story mbili mpya kuhusu Diamond Platinumz

dd
Story ya kwanza ni kuhusu ujumbe mrefu aliondika Diamond kupitia ukurasa wake wa
instagram
. Ujumbe huo unaonekana unaenda kwa msanii fulani japokuwa hakuweka wazi ni msanii gani. Diamond aliweka post hii na baada ya muda mfupi aliifuta lakini maneno yote yalikuwa yanasomeka hivi. “Nafkiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu… kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe…
Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi…. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng’ombe wake Kwenye Maji safi….ila yeye ng’ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!!
Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!… leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!….Mxieeeeeeeew!�� Kama nimekuchefua Lamba ndimu Usitapike”.
Story ya pili ni kuhusu Diamond kushinda award ya wimbo bora wa East Africa na wimbo wa Number One. Award hiyo imetolewa nchini Burundi kwenye TTTMAwards.
diamond2
diamond3
source/credit to:millard ayo.com

0 comments:

Taarifa za msiba kutoka kwa Afande Sele


Screen Shot 2014-08-14 at 11.10.46 AM
Msanii wa longtime kwenye bongofleva Afande Sele amewajulisha watu wake wa karibu na mashabiki kuhusu msiba uliomkuta kwa kufiwa na mama wa wanae.
Kupitia ukurasa wa
facebook
Afande Sele aliandika “Ndugu zangu!! Nimefiwa na mzazi mwenzangu (Asha) /mama wa wanangu (mama Tunda) ..ni pigo kubwa kwangu na wanangu. Sisi ni waja wa mwenyezi mungu na hakika kwake tutarejea; mungu ampumzishe pema.”
Screen Shot 2014-08-14 at 11.12.56 AM
Kutoka kulia ni Marehemu Asha, Afande na watoto wake Asante na wa mwisho kushoto ndio Tunda.
AFANDE

0 comments:

Picha 7 za Treni yenye abiria 200 ilivyopata ajali mlimani.


2
Treni iliyokuwa imebeba abiria zaidi ya 200 imepata ajali kwa kuteleza pembeni ya reli na kusababisha baadhi ya mabehewa kuwa nje ya reli ambapo abiria waliokuwemo ndani ya treni hiyo walilazimika kukimbilia upande wa pili wa treni ili kuepuka lisidondoke kwenye maporomoko.
Juhudi hizo zilisaidia na hakuna mtu aliyefariki kwenye hiyo ajali lakini watu 11 walipata majeraha na watano kati yao kupata majeraha makubwa kwenye hii ajali iliyotokea nchini Uswisi.
1
3
4
5
6
7
source:millard ayo

0 comments: