AFRICAN PRINT DRESSES 2014 TREND


I love this lol

CLUTCHES 2014 FASHION TREND

AA

JIMMY CHOO SHOES FASHION TREND FOR MEN 2014

duu hii ikija bongo wangapi wataudhuria kanisani ukiingia 2 unapewa dola $100(Abuja based church gave $100 to its members for attending church?)

Did this really happen? Oh dear!

timu ya taifa ya Nigeria yazindua uzi wa kueleke Brazil 2014

The Nigerian Football Federation today February 27th unveiled a brand new jersey our national team would use during the 2014 FIFA World Cup in Brazil. The jersey, which is lemon green, will be officially launched on March 5th when the Super Eagles meet Mexico in a pre-world cup friendly which will take place in Atlanta, Georgia.

According to the Head Marketing of the NFF, Adama Idris, the jersey was designed to suit the weather condition in Brazil. See more photos after the cut...














Ex-girlfriend wa Samuel Eto’o ashtua watu kuhusu umri wa mchezaji huyo.


hu
“Tatizo la Chelsea ni kukosa wafungaji, nina Eto’o ambaye ana miaka 32 au labda 35 nani anayejua?”.
Hiyo ilikua ni kauli ya kocha Jose Mourinho akimzungumzia Samuel Etoo na baadae mpenzi wa zamani wa Eto’o aliongea kuhusu umri wa mchezaji huyo kitu ambacho kimewashangaza watu wengi.
Anna Barranca alikuwa mpenzi wa zamani wa Eto’o na kupata mtoto mmoja wa kike ambaye hivi sasa ana miaka 11 amesema Eto’o ana miaka 39 kuelekea 40 na sio 35.
Mwanamke huyo amesema kwamba alijua kuhusu umri wa Eto’o wakati wapo Cameroon kutoka kwa mtu ambaye alikua pamoja na Etoo tangu utotoni.

Taarifa kuhusu kocha wa Taifa Stars kuachishwa kazi

Kim-PoulsenShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen wamekubaliana kuvunja mkataba katika makubaliano ambayo ni siri kwa pande zote mbili.
Uamuzi huo umetangazwa leo (Februari 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Kocha Poulsen mbele ya waandishi wa habari.
Rais Malinzi kwa niaba ya TFF ametoa shukrani za dhati kwa Kocha Poulsen kwa ushirikiano na mchango ambao ameutoa kwa Tanzania kuanzia kwenye mpira wa miguu wa vijana.
Naye Kim amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi cha miaka mitatu alichokaa nchini kuanzia Mei 2011 alipoteuliwa kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana, na baadaye Taifa Stars.
Akizungumzia benchi jipya la ufundi la Taifa Stars, Rais Malinzi amesema linatarajiwa kutangazwa hivi karibuni likiongozwa na kocha kutoka nje ya Tanzania.
Amesema kwa upande wa mechi dhidi ya Namibia itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Stars itaongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi akisaidiwa na kocha Hafidh Badru kutoka Zanzibar.
Katika hatua nyingine, Kocha Madadi amewaondoa wachezaji watano wa Yanga katika kikosi kilichotajwa awali ili wapate fursa ya kuitumikia timu yao kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Ahly ya Misri.
Wachezaji hao ni Athuman Idd, David Luhende, Deogratius Munishi, Frank Domayo, Kelvin Yondani na Mrisho Ngasa. Pia kipa Ivo Mapunda ameondolewa katika kikosi hicho baada ya kupata msiba.
Nafasi zao zimezibwa na wachezaji Abdi Banda (Coastal Union), Himid Mao (Azam), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Said Moradi (Azam) na Shabani Kado (Coastal Union).
Taifa Stars itaingia kambini keshokutwa (Machi 1 mwaka huu) jioni kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam, na itaondoka Machi 3 mwaka huu alfajiri kwa ndege ya South African Airways na kurejea nchini Machi 7 mwaka huu saa 8.15 mchana.