MOISE KATUMBI: LENGO LETU MSIMU UJAO KUCHEZA KLABU YA BINGWA YA DUNIA NA KUSHINDA
Mmiliki
na mwenyekiti wa timu ya soka ya TP Mazembe kutoka Jamuhuri ya
Demokrasia ya Congo Moise Katumbi amesema ana mpango wa kuiimairisha
timu hiyo ili iwe na nguvu ya kushiriki katika mashindano ya kidunia,
Katumbi anaamini kuwa anaweza kuifikisha timu hiyo katika ngazi ya
fainali za kombe la dunia la FIFA kwa ngazi ya vilabu.
Pamoja
na TP Mazembe kushindwa katika michuano ya kombe la shirikisho la CAF
lakini bado Katumbi anasema anajiandaa vyema na msimu ujao na mashindano
mengine."Malengo yetu ni kuleta ushindani mkubwa na ninaamini tunaweza
kufikia mafanikio kwa kile tulichonacho sasa"alisema Katumbi.
Katumbi
pia ameiambia BBC kuwa iwapo wataimarisha zaidi timu yao na kwamba
haoni ni kwanini siku moja TP Mazembe siku moja wasishinde kombe la
dunia.
Mwaka
2010, timu hiyo ya soka ya Mazembe ndio iliyokuwa klabu ya kwanza toka
bara la Afrika kutinga fainali katika mashindano ya kombe la dunia la
FIFA kwa ngazi ya vilabu lakini wakaondolewa na klabu ya Inter Millan ya
Italia.
Baada
ya michuano hiyo ya michuano hiyo ya shirikisho timu hiyo toka mji wa
Lubumbashi nchini Demokrasia ya Congo wanatarajiwa kurejea tena katika
michuano ya ligi ya mabingwa mwaka ujao.
Tambo
hizi za Mazembe ni kutokana na vipaji vya kutosha kutoka katika shule
ya vipaji vya michezo ambapo wanatarajia baada ya miaka mitatu wantakuwa
na wachezaji wenye uwezo wa kuwafikisha na kushinda kombe la dunia.
Hata
hivyo Katumbi kiongozi wa miongoni mwa timu tajiri barani Afrika
amesema kuwa ameweza kuhakikisha fedha zinapatikana ili kuimarisha
kikosi chake,kutengezeza uwanja mpya na wa kisasa ikiwa ni pamoja na
ununuzi wa ndege ya timu.
Mipango
yake katika kupata wachezaji wa kimataifa inaendelea ambapo kwa sasa
anawachezaji nchi za nje ambapo kwa ana wachezaji kutoka nchi za
Tanzania, Ghana, Zambia, Cameroon, Botswana na hivi karibuni amesajili
kutoka Malawi.
Timu
hii ya TP Mazembe ni miongoni mwa timu ambazo wachezaji wake wanalipwa
vizuri kwa viwango vya Afrika ikiwa ni jitihada za Katumbi kupunguza
kaksi ya vipaji vya Afrika kupotelea ulaya.
"Wachezaji
wazuri wa Afrika wanakwenda ulaya kwa sababu ya malipo mazuri kutokana
na kutolipwa vizuri hapa Afrika" anasema Katumbi.
Katumbi
anasema kuwa sera yao ni kuwachukua wachezaji toka nchi za Afrika ili
kuonyesha umoja ndania ya bara hilo na kwamba Afrika ni nnzuri lakini
kinachotakiwa ni umoja hasa kutokana na mapigano ambayo yamekuwa
yakitokea kila siku katika bara la Afrika.
source:shafih dauda
0 comments: