina hati miliki ya jengo la Jangwani, pia ninayo ya jengo la Mafia, lakini hiyo waliiba na tayari nilisharipoti polisi.
“Kuhusu hati ya jengo la Jangwani ipo benki na yenyewe sijailipia kwa kuwa kuna deni, deni hilo ni zile fedha ziliyotumika kujenga Uwanja wa Kaunda. Hivyo,
deni likilipwa benki itakubali kutoa hati kisha kuirudisha wizarani na kutolewa rasmi.
“Nashangaa Yanga wanapodai wanatumia katiba mpya, hii siyo halali, katiba halali ya Yanga ni ile ya mwaka 1967 ambayo nakala yake hii hapa (anaonyesha),” alisema.
Alipoulizwa juu ya uhalali wa wanachama wa sasa wa klabu hiyo, alisema: “Wanachama wengine wote ni feki, mpaka unatokea mgawanyiko mwaka 1975, wanachama halali wa Yanga walikuwa 400, kuanzia hapo hakuna wanachama halali tena, hata akaunti zinazotumika siyo za klabu.
“Hapa nilipo nimekuja polisi (Magomeni) ili kutoa taarifa ya kujihami, nahofia kupigwa kutokana na walichokisema kwenye mkutano,” alisema.
Katika mkutano mkuu wa Jumapili, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Karume, PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam, uongozi wa Yanga ulimtaja mzee Juma kuwa ndiye aliyeiiba hati ya jengo la klabu hiyo tangu Juni 24, 2009.
“Mimi nilipigwa na watu mwaka 1987 nikapoteza fahamu kwa siku tano, tangu pale sijawahi kwenda klabuni wala uwanjani kuitazama Yanga, hata huyo Mrisho Ngassa simjui, namuona tu kwenye magazeti, kikubwa ninachotaka ni utaratibu ufuatwe ndani ya Klabu ya Yanga,” alisisitiza huku akitabasamu.
source:gpl
Meli nyingine ya Titanic kutengenezwa nchini China kwa $164m - Bongo5
Kampuni ya Seven Star Energy Investment Group, yenye makazi yake jimboni Sichuan nchini
China itatumia dola milioni 164 kutengeneza meli inayofanana kila kitu la meli kama ya
Titanic (replica) iliyozama karne moja iliyopita.
Meli hiyo itajengwa na kampuni ya China Shipbuilding Industry Corporation na itatumika
kupamba park ya kaunti ya Daying iliyopo Sichuan kwa kuegeshwa kwenye mto Qi nchini China.
Meli hiyo haitatumika kusafirisha abiria na watalii kwenye kina kirefu cha bahari kwakuwa si
watu wengi wanaweza kuingia tena kwenye safari ya kufanana na Titanic ambayo haikukamilika.
Badala yake meli hiyo itakuwa alama ya mzuka wa Titanic.
Shirika la habari la Xinhua limesema meli hiyo itatengeneza hali ilivyokuwa pale meli hiyo
ya kufahari ilipogongana na mwamba wa barafu.
Ujenzi wa meli hiyo yenye urefu wa meta 270 unatarajia kumalizika baada ya miaka miwili.
Hii si mara ya kwanza kwa watu kutaka kutengeneza meli nyingine ya Titanic. Bilionea wa
Australia, Clive Palmer alitangaza kutengeneza
BARCELONA YATHIBITISHA KUTUMIA KIASI CHA PAUNDI MILIONI 495 KUUBORESHA UWANJA WA NOU CAMP.
Bodi ya wakurugenzi ya FC Barcelona
imekataa wazo la kujenga kiwanja kipya na badala yake wamekubaliana kuongeza
nguvu kuufanyia marekebisho uwanja wao wa Nou Camp.
Wanachama wa klabu ya FC Barcelona
ambao kimsingi ndio wamiliki wa timu hiyo watapewa nafasi ya kupitisha wazo hilo
la kuuboresha uwanja Wa Nou Camp kwa kupiga kura mnamo mwezi wanne mwaka huu
kwenye mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo.
Kama wazo hilo litapitishwa na
wanachama basi uwanja huo mkubwa kuliko viwanja vyote barani ulaya wenye uwezo
wa kuingiza mashabiki 98,000 kwasasa, utakuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki
105,000 na kusaidia kuongeza kipato kutokana na vyanzo vya uwanja huo.
Pia itakuwa fursa kwa mashabiki
kuweza kuwaona wachezaji nyota ulimwenguni kama vile Lionel Messi na Neymar.
Mradi huo ambao pia unahusisha
ujenzi wa kiwanja cha ndani cha mchezo wa kikapu pamoja na vitega ychumi
vingine vingi unataraji kuighalimu kiasi cha paundi milioni 495 ambazo ni sawa
na euro milioni 600.Kazi hiyo ya maboresho ya uwanja inataraji kuanza mwaka
2017 na inataria kumalizika mapema mwaka 2021.
Ili kufanikisha mradi huo Barcelona
inategemea kuchukua mkopo benki wa kiasi cha paundi milioni 165,pia inategemea
kupata kiasi cha paundi milioni 82 kutokana na haki za jina la uwanja huo na
kiasi kingine kilichobaki cha pesa kitatokana na vyanzo vilivyopo hivi sasa.
Raisi wa klabu hiyo Sandro Rosell
amesema wakati woote wa ujenzi michezo mbali mbali inayoihusu klabu hiyo
itaendelea kuchezwa kwenye uwanja huo. #Exclusive: Unataka kuona mshindi wa BSS 2013 amezitumiaje milioni 50 zake? picha za alivyovifanya ziko hapa
Unaambiwa kabla ya hapo, Msuya hakuwahi kushika au kumiliki zaidi ya shilingi laki tano… yani aliwahi kupata shilingi laki tano mara moja tu siku alipolipwa pesa ya miezi mitatu iliyotokana na mkataba wa kuifundisha na kuisimamia Kwaya ya KKKT kucheza ili ikafanye video.
Mambo matatu makubwa aliyoyafanya kwa hizi milioni 50 za ushindi wa BSS…. >>> Msuya amenunua nyumba ya milioni 17 nyumbani kwao Musoma mjini kama unavyoiona hapa chini kwenye picha, amenunua hili gari lenye thamani ya milioni 9, amejenga studio hiyo hapo juu kwenye picha ambayo imegharimu milioni 12 na tayari ameshapata nyumba ya kufanyia biashara ya Stationary Musoma Mjini.
Jaguar Kioo (Official Video) Main Switch
PICHA:UZINDUZI WA MREMA CUP 2014 TIMU 14 KUUMANA
Mbunge wa vunjo Dkt Austino Mrema alipokuwa akizindua mashindano ya Mrema cup ambayo anayadhamini yeye ambayo yanashirikisha timu 15 kutoka jimbo hilo.
Mh Mrema akisalimiana na vijana na kukagua timu ya himo na njia panda katika mechi ya ufunguzi iliyofanyika katika viwanja vya Himo,wilaya ya moshi mkoani Kilimanjaro
PICHA:MH JUMA NKAMIA ALIVYOPOKELEWA KWENYE KITUO CHAKE KIPYA CHA KAZI KAMA NAIBU WAZIRI WA MICHEZO,
Naibu katibu mkuu wa wizara ya habari,vijana utamaduni wa michezo Prof.Elisante Olegabriel akimkaribisha Naibu wa wizara ya habari vijana,utamaduni na michezo Mheshimiwa Juma Nkamia katika tukio la kumkaribisha lilifanyika leo jijini dar es salaam leo.
Waziri wa Habari wizara ya habari vijana,utamaduni na michezo Mheshimiwa Dkt Fenela Mukangara akimkaribisha Juma Nkamia katika ofisi za wizara zilizopo katika jengo la mfuko wa pensheni wa PSPF jijini Dar es salaam leo
Picha:mbalimbali ikiwemo ya Baa iliyo ndani ya ndege ya Emirates.

Mpaka mwaka 2010, wanasema Emirates walikua wanasafirisha abiria elfu mbili mia nne kwa wiki kutoka Dubai International Airport kwenda kwenye majiji 105 ndani ya nchi 62 duniani ambazo ziko ndani ya mabara sita.
Mpaka mwaka 2010 pia, Emirates walikua wameajiri Wafanyakazi elfu kumi na mia saba wanaotoka kwenye nchi mia moja ishirini duniani na kwenye kutimiza kwao miaka 25, walitangaza faida yao iliyofikia dola za kimarekani milioni 964.
Unaambiwa Terminal 3 kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Dubai ambayo ilianza kutumika mwaka 2008 baada ya kujengwa maalum kwa ajili ya kutumiwa na shirika hili la Emirates peke yake, iligharimu dola za Kimarekani bilioni 4.5 ikiwa ni jengo lililotajwa mwaka 2010 kuwa kubwa kwa kipimo cha upana likiwa na over 1,500,000 sq. m. (370 acres) of space.
Picha zinazofata hapa chini ndio zinaonyesha baa ambayo iko ndani ya Emirates Airline



source:milardayo.com
HUU NDIO UTAFAUTI ULIOPO KATI YA GARI YA GHARMA YA LADY JAY DEE NA GARI YA GHARAMA YA DIAMOND NI HUU HAPA
![]() |
NDINGA YA JIDE HII |
5 reasons to buy Land Rover Range Rover Evoque
5 reasons to buy Toyota Land Cruiser V8 200
Engine and transmission | ||
More cylinders | 8 vs 4 | 4 more cylinders. The more cylinders = the less vibration and the engine runs more smoothly. |
More engine power | 286 bhp vs 236 bhp | 17% or 50 bhp More power of car = more top speed. |
Fuel consumption | ||
Less fuel consumption (Combined cycle) | 27.7 mpg vs 33.71 mpg | 22% or 6.01 mpg |
Weight and capacity | ||
More capacity of fuel tank | 93 liters vs 70 liters | 25% or 23 liters |
More maximum towing weight with brakes | 3500 kg vs 1800 kg | 49% or 1700 kg |
Neutral reasons Land Rover Range Rover Evoque vs. Toyota Land Cruiser V8 200
Engine and transmission | ||
Engine capacity | 1999 cm3 vs 4461 cm3 | 55% or 2462 cm3 less |
Fuel supply | Direct fuel injection with turbocharging vs COMMON RAIL | |
Turbocharging | Yes vs Yes | |
Dimensions | ||
Length | 4365 mm vs 4950 mm | 12% or 585 mm shorter |
Width | 2125 mm vs 1970 mm | 7% or 155 mm wider |
Height | 1635 mm vs 1865 mm | 12% or 230 mm lower |
Wheels and tires | ||
Wheelbase | 2660 mm vs 2850 mm | 7% or 190 mm less |
YALIYOJIRI JANA KWENYE KUAPISHWA KWA MAWAZIRI

MAWAZIRI na manaibu waziri walioteuliwa kushika
nafasi mbalimbali jana waliapishwa na Rais Jakaya Kikwete katika viwanja
vya Ikulu jijini Dar es Salaam, huku baadhi yao wakianza na tambo za
uwajibikaji na wengine wakiomba ushirikiano wa karibu kutoka kwa wadau
ili waweze kutimiza majukumu yao.
Rais
Kikwete na Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani
wakiwa na wakuu wa vyombo vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Wakizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya mawaziri hao, Saada
Mkuya Salum (Wizara ya Fedha na Uchumi), Juma Nkamia (Naibu Waziri
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo) na Dk. Asha-Rose Migiro
(Wizara ya Katiba na Sheria), kila mmoja aliomba ushirikiano kutoka kwa
wadau na Watanzania kwa ujumla.
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, alisema changamoto ya kwanza atakayokabiliana nayo ni kuimarisha eneo la fedha ili nchi iweze kujitegemea na kuwabeza wanaomwita ‘waziri mzigo’, wasubiri waone utendaji wake.
Akizungumzia suala la mishahara ya wafanyakazi, alisema kama kuna upungufu uliojitokeza kipindi cha nyuma kwa mishahara kuchelewa, halitajirudia na kwamba mishahara itatolewa kwa wakati husika.
Alisema wanachotarajia kufanya kama wizara ni kuimarisha mapato ya ndani ili kuweza kuondokana na utegemezi wa mataifa mengine, hasa katika miradi ya ndani.
Alisema lazima serikali ijielekeze katika kupata miundombinu ya kiuchumi kwa ajili ya kuondoka katika hatua ya sasa na kuelekea hatua nyingine.
Aliongeza kuwa wakati wa uhai wa William Mgimwa, kuna mipango mingi ya kimaendeleo waliyofanya na kuahidi kuitekeleza kwa nafasi yake mpya ya uwaziri.
“Mimi sijui dhana ya kuitwa mizigo ina tafsiri gani, ninachojua ni kuwa Katibu Mkuu wetu, Kinana, alikuwa mikoani na wananachi walikuwa wanalalamikia baadhi ya mambo, hivyo ilikuwa ni wajibu wake kutuita na kupata ufafanuzi wa yale yaliyokuwa yanalalamikiwa na wananchi na si kwamba sisi ni mizigo,” alisema Mkuya.
Mwigulu aahidi kupambana na fedha chafu
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi (Sera), Mwigulu Nchemba, amesema jambo la msingi atakalolitilia mkazo ni udhibiti wa fedha chafu na kwamba hiyo ni moja ya sekta iliyo katika Benki Kuu.
Alisema taasisi za kifedha zitafanya uchambuzi wa kitaalamu na kisha kuwasilisha bungeni mipango dhabiti ya kuwabana watu wanaotafuta njia ya kusafisha fedha haramu.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro, alisema alipokuwa nje ya majukumu ya kiserikali amejifunza mengi ambayo atayatumia katika majukumu yake ya sasa, huku akieleza kuwa uzalendo utatawala katika suala zima la upatikanaji wa Katiba mpya.
Alisema hataruhusu hisia za kichama zitawale katika kuwapatia Watanzania katiba waitakayo, kwa kile alichoeleza kuwa mchakato wa katiba unamhusu kila Mtanzania pasipo kuangalia itikadi yake ya chama.
Nkamia alilia ushirikiano kwa waandishi
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia, kwa upande wake alisema pasipo ushirikiano kutoka kwa wadau wasitegemee miujiza katika sekta nzima ya habari.
“Naomba kila mmoja wetu kwa nafasi yake ashiriki na tushirikiane, katika hili hakuna muujiza utakaofanywa na mtu mmoja, hasa ninyi ndugu zangu waandishi ni nguzo muhimu katika kutoa ushirikiano, naomba tushirikiane,” alisema Nkamia.
Mwanza waponda
Naye mwandishi, Sitta Tumma, kutoka Mwanza, anaripoti kuwa baadhi ya wananchi wakiwemo wanasiasa jijini Mwanza na mjini Musoma, mkoani Mara, wameponda na kubeza uteuzi huo, ambapo wameuita ni mtindo wa kupeana fadhila na kutesa kwa zamu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya wananchi na wanasiasa hao walisema baraza hilo ni mzigo usiobebeka kwa wananchi, na Rais Kikwete amejitwisha mzigo ambao hatima yake ni kiama kwa taifa, kwani Watanzania walitarajia kuona mawaziri wawajibikaji, na si watu wa kutafuta fedha za uchaguzi mwaka 2015.
Walieleza kushangazwa na kuingizwa wizarani Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, ambaye amepewa Unaibu Waziri wa Fedha (Sera), Dk. Titus Kamani (Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi), Shukuru Kawambwa (Wizara nyeti ya Elimu), Hawa Ghasia (TAMISEMI), Juma Nkamia (Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo), Profesa Anna Tibaijuka (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Lazaro Nyalandu (Wizara ya Maliasili na Utalii), pamoja na Mathias Chikawe kupewa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti mstaafu wa CCM Wilaya ya Nyamagana, jijini hapa, Athumani Zebedayo, alieleza kushangazwa na hatua ya Rais Kikwete kumbakisha serikalini Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa na mawaziri wengine mizigo waliotakiwa na CCM kuondolewa.
Alisema kuachwa kwa mawaziri hao kunatia shaka iwapo kuna dhamira ya kweli ya kuwasaidia wananchi kupata maendeleo yaliyodumaa, na kwamba ni maajabu pia kuingizwa katika baraza hilo, Nchemba, Dk. Kamani, Ghasia, Chikawe, Nyalandu, Tibaijuka na Nkamia, kwani watu hao hawawezi kuwasaidia wananchi maskini.

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, alisema changamoto ya kwanza atakayokabiliana nayo ni kuimarisha eneo la fedha ili nchi iweze kujitegemea na kuwabeza wanaomwita ‘waziri mzigo’, wasubiri waone utendaji wake.
Akizungumzia suala la mishahara ya wafanyakazi, alisema kama kuna upungufu uliojitokeza kipindi cha nyuma kwa mishahara kuchelewa, halitajirudia na kwamba mishahara itatolewa kwa wakati husika.
Alisema wanachotarajia kufanya kama wizara ni kuimarisha mapato ya ndani ili kuweza kuondokana na utegemezi wa mataifa mengine, hasa katika miradi ya ndani.
Alisema lazima serikali ijielekeze katika kupata miundombinu ya kiuchumi kwa ajili ya kuondoka katika hatua ya sasa na kuelekea hatua nyingine.
Aliongeza kuwa wakati wa uhai wa William Mgimwa, kuna mipango mingi ya kimaendeleo waliyofanya na kuahidi kuitekeleza kwa nafasi yake mpya ya uwaziri.
“Mimi sijui dhana ya kuitwa mizigo ina tafsiri gani, ninachojua ni kuwa Katibu Mkuu wetu, Kinana, alikuwa mikoani na wananachi walikuwa wanalalamikia baadhi ya mambo, hivyo ilikuwa ni wajibu wake kutuita na kupata ufafanuzi wa yale yaliyokuwa yanalalamikiwa na wananchi na si kwamba sisi ni mizigo,” alisema Mkuya.
Mwigulu aahidi kupambana na fedha chafu
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi (Sera), Mwigulu Nchemba, amesema jambo la msingi atakalolitilia mkazo ni udhibiti wa fedha chafu na kwamba hiyo ni moja ya sekta iliyo katika Benki Kuu.
Alisema taasisi za kifedha zitafanya uchambuzi wa kitaalamu na kisha kuwasilisha bungeni mipango dhabiti ya kuwabana watu wanaotafuta njia ya kusafisha fedha haramu.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro, alisema alipokuwa nje ya majukumu ya kiserikali amejifunza mengi ambayo atayatumia katika majukumu yake ya sasa, huku akieleza kuwa uzalendo utatawala katika suala zima la upatikanaji wa Katiba mpya.
Alisema hataruhusu hisia za kichama zitawale katika kuwapatia Watanzania katiba waitakayo, kwa kile alichoeleza kuwa mchakato wa katiba unamhusu kila Mtanzania pasipo kuangalia itikadi yake ya chama.
Nkamia alilia ushirikiano kwa waandishi
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia, kwa upande wake alisema pasipo ushirikiano kutoka kwa wadau wasitegemee miujiza katika sekta nzima ya habari.
“Naomba kila mmoja wetu kwa nafasi yake ashiriki na tushirikiane, katika hili hakuna muujiza utakaofanywa na mtu mmoja, hasa ninyi ndugu zangu waandishi ni nguzo muhimu katika kutoa ushirikiano, naomba tushirikiane,” alisema Nkamia.
Mwanza waponda
Naye mwandishi, Sitta Tumma, kutoka Mwanza, anaripoti kuwa baadhi ya wananchi wakiwemo wanasiasa jijini Mwanza na mjini Musoma, mkoani Mara, wameponda na kubeza uteuzi huo, ambapo wameuita ni mtindo wa kupeana fadhila na kutesa kwa zamu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya wananchi na wanasiasa hao walisema baraza hilo ni mzigo usiobebeka kwa wananchi, na Rais Kikwete amejitwisha mzigo ambao hatima yake ni kiama kwa taifa, kwani Watanzania walitarajia kuona mawaziri wawajibikaji, na si watu wa kutafuta fedha za uchaguzi mwaka 2015.
Walieleza kushangazwa na kuingizwa wizarani Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, ambaye amepewa Unaibu Waziri wa Fedha (Sera), Dk. Titus Kamani (Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi), Shukuru Kawambwa (Wizara nyeti ya Elimu), Hawa Ghasia (TAMISEMI), Juma Nkamia (Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo), Profesa Anna Tibaijuka (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Lazaro Nyalandu (Wizara ya Maliasili na Utalii), pamoja na Mathias Chikawe kupewa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti mstaafu wa CCM Wilaya ya Nyamagana, jijini hapa, Athumani Zebedayo, alieleza kushangazwa na hatua ya Rais Kikwete kumbakisha serikalini Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa na mawaziri wengine mizigo waliotakiwa na CCM kuondolewa.
Alisema kuachwa kwa mawaziri hao kunatia shaka iwapo kuna dhamira ya kweli ya kuwasaidia wananchi kupata maendeleo yaliyodumaa, na kwamba ni maajabu pia kuingizwa katika baraza hilo, Nchemba, Dk. Kamani, Ghasia, Chikawe, Nyalandu, Tibaijuka na Nkamia, kwani watu hao hawawezi kuwasaidia wananchi maskini.
(CHANZO NI TANZANIA DAIMA/ PICHA NA IKULU)
Subscribe to:
Posts (Atom)
Popular Posts
-
SANAMU YA CRISTIANO RONALDO ILIYOZINDULIWA JANA
-
PICHA:hivi ndivyo viwanja kumi na mbili vya kombe la dunia 2014 Brazil
-
PICHA 8: MJI WA PONGWE CITY TANGA UTAKAVYOKUWA NI NOMAA
-
Picha 17 za Diamond hapa South Africa jinsi ilivyokua akirekodi kolabo na Mafikizolo
-
MITINDO YA NYWELE KWA AKINA DADA AMAIZING!!!!!!!!!!!!!!
-
ROSTAM KUUZA HISA ZAKE VODACOM
-
hili ndilo Tamko la TFF kuhusu tiketi za Ki-elektoniki.
-
picha 8 jinsi vurugu za mashabiki wa simba na yanga zilizopelekea mashabiki kungoa viti
-
picha: gari jipya la Jux mwimbaji wa bongofleva? picha 14 ziko hapa
-
RAIS MPYA WA ZAMBIA KATIKA SHEREHE ZA KUAPISHWA MATUKIO KATIKA PICHA
Total Pageviews
Blogger news
NANI MSANII KATI YA HAWA NDO MSANII MKALI TANZANIA KWA SASA
Translate
Blog Archive
-
►
2015
(43)
- ► 06/14 - 06/21 (1)
- ► 04/26 - 05/03 (1)
- ► 02/08 - 02/15 (8)
- ► 02/01 - 02/08 (8)
- ► 01/25 - 02/01 (12)
- ► 01/18 - 01/25 (2)
- ► 01/11 - 01/18 (8)
- ► 01/04 - 01/11 (3)
-
▼
2014
(369)
- ► 12/28 - 01/04 (3)
- ► 12/21 - 12/28 (1)
- ► 11/16 - 11/23 (2)
- ► 09/07 - 09/14 (5)
- ► 08/10 - 08/17 (3)
- ► 07/20 - 07/27 (1)
- ► 07/06 - 07/13 (2)
- ► 06/22 - 06/29 (4)
- ► 06/15 - 06/22 (2)
- ► 06/08 - 06/15 (16)
- ► 06/01 - 06/08 (18)
- ► 05/25 - 06/01 (25)
- ► 05/18 - 05/25 (15)
- ► 05/11 - 05/18 (10)
- ► 05/04 - 05/11 (20)
- ► 04/27 - 05/04 (11)
- ► 04/20 - 04/27 (1)
- ► 04/06 - 04/13 (2)
- ► 03/30 - 04/06 (3)
- ► 03/23 - 03/30 (2)
- ► 03/02 - 03/09 (14)
- ► 02/23 - 03/02 (28)
- ► 02/16 - 02/23 (9)
- ► 02/09 - 02/16 (33)
- ► 02/02 - 02/09 (35)
- ► 01/26 - 02/02 (29)
-
▼
01/19 - 01/26
(44)
- LULU APEWA USHAURI MZITO NA SINTA BAADA YA KUPATA ...
- Tattoo za wasanii wa bongo na maana zake
- Hili ndilo jumba jipya la Rick Ross, lina vyumba 106
- picha: gari jipya la Jux mwimbaji wa bongofleva? p...
- HUYU NDO BAUNSA WA DIAMOND MWENYE KITAMBI..ANAYE K...
- HIVI NDIVYO AFRICA INAPIGA MAENDELEO Hii ndo aina ...
- NJE YA BOX - Joh Makini, Nikki wa II, Gnako
- Hizi ndio taarifa rasmi za Rais wa Barcelona kuj...
- PICHA NA HABARI WAZIRI MKUU MSTAAFU SUMAYE ALIPOTE...
- PICHA:DK MAGUFULI AHAMIA MOROGORO KUSIMAMIA UJENZI...
- Roma atoa sababu za kwanini hutoa wimbo mmoja kwa ...
- PICHA DIAMOND :NAIROBI,NAIROBI!!!TODAY I WILL BE T...
- HII NDO JEURI YA PESA YA MWANAMUZIKI KOFFI OLOMIDE...
- MCHUMBA WA LULU SI SIRI TENA! MAMA YAKE AKUBALI AO...
- HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA MANCHESTER CHELSEA W...
- BREAKING NEWS! KATIBU MKUU MPYA WA SIMBA NI EZEKIE...
- Picha 7 za kitakachoonekana ktk video mpya ya Weus...
- HII NDIO PICHA YA MPENZI WA MMILIKI WA CLUB YA CHE...
- REAL MADRID YAINGIA KWENYE MBIO ZA KUMSAJILI ROONEY.
- OFFICIAL: TFF YAZUIA USAJILI WA EMMANUEL OKWI YANGA
- BREAKING NEWS! USAJILI WA OKWI YANGA WAADUNDA..
- ALICHOKISEMA TUNDA MAN KUHUSU YEYE NA ROSE NDAUKA ...
- PICHA ZA KICHUPA KIPYA CHA JOH MAKINI FT NIKI WA P...
- HII NDO KUFURU YA PESA YA MCHEZAJI..'SAMUEL ETO’O'...
- KAMA ULIKUWA HUJUI HUYU NDIYE MMILIKI WA YANGA ALI...
- Meli nyingine ya Titanic kutengenezwa nchini China...
- PICHA : PETER OKOYE WA PSQURE AKIWA NA MWANAE WA K...
- BARCELONA YATHIBITISHA KUTUMIA KIASI CHA PAUNDI MI...
- #Exclusive: Unataka kuona mshindi wa BSS 2...
- Jaguar Kioo (Official Video) Main Switch
- PICHA:UZINDUZI WA MREMA CUP 2014 TIMU 14 KUUMANA ...
- PICHA:MH JUMA NKAMIA ALIVYOPOKELEWA KWENYE KITUO C...
- PICHA:HII NDIYO NDEGE ANAYOMILIKI JAGUAR MSANII W...
- Picha:mbalimbali ikiwemo ya Baa iliyo ndan...
- HUU NDIO UTAFAUTI ULIOPO KATI YA GARI YA GHARMA Y...
- HUWEZI AMINI...KAMA HUYU NDO MAMA WA RAIS WA MALA...
- YALIYOJIRI JANA KWENYE KUAPISHWA KWA MAWAZIRI ...
- PICHA : 2face Idibia amwonyesha mwanae aliempata...
- MAKALA:JOSE MOURINHO NA VIBONDE WAKE MAN UNITED: ...
- PICHA:YANGA IMEKAMILISHA ZIARA YA UTURUKI KWA KUF...
- Picha: P-Square wanunua mijengo miwili ya kifaha...
- Picha: Lady Jaydee auonesha mkoko wake mpya ...
- huu ndo ujumbe mfupi aliyouandika mtangazi wa BB...
- Haya ndio mabadiliko yaliyofanywa na Rais...
- ► 01/12 - 01/19 (16)
- ► 01/05 - 01/12 (15)
-
►
2013
(116)
- ► 12/29 - 01/05 (5)
- ► 12/22 - 12/29 (9)
- ► 12/15 - 12/22 (20)
- ► 12/08 - 12/15 (45)
- ► 12/01 - 12/08 (25)
- ► 11/24 - 12/01 (11)
- ► 11/17 - 11/24 (1)
0 comments: