Roma atoa sababu za kwanini hutoa wimbo mmoja kwa mwaka


  
Rapper Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki& amesema kile kinachoonekanan kama
 ukimya wake kinatokana na desturi aliyojiwekea tangu aanze muziki wa kutoa wimbo mmoja
 kwa mwaka.

Akizungumza na Bongo5 leo, Roma amesema ukiona yupo kimya katika muziki ujue anafanya 
shughuli za kiujasiriamali ambazo ni tofauti na muziki.
Mwaka jana hakukuwa na kimya chochote kwa mtu anayemjua Roma kwa miaka yote,
amesema Roma. Roma kwa mwaka anatoaga wimbo moja. Kwahiyo mtu yoyote ambaye ana ‘judge’ 
kwanini Roma alikuwa kimya, ujue huyo kamjua Roma juzi.2007 ilitoka nyimbo ya kwanza, 2008
 nyimbo ya pili, na nyimbo sita, kwahiyo kila mwaka natoaga nyimbo moja,sijawahi kutoa
 nyimbo mbili kwa mwaka. Kwa mwaka jana ni 2030. Nilikuwa kimya kwasababu ndio nyimbo 
iliyokuwa inachezwa.Na mwaka huu nitatoa nyimbo moja nanitakuwa kimya mpaka mwakani ndio 
kawaida ya Roma.
Nimeandaa nyimbo kama sita ndani ya ‘Tongwe records’ sema ni kuchagua nitoe nyimbo gani 
kwa mwaka huu. Sema nilikuwa kimya kidogo kutokana na majukumu ya maisha.Kama kawaida ya 
Roma ni nyimbo moja kwa mwaka, hata  wimbo wangu 2030 ulitoka 28/12/2012. Lakini wimbo huu 
ni wa mwaka 2013 ndio maana ulipata air time nzuri 2013,” aliongeza.
Katika hatua nyingine, Roma amesema mwaka huu anatarajia kurudi shule baada ya kuhitimu na 
kushindwa kuendelea kutokana na muziki.
Mimi ni mjasiriamali pia najarajia kurudi shule hivi karibuni,kwasababu nilihitimu 
nikashindwa kuendelea,ila mwaka huu nadhani suala la kurudi shule ni miongoni mwa mikakati 
yangu kwa mwaka huu.

0 comments:

PICHA DIAMOND :NAIROBI,NAIROBI!!!TODAY I WILL BE THERE BABY

0 comments:

HII NDO JEURI YA PESA YA MWANAMUZIKI KOFFI OLOMIDE BAADA YA KUNUNUA GARI LA KIFAHARI LA BEI MBAYA

Ukiwataja wanamuziki matajiri basi Koffi ni mmoja wao, akiwa anamiliki 5 Star Hotel na akiwa na hisa kwenye kampuni kadhaa ndani ya Congo na nje ya Congo Koffi anaorodheshwa kuwa ni mmoja wa wanamuziki ambao wamefaidika vilivyo na muziki wao.

Majuzi Koffi aliingiza gari mpya Model ya 2012 aina ya Rolls Royce Phantom na kuitambiulisha kwa mashabiki.

Pichani Koffi Olomide akiwa mbele ya gari yake. Koffi ametangaza kung’atuka kwenye shughuli ya Muziki baada ya kutoa albamu yake mpya ambayo iko studio kwa sasa, Hii itakuwa ni Albamu ya 20 ya mwanamuziki huyu ambaye anamaliza akiwa na mafanikio na mpaka sasa albamu zake tatu zimeorodheshwa kwenye listi ya albamu 1000 ambazo unapaswa kusikiliza kabla ya kuondoka duniani (kufariki).

0 comments:

MCHUMBA WA LULU SI SIRI TENA! MAMA YAKE AKUBALI AOLEWE,MAMA KANUMBA ACHEKELEA:


HAYAWIHAYAWI hatimaye yamekua! Siku chache baada ya sexy lady wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ kutangaza sifa za mwanaume atakayemchumbia,
amejitokeza mtu anayetaka kuchukua jumla na si siri tena, Amani limenyetishiwa.
Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
SIFA ZAKE
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa familia ya staa huyo anayekimbiza sokoni na filamu yake ya Foolish Age, mchumba huyo anaitwa Johnson lakini ni maarufu kwa jina la JR na pia ni Mkristo kama ilivyo kwa Lulu.

JR ni mfanyabiashara kigogo wa jijini Dar mwenye ‘mahela’ ya kufa mtu.
Pia mchumba huyo ni bosi wa kampuni kubwa ya uandaaji, usambazaji wa kazi za sanaa Bongo.

ALISHAKWENDA KWA AKINA LULU
“Kwa taarifa yenu, tayari JR anafahamika vizuri kwa akina Lulu kwani alishakwenda kujitambulisha na kuna maneno kwamba ndiye aliyempangia nyumba kubwa, Tegeta jijini Dar.

“Unajua yule jamaa aliona fursa akaitumia. Baada ya Lulu kutoka mahabusu kwa matatizo ya kifo cha mwandani wake, Steven Kanumba ndipo JR akafanya juu chini kumnasa hadi akafanikiwa,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Muda siyo mrefu zitasikika cherekochereko za Lulu kuolewa.
“Ukweli ni kwamba hata mama Lulu (Lucresia Karugila) amemkubali yule mchumba kwani ndiye anayemfanya Lulu aonekane kama alivyo kwa sasa.

“Sasa hivi Lulu anaishi kwenye bonge la nyumba kule Tegeta (Dar) na suala la usafiri si ishu. Anabadili tu magari. Kusema kweli kwa sasa bidada mambo yamemwendea vizuri.
“Anachoogopa tu yasitokee kama yale ya Clement wa Wema Sepetu.”

AMANI LASAKA WAHUSIKA
Baada ya kumwagiwa upupu huo, gazeti hili liliwasaka wahusika mmoja baada ya mwingine ili kupata mbivu na mbichi za ishu hiyo.

Mama Lulu, Lucresia Karugila.
MAMA LULU
Kwa kuwa ni jambo la kifamilia, gazeti hili lilipozungumza na mama Lulu, Lucresia Karugila alisema si jambo baya kwa mwanaye kuwa na mchumba hivyo anamkubali (huyo mchumba) huku akiweka wazi kuwa hana kipingamizi chochote.
Alipoulizwa jina la mwanaume huyo na kwamba ni kigogo mwenye fedha nyingi, mzazi huyo alitoa ruksa aulizwe Lulu mwenyewe. “Mimi sina sababu ya kumkataa mwanaume ambaye wamekubaliana na mwanangu, kikubwa ni makubaliano, namkubali,” alisema mama Lulu. HUYU HAPA LULU
Kwa upande wake Lulu mambo yalikuwa hivi;
Amani: Mambo vipi Lulu?
Lulu: Poa, naongea na nani?
Amani: (akatajiwa jina la mwandishi) kwanza hongera kwa kupata mchumba.
Lulu: Nani kawaambia?
Amani: Kwa kazi yetu hii hatushindwi kujua. Je, ni kweli umepata mchumba?
Lulu: Ndiyo lakini nisingependa sana kulizungumzia hilo.
Amani: Anaitwa nani?
Lulu: Siwezi kumtaja leo (Jumanne iliyopita). Nitawatajia tu ninyi subirini. Itakuwa surprise (mshangao), siku si nyingi nitamuanika.
Amani: Je, ni kweli ni maarufu kwa jina la JR? Au wewe tutajie hata jina la mwanzo tu.
Lulu: Nimeshasema jamani nitawatajia kwani ninyi mna haraka gani?
Amani: Je, ni kweli ni mmiliki wa kampuni ya burudani? (anatajiwa kampuni).
Lulu: Hayo yote yatafahamika kwenye utambulisho. Naomba niishie hapo ‘coz’ sina cha zaidi kuhusu ishu hiyo jamani subirini siku si nyingi.
MAMA KANUMBA
Baada ya kujiridhisha kuwa sasa Lulu ana mchumba rasmi, ‘kijumbe’ wetu alimfikishia taarifa aliyekuwa mama mkwe wa staa huyo wakati akiwa na Kanumba, mama Kanumba, Flora Mtegoa ili naye atie neno.
Mama Kanumba hakuwa na kipingamizi juu ya suala hilo zaidi ya kuchekelea huku akiweka wazi kuwa Lulu kwa sasa anaweza kuolewa.
“Mimi sina tatizo kabisa, namjua. Lulu anaweza kuolewa na nimempa baraka zote,” alisema mama Kanumba ambaye kwa sasa ni shosti mkubwa wa mama Lulu.
JR SASA
Hata hivyo, gazeti hili halikuishia hapo kwani lilisaka namba ya simu ya kiganjani ya mwanaume huyo ambapo ilipopatikana, alipigiwa, mambo yakawa hivi:
Amani: Habari yako mkuu JR?
JR: Safi, nikusaidie nini?
Amani: Mimi…(akatajiwa jina la mwandishi na kampuni) wewe ndiye JR mmiliki wa kampuni ya…(anatajiwa jina la kampuni).
JR: Kwanza mimi siyo JR ni GR. Huyo JR ni mdogo wangu.
Amani: Mbona sisi tumetajiwa JR ambaye anamiliki kampuni ya...(anatajiwa tena jina la kampuni).
JR: Oke, ndiyo mimi nikusaidie nini?
Amani: Taarifa tulizonazo ni kwamba una uhusiano na Lulu? Yaani wewe ndiye mchumba wake?
JR: Ndiyo, sitaki maswali (tusi na kukata simu).
Tangu kitokee kifo cha Kanumba ambaye alikuwa na uhusiano wa siri na Lulu, bidada huyo hajawahi kuwa na mwanaume hadi huyo mchumba aliyejitokeza.

credit:Boss ngasa

0 comments:

HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA MANCHESTER CHELSEA WAKUBALI OFA YA £37M KUTOKA MAN UNITED KWA AJILI YA MATA - KUFANYIWA VIPIMO LEO



Ofa ya Manchester United ambayo inaaminika kuwa kiasi cha £37m, imekubaliwa na klabu ya Chelsea kwa ajili ya usajili kiungo wa kihispania Juan Mata.

Kiungo mwenye miaka 25 atafanyiwa vipimo vya afya leo Alhamisi kabla ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na mabingwa hao wa EPL.

Mata anategemewa kusaini mkataba wa miaka minne na nusu wa kuwepo Old Trafford.

Mhispania huyo, ambaye alikuwa mchezaji bora wa Chelsea katika misimu miwili iliyopita, aliwaaga wachezaji wenzie jana Jumatano katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea - Cobham.

United hata hivyo wameendelea kukaa kimya kuhusu uthibitisho wa dili hilo huku kocha wa klabu hiyo akikataa kujibu swali kumhusu Mata baada ya kipigo kutoka kwa Sunderland katika nusu fainali ya kombe la ligi.

Waandishi wa habari walikuwa wametaarifiwa kabla ya mkutano wa baada ya mechi kwamba Moyes atajibu maswali kuhusu mechi tu na baadae walipojaribu kumuuliza kuhusu Mata, kocha huyo mscotish alijibu: "Hatusemi kitu chochote kuhusu hilo jambo."

Ikiwa uhamisho huo utakamilika basi United watakuwa wamevunja rekodi ya ada ya usajili ya klabu hiyo - walilipa kiasi cha £30.75m kwa Spurs kwa ajili ya kumsaini  Dimitar Berbatov  September 2008.
source:shafih dauda 

0 comments:

BREAKING NEWS! KATIBU MKUU MPYA WA SIMBA NI EZEKIEL KAMWAGA,HAFISA HABARI NI ASHA MUHAJI




Uongozi wa klabu ya Simba umempandisha cheo  aliyekuwa hafisa habari wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga na kuwa katibu mkuu mpya, Kamwaga anachukua nafasi ya Evodius Mtawala aliyepata ajira akiwa kama mkurugenzi wa kitengo cha wanachama na sheria pale TFF.

Klabu ya Simba pia imemteua mwandishi mkongwe wa habari za michezo Asha Muhaji kuwa hafisa habari mpya wa klabu hiyo.

credit:shafih dauda

0 comments:

Picha 7 za kitakachoonekana ktk video mpya ya Weusi ‘nje ya box’ manka wa kichaga

Screen Shot 2014-01-22 at 9.38.51 PMUnaambiwa Ijumaa hii ya January 24 2014 ndio video hii itawafikia mamilioni ya Watanzania manake ndio siku ya kuachiwa kwake ikiwa imefanywa na mkali kutoka 87.9 Arusha >> Nisher.
Mwezi wa kwanza wa 2014 tayari umemilikiwa na video za wasanii kama Diamond, Chege, Madee, Makomando na sasa wanafata Weusi na ‘nje ya box’ ambayo hizi ni baadhi tu ya picha za kitakachoonekana ndani yake.

5
4
3
2

1

0 comments:

HII NDIO PICHA YA MPENZI WA MMILIKI WA CLUB YA CHELSEA ROMANI ABRAMOVICH ALIVYOMDHALILISHA MREMBO HUYU MWEUSI

[clip_image001%255B5%255D.jpg]

 
Hii ni dhahiri kabisa kuwa bado ubaguzi wa rangi uko ndani ya damu za watu weupe
dhidi ya watu wenye asili ya Kiafrika, Tumeshaona matukio mengi ya ubaguzi wa rangi katika nyanja mbalimbali,

0 comments:

REAL MADRID YAINGIA KWENYE MBIO ZA KUMSAJILI ROONEY.


Taarifa kutoka jijini Madrid zinasema mshambuliaji Wayne Rooney ameingia kwenye orodha ya washambuliaji wanaowataka mwishoni mwa msimu.
Huku mkataba wa Rooney ukiwa umebaki miezi 18 na inavyoelekea hana nia ya kuongeza mkataba mpya  pia klabu ya Manchester Utd haipo tayari kumuuza Rooney kwa vilabu vya England.
Kwenye orodha ya majina ya washambuliaji wanaotakiwa na Real Madrid ukiacha jina la Rooney ni Radamel Falcao na Kun Aguero
Sababu inayompa nafasi kubwa Rooney kusajiliwa na Madrid ni uwezo wake kucheza nafasi mbali mbali ukiacha nafasi ya ushambuliaji pia kocha wa sasa wa Madrid Carlo Anceletti anamfahamu vizuri katika kipindi alichokuwa anaifundisha Chelsea.
Kama Rooney atafanikiwa kujiunga na Madridi msimu ujao basi atajiunga tena na mshambuliaji Cristiano Ronaldo waliyekuwa pamoja kwenye klabu ya Manchester Utd.
source:shafih dauda

0 comments:

OFFICIAL: TFF YAZUIA USAJILI WA EMMANUEL OKWI YANGA


USAJILI WA OKWI YANGA WAZUIWA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesimamisha usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi kutoka Uganda katika timu ya Yanga wakati likisubiri ufafanuzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana leo (Januari 22 mwaka huu) kupitia masuala mbalimbali, imesimamisha usajili huo baada ya kubaini kuwa Okwi aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu kutoka FIFA.
Okwi ambaye aliingia mgogoro na klabu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia aliruhusiwa na FIFA kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu (provisional permit) cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi ya Etoile du Sahel likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.
Katika FIFA kuna kesi tatu kuhusiana na suala la mchezaji huyo. Wakati Okwi ameishitaki klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. Nayo Simba imeishitaki Etoile du Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola za Marekani 300,000.
Hivyo, TFF imeiandikia FIFA kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza Ligi nchini Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake.
MECHI ZA TANZANIA PRISONS YAZASOGEZWA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesogeza mbele mechi za raundi ya 14 na 15 zinazoihusu timu ya Tanzania Prisons zilizokuwa zichezwe Januari 25 na 29 mwaka huu.
Awali Tanzania Prisons ilitakiwa kutafuta uwanja mwingine wa kuchezea mechi hizo dhidi ya Ruvu Shooting na JKT Ruvu kutokana na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine kutokuwa tayari kwa Ligi Kuu ya Vodacom wikiendi hii.
Mechi hizo sasa zitachezwa kati ya Februari 6 na 8 mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya Sokoine.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

0 comments:

BREAKING NEWS! USAJILI WA OKWI YANGA WAADUNDA..

Taarifa ambazo mtandao huu umezipata hivi punde jina la Emmanuel Okwi halijaidhinishwa kwenye usajili wa klabu ya Yanga.
Kwa maana hiyo Okwi hataruhusiwa kucheza raundi ya pili ya Ligi Kuu ya Vodacom mpaka sakata lake la usajili kutoka klabu ya Etoile du Sahel litakapotafutiwa ufumbuzi. 
credit :shafih dauda

0 comments:

ALICHOKISEMA TUNDA MAN KUHUSU YEYE NA ROSE NDAUKA KATIKA MAHUSIANO

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tunda Man, amesema mpenzi wake wa kwanza katika maisha yake ni mwanadada muigizaji wa filamu nchini Rose Ndauka,ambaye waliachana tangu 
2006.Akizungumza na XXL ya Clouds Fm  Tunda amesema walikuwa wakikutana na mwanadada huyo katika studio moja huko kariakoo hali iliyowapelekea kuanza mahusiano yao yamapenzi.
“Kuna studio moja kariakoo,wanadada walikuwa wanakuja kuchana na yeye anakuja studio anaangalia situation zinavyoenda, kwahiyo kuanzia hapo ndiyo akaanza kunijua nini, nikaenda kwao kila kitu kikawa fresh kila kitu kikawa kinaenda poa ni 2006 kitu kama hicho, yani tumeachana kabla, hamna hata mmoja aliyekuwa star, sasa tumejikuta kila mmoja anafanya issue zake na mimi nafanya issue zangu, mpaka sasa hivi nikikutana nae, nasikia ameolewa peace tu ,kama na shida na yeye kwasababu na yeye sasa hivi anapiga mapigo ya movie na mimi na movie zangu kama vipi namdondosha halafu namlipa”, alisema Tunda
Credit:-Bongo5

0 comments:

PICHA ZA KICHUPA KIPYA CHA JOH MAKINI FT NIKI WA PILI "NJE YA BOX"





0 comments:

HII NDO KUFURU YA PESA YA MCHEZAJI..'SAMUEL ETO’O' HAYA NDIYO MAGARI YA KIFAHARI ANAYOMILIKI NA ANAYOPENDELEA

Huyu ni Mka Cameroon anayesakata Kabumbu la kulipwa huko barani Ulaya, kwa sasa anaichezea Timu ya Chelsea, Pia Samuel ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Cameroon. 
 
Eto'o hivi karibuni ameonekana kutisha sana katika kabumbu analocheza huko ulaya. Tarehe 19 mwezi huu aliweka historia kubwa katika maisha yake kwa kupiga Hat trick kwa kuifuna Manchester united bao 3-1 na kufanikiwa kunyakuwa mpira kama zawadi.Pia Kati ya Vitu samwel Eto'o anavyovipenda katika maisha yake ni kuwa na Magari ya Kifahari. Hayo hapochini ni baadhi ya Magari ya kifahari anayomiliki mchezaji huyu mkameruni. Nukuu Eto'o said: "I like to have a few cars because it gives me choice and it doesn't hurt anybody. To give happiness, the first thing is to be happy oneself, and I am."


Maybach Xenatec Coupe worth £750,000


Aston Martin V12 Zagato, worth at £450,000



Bugatti Veyron worth at £1.55m
Credit:charleslimelight.blog

0 comments:

KAMA ULIKUWA HUJUI HUYU NDIYE MMILIKI WA YANGA ALIYEAIBUKA, ATAKA KWENDA KWA KIKWETE



ALIYEJITANGAZA kuwa mmiliki wa klabu ya Yanga, Juma Mwambelo, amesema yu tayari kukabidhi nyaraka zinazotafutwa na uongozi wa klabu hiyo kwa Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, alitangaza kwenye mkutano wa Yanga kwamba Mwambelo anashikilia hati za umiliki wa klabu ya Yanga kimakosa na anatakiwa kuzikabidhisha haraka iwezekanavyo kabla ya kuchukuliwa hatua.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwombelo alisema yupo tayari kumpa Rais Kikwete naye aukabidhi uongozi wa Yanga chini ya Yusuf Manji.
“Kweli hati hizo ninazo kwa kuwa mimi ni mmiliki wa Klabu ya Yanga, ila Rais Kikwete pekee ndiye naweza kumkabidhi, hata mwanaye Ridhwani nimewahi kumueleza kuhusiana na hili,” alisema.
“Mimi ndiye mmiliki wa Klabu ya Yanga, nina hati miliki halali ya klabu, hii hapa (anaonyesha), nina hati miliki ya jengo la Jangwani, pia ninayo ya jengo la Mafia, lakini hiyo waliiba na tayari nilisharipoti polisi.
“Kuhusu hati ya jengo la Jangwani ipo benki na yenyewe sijailipia kwa kuwa kuna deni, deni hilo ni zile fedha ziliyotumika kujenga Uwanja wa Kaunda. Hivyo,
deni likilipwa benki itakubali kutoa hati kisha kuirudisha wizarani na kutolewa rasmi.

“Nashangaa Yanga wanapodai wanatumia katiba mpya, hii siyo halali, katiba halali ya Yanga ni ile ya mwaka 1967 ambayo nakala yake hii hapa (anaonyesha),” alisema.
Alipoulizwa juu ya uhalali wa wanachama wa sasa wa klabu hiyo, alisema: “Wanachama wengine wote ni feki, mpaka unatokea mgawanyiko mwaka 1975, wanachama halali wa Yanga walikuwa 400, kuanzia hapo hakuna wanachama halali tena, hata akaunti zinazotumika siyo za klabu.
“Hapa nilipo nimekuja polisi (Magomeni) ili kutoa taarifa ya kujihami, nahofia kupigwa kutokana na walichokisema kwenye mkutano,” alisema.
Katika mkutano mkuu wa Jumapili, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Karume, PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam, uongozi wa Yanga ulimtaja mzee Juma kuwa ndiye aliyeiiba hati ya jengo la klabu hiyo tangu Juni 24, 2009.
“Mimi nilipigwa na watu mwaka 1987 nikapoteza fahamu kwa siku tano, tangu pale sijawahi kwenda klabuni wala uwanjani kuitazama Yanga, hata huyo Mrisho Ngassa simjui, namuona tu kwenye magazeti, kikubwa ninachotaka ni utaratibu ufuatwe ndani ya Klabu ya Yanga,” alisisitiza huku akitabasamu.
source:gpl

0 comments:

Meli nyingine ya Titanic kutengenezwa nchini China kwa $164m - Bongo5

 
 
Kampuni ya Seven Star Energy Investment Group, yenye makazi yake jimboni Sichuan nchini
 China itatumia dola milioni 164 kutengeneza meli inayofanana kila kitu la meli kama ya 
Titanic (replica) iliyozama karne moja iliyopita.

Meli hiyo itajengwa na kampuni ya China Shipbuilding Industry Corporation na itatumika 
kupamba park ya kaunti ya Daying iliyopo Sichuan kwa kuegeshwa kwenye mto Qi nchini China. 

Meli hiyo haitatumika kusafirisha abiria na watalii kwenye kina kirefu cha bahari kwakuwa si 
watu wengi wanaweza kuingia tena kwenye safari ya kufanana na Titanic ambayo haikukamilika.
 Badala yake meli hiyo itakuwa alama ya mzuka wa Titanic.
Shirika la habari la Xinhua limesema meli hiyo itatengeneza hali ilivyokuwa pale meli hiyo 
ya kufahari ilipogongana na mwamba wa barafu.
Ujenzi wa meli hiyo yenye urefu wa meta 270 unatarajia kumalizika baada ya miaka miwili.
Hii si mara ya kwanza kwa watu kutaka kutengeneza meli nyingine ya Titanic. Bilionea wa 
Australia, Clive Palmer alitangaza kutengeneza 

0 comments:

PICHA : PETER OKOYE WA PSQURE AKIWA NA MWANAE WA KWANZA WA KIUME

 That little boy has got so much swag and style...and he's soooo cute! Another pic after the cut...



0 comments:

BARCELONA YATHIBITISHA KUTUMIA KIASI CHA PAUNDI MILIONI 495 KUUBORESHA UWANJA WA NOU CAMP.



Bodi ya wakurugenzi ya FC Barcelona imekataa wazo la kujenga kiwanja kipya na badala yake wamekubaliana kuongeza nguvu kuufanyia marekebisho uwanja wao wa Nou Camp.



Wanachama wa klabu ya FC Barcelona ambao kimsingi ndio wamiliki wa timu hiyo watapewa nafasi ya kupitisha wazo hilo la kuuboresha uwanja Wa Nou Camp kwa kupiga kura mnamo mwezi wanne mwaka huu kwenye mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo.



Kama wazo hilo litapitishwa na wanachama basi uwanja huo mkubwa kuliko viwanja vyote barani ulaya wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 98,000 kwasasa, utakuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 105,000 na kusaidia kuongeza kipato kutokana na vyanzo vya uwanja huo.  
Pia itakuwa fursa kwa mashabiki kuweza kuwaona wachezaji nyota ulimwenguni kama vile Lionel Messi na Neymar.



Mradi huo ambao pia unahusisha ujenzi wa kiwanja cha ndani cha mchezo wa kikapu pamoja na vitega ychumi vingine vingi unataraji kuighalimu kiasi cha paundi milioni 495 ambazo ni sawa na euro milioni 600.Kazi hiyo ya maboresho ya uwanja inataraji kuanza mwaka 2017 na inataria kumalizika mapema mwaka 2021.

Ili kufanikisha mradi huo Barcelona inategemea kuchukua mkopo benki wa kiasi cha paundi milioni 165,pia inategemea kupata kiasi cha paundi milioni 82 kutokana na haki za jina la uwanja huo na kiasi kingine kilichobaki cha pesa kitatokana na vyanzo vilivyopo hivi sasa.
Raisi wa klabu hiyo Sandro Rosell amesema wakati woote wa ujenzi michezo mbali mbali inayoihusu klabu hiyo itaendelea kuchezwa kwenye uwanja huo.

0 comments:

#Exclusive: Unataka kuona mshindi wa BSS 2013 amezitumiaje milioni 50 zake? picha za alivyovifanya ziko hapa

.
.
Jina lake ni Emmanuel Msuya ambae usiku wa November 30 2014 Escape One Mikocheni Dar es salaam alitangazwa mshindi wa BSS kwa mwaka 2013 na kuzichukua MILIONI 50 kutokana na matokeo kamili ya mizani hiyo ya vipaji vya muziki kwa wachanga.
Unaambiwa kabla ya hapo, Msuya hakuwahi kushika au kumiliki zaidi ya shilingi laki tano… yani aliwahi kupata shilingi laki tano mara moja tu siku alipolipwa pesa ya miezi mitatu iliyotokana na mkataba wa kuifundisha na kuisimamia Kwaya ya KKKT kucheza ili ikafanye video.
Mambo matatu makubwa aliyoyafanya kwa hizi milioni 50 za ushindi wa BSS…. >>> Msuya amenunua nyumba ya milioni 17 nyumbani kwao Musoma mjini kama unavyoiona hapa chini kwenye picha, amenunua hili gari lenye thamani ya milioni 9, amejenga studio hiyo hapo juu kwenye picha ambayo imegharimu milioni 12 na tayari ameshapata nyumba ya kufanyia biashara ya Stationary Musoma Mjini.
.
.
.
.
.
Msuya ndio huyo mwenye shati jekundu na hii ndio ile siku aliyotangazwa mshindi wa zile milioni 50, ilikua November 30 2013.
source:millard ayo

0 comments:

Jaguar Kioo (Official Video) Main Switch

0 comments:

PICHA:UZINDUZI WA MREMA CUP 2014 TIMU 14 KUUMANA
 Mbunge wa vunjo Dkt Austino Mrema alipokuwa akizindua mashindano ya Mrema cup ambayo anayadhamini yeye ambayo yanashirikisha timu 15 kutoka jimbo hilo.
 Mh Mrema akisalimiana na vijana na kukagua timu ya himo na njia panda katika mechi ya ufunguzi iliyofanyika katika viwanja vya Himo,wilaya ya moshi mkoani Kilimanjaro

0 comments: