PICHA 5: ZA WAPENZI WALIOVUNJA REKODI YA KUWA NA TATOO NYINGI ZAIDI


 Gabriela, 42, and Victor, 43, from Buenos Aires, Argentina,hold the official Guinness World Record for the most modified married couple .
They have a total of 77 bodily alterations that also include four microdermals, 11 body implants, five dental implants, four ear expanders, two ear bolts and one forked tongue.And  have been together for 13 years and say they are 'perfect' for each other.
Victor said:
 'We spent Valentine's Day together, we prepared a meal together and I was able to share the day with my Queen, Gaby.We met 18 years ago, we are perfect for each other and we love each other very much.
'We both have lots of tattoos and modifications and we continue to get them - we don't really care what other people think.



0 comments:

Hili ni ombi la Mama Mangwea kwenda kwa Maproducer wote.

mama mangwea 
Albert Mangwea ni miongoni mwa wasanii wanaoaminika kuwa na nyimbo nyingi sana ambazo bado hazijatoka,wakati wa kumbukumbu ya kifo cha Mangwea Morogoro iliyofanyika November 2013 Millardayo.com iliongea na familia yake kuhusu mpango wa nyimbo ambazo bado hazijatoka za Mangwea.
Keneth Mangwea kaka wa Marehemu Mangwea alisema wanashirikiana na rafiki wa karibu wa Marehemu Mangwea M to The P kukusanya nyimbo kwenye studio tofauti tofauti ambazo aliwahi fanya marehemu Mangwea na nia ni kuziweka kwenye album moja.
ngwea 
Leo kupitia XXL ya Clouds Fm Mama mzazi wa Mangwea ameomba kwa watayarishaji wote[Producers]ambao Marehemu Mangwea amewahi kufanya nao kazi kumletea nyimbo hizo kwa ajili ya kupata haki miliki[Copyright]Mama mzazi katoa namba za simu ili ikitokea ukiamini unao hata wimbo mmoja wa Marehemu umpigie.
Namba hizo alizozitoa mama ni 0754 967738,0755 303552 na 0718 592620 hii ni kama una kazi za Marehemu Mangwea.

0 comments:

Hii ni mpya kuhusu sakata la usajili wa Neymar FC Barcelona

363687_heroaUchunguzi unaoendelea wa sakata la usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar kwenda Barcelona umesimamishwa baada ya FIFA kukataa kuwasilisha baadhi ya vielelezo kwa ajili ya kesi hiyo kuendelea.
Jaji a mahakama moja nchini Spain Pablo Ruz alitoa ombi la ushahidi wa vielelezo kadhaa vinavyohusisha uhamisho huo wa Neymar kutoka Santos kwenda Catalunya, vielelezo hivyo vilikuwa vinahusisha hati kadhaa kutoka FIFA pia mkataba wa Neymar na kampuni ya  N&N (kampuni inayomilikiwa na wazazi wa mchezaji), mkataba wake na pamoja na hati zingine za masuala ya kifedha kutoka kwenye kampuni ya Deloitte.
Hata hivyo uchunguzi huo ulishindikana kufuatia FIFA kukataa kutoa taarifa hizo zilizohitajika wakisema ni vitu vya siri na inabidi vikachukuliwe kwenye mamlaka za nchi ya Uswis yalipo makao makuu ya FIFA.
Jaji Ruz sasa atatuma barua kwenda kwenye mahakama nchini Uswis kuomba msaada wa kupatiwa vilelezo vya ushahidi vinavyohitajika, jambo linawekana kufanikiwa.
Sakata la usajili wa Neymar tayari limemuondoa Sandro Rossell katika urais wa klabu ya FC Barcelona, baada ya kufunguliwa kwa kesi ya matumizi mabaya fedha yaliyolizunguka suala la uhamisho wa mchezaji huyo.

0 comments:

hii ndiyo makala aliyoandika Nikki wa II kuhusu thamani ya sanaa bongo.


 
Screen Shot 2014-02-13 at 4.59.27 PM 
Hii makala imeandikwa na rapper Nikki wa II, ukishaisoma unaweza kusema chako chochote…
Anaanza kwa kuuliza >>>> thamani ya sanaa ni KIKIII? ? ?
Nakutana na wasaniii wachanga wengi, Kwenye show, mitandaoni, mtaani, studio na wengine wananipigia
Wengi huomba kolabo, ushauri, namba za simu za watu mbali mbali wa Kwenye industry hii
80% huomba ushauri wa kutoka, kolabo kwa dhana ya kuwasaidia kujulikana mapema, ama kusaidiwa kufikisha cd zao kwa watu Fulani Fulani.
Ni Ngumu sana kukutana na msanii mchanga akakuuliza namna ya kuboresha uwezo wake wa ku rap, kuimba ama kuwa mwandishi mzurii…kwa kifupi kuwa msanii bora
Msanii wa kwenda Kwenye concert anataka kwenda studio, msanii Ana nyimbo Moja na nusu Ana taka umtafutie Dili ya kurekodi….Mimi mpaka naenda studio nilikuwa nishaperfom matamasha mengi ya kushindanisha vipaji na nilikuwa na nyimbo mbili mpya kila wiki hazikuwa Kali ila ndio zilikuwa hatua za kujifunza ku rap na kuandika mashairi.
Wakati natafakari nini msingi wa Sanaa kuonekana rahisi namna hii na kua maarufu kuwa ndio inspiration kwa wasaniii wachanga na wala sio usaniii bora…nikawasha TV Mara nikaona nyimbo ya kiwango sawa kabisa na jamaa Mmoja ananiimbiaga nikienda saloon,
ikafuata nyingine na nyingine za aina hiyo
Theni ikaja interview mtangazaji anamuuliza msanii kwa nin mziki haulipi?? Nikacheka utalipaje wakati ni kitu rahisi sana nikitoka nje tu hapo nakipata, na hata mfanya kazi wako wa ndani anaimba sawa tu na unaye muona kwenye TV. hamna kitu kisicho na thamani kinacholipa….kitu ambacho sina uhakika ni Kama na yeye akiwa gheto kwake huwa Ana angalia play list anayoipangaga
Nibiashara Binafsi sio sahihi kumjaji MTu kwa anachofanya…lakini je haujiskii furaha kipindi ulikuta una fans 200 ukafanya wakawa 2000 loyal fans, hautajisikia furaha kizazi kinachofuata nao wakaja kalia kiti hicho. Biashara zetu ni binafsi lakini Jamii yetu sio na nijukumu letu la ujumla kuandaa mazingira bora kwa watoto na wadogo zetu.
Any way turudi Kwenye mada, natafakari watu Kama kendrik lamar, 50 cent, iliwachukuwa si chini ya miaka 10 kufika mainstream, kina keri hillson miaka 5 yakuwa backup singer, nikakumbuka mfuko wa joh makini uliokuwa umejaa mashaiiri tumeutundika pale sebleni kwetu.
Nikakumbuka kuwa gemü ya mziki wa kizazi kipya ina Kama miaka 15 ila ina zaidi ya wasanii 50 walio wika na kupotea wakati NAs, snoop, jay z wana karibia miaka 20 Kwenye gem on top. Radio Kama hot 97 na host Kama funk master flex toka miaka ya 90 mpaka Leo wanakimbiza New York, source magazine, alafu nawaza baadhi ya vipind vikubwa vilivyo poteza umaarufu hapa bongo, shows za TV ambazo nilikuwaga naziota kuwepo, sikumbuki Mara ya mwisho nimeaangalia lini
Shows za kujaza diamond jubilee, msanii mmoja ndio alikuwa na thamani ya show Moja ya club Leo ni wasanii 8.
Thamani…value…hujengwa na nini?………na hujengwa na nani?,…….na unawezaje kuilinda kulingana na mabadiliko ya muda na tamaduni za kinyakati?………..towa maoni yako uki ya elekeza kujibu maswali hayo…..
Unaweza niandika on my twitter account Nick mweusi @nikkwapili ama on Instagram @nikkwapili

0 comments:

PICHA MBALI MBALI ZA AZAM FC WAKIWA TAYARI NCHINI MSUMBIJI WAKIFANYA MAANDALIZI.



  Wachezaji wakiwa tayari mazoezini....
   Himid Mao,Aggrey Moris,Brian Umony,Jabir,Mcha na Bocco.



 Katibu mkuu Nassor Idrissa 'Father' na Meneja wa timu Jemedari Said


0 comments:

picha za night club mpya iringa ya le-parte .


3 
 Iringa imepata Club mpya na ya kisasa ambayo kwa taarifa za awali nimeambiwa February 14 siku ya Valentine ndiyo uzinduzi wake.
5 
Club hiyo ambayo ina vitu vingi vya burudani kwa wateja wake kukufanya usiwe bored ambapo kuna flat screen za kutosha na nimeambiwa hadi toilet pia kuna sehemu za kuvutia sigara, varanda ya juu, sehemu saba (4) za baa, jiko na TV zaidi ya 9 zote kubwa zilifungwa chanel mbalimbali kwa wateja wake.
7Club hii inaitwa La-parte na  iko chini ya Ebony Entartainment.
8
4
source:milard ayo

0 comments:

PICHA 5: ZA KUSTAAJABISHA KWELI DUNIA INA MAMBO:





0 comments:

photos:Wasafi ClothingLine sample




0 comments:

KALI YA LEO: KUTANA NA SHABIKI NAMBA 1 WA BOTAFOGO ALIYEJICHORA TATTOO 83 KUHUSIANA NA MAPENZI YAKE KWA KLABU HIYO


Bo-tattoo-go!
Kutana na mzee huyu ambaye anajiita "Shabiki namba moja wa Botafogo" - na amejichora tattoo 83 kuthibitisha hilo.

“Nilizaliwa mjini Botafoguense,” anaelezea Delneri Martins Viana, 69, mwanajeshi mstaafu. 
Alikuwa huku akiwaangalia wachezaji kama vile Manga, Nilton Santos, Didi, Zagallo, Quarentinha, Garrincha na Amarildo kundi la wachezaji wa kikosi kizuri kuliko vyote katika historia ya klabu hiyo, baada ya hapo akawashuhudia akina, Paulo Cesar Caju na Jairzinho, baadae akashuhudia kikosi cha Botafogo kilichokuwa kikiongozwa na Tulio Maravilha kikipata mafanikio makubwa mnamo mwaka  1995.

Delneri alijichora tattoo ya kwanza - ikiwa kama kumbukumbu ya  Garrincha – miaka 14 iliyopita. Baada ya hapo akaanza kunogewa na kuingiza wino mwilini mwake.  
Mwili wake sasa umezungukwa na tattoo za kauli mbiu za Batafogo, majina ya wachezaji wa zamani, beji na hata Biriba, mbwa ambaye Raisi wa zamani wa klabu hiyo Carlito Rocha alivunja sheria za klabu zilizokataza wanyama - yeye alikuwa akiingia nae uwanjani akiamini ataleta bahati kwa klabu. 
Alama iliyopo nje ya nyumba ya Delneri  anayoishi na mkewe Marina Gonalves, na mbwa aliowapa majina ya Garrincha na Loco Abreu, iliyopo eneo la Bangu, ndani ya jiji la  Rio de Janeiro, inasomeka: ‘Karibu……lakini tafadhali usiongee vibaya kuhusu Botafogo.’

Delneri anajaribu kwenda kwenye kila mchezo wa Botafogo - nyumabani na ugenini - mara nyingi akiwa anasindikizwa na watoto wake wa kike Glaucia and Marcela.

0 comments:

PICHA MZEE MWENYE WATOO 70 NA WAKE 15 KATIKA PICHA YA PAMOJA


aoa_1ffb1.jpg
Lukata Singu na baadhi ya wake, watoto na wajukuu zake katika picha ya pamoja. Picha Elias Msuya Mzee Lukata Singu (65) anayeishi katika Kijiji cha Nyamwage wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani, anajivunia kuwa na familia kubwa yenye wake wengi wanaofikia 15 na watoto zaidi ya 70.kijijini hapo ambapo amejenga boma analoishi na baadhi ya wake, watoto na wajukuu.

0 comments:

KISA CHA MSANII WA BONGO MOVIE WASTARA KUNYWA SUMU!


 
Stori: Gladness Mallya
IKIWA imetimia mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu kifo cha mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’, staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma, Jumamosi iliyopita amedaiwa kufanya jaribio la kutaka kujiua kwa kunywa sumu.

Wastara akiwa kitandani baada ya kunywa sumu.

KABLA YA YOTE

Awali, staa huyo ambaye amepitia mitihani mingi, alitundika picha katika Mtandao wa Kijamii wa Instagram na kulalamika kuumwa tumbo.
Katika maelezo aliyoyaandika sambamba na picha hiyo, Wastara alimshukuru msanii mwenzake, Tamrina Poshi ‘Amanda’ kwa msaada aliompatia kwa kuwa alikuwa katika hali mbaya.

SUMU YATAJWA
Siku chache baada ya kuweka picha hiyo, Risasi Mchanganyiko lilipata kisa kizima kupitia kwa chanzo chake makini kuwa staa huyo alisumbuliwa na maumivu ya tumbo baada ya kuokolewa katika jaribio lake la kutaka kukatisha uhai wake kwa kunywa sumu.

SUMU ILIYOTUMIKA
Inadawa kuwa Wastara aliamua kunywa vidonge aina ya fragile kwa kuchanganya na pombe kwa lengo la kukatisha uhai wake ili kuondokana na manyanyaso anayoyapa kutoka kwa baadhi ya watu.

HAUSIGELI AOKOA JAHAZI
Inadaiwa kuwa wakati staa huyo akiwa chumbani kwa lengo la kujiua, msaidizi wa kazi ‘hausigeli’ aliingia chumbani humo kwa nia ya kufanya usafi ndipo alipomkuta Wastara akiwa analia huku amejiinamia.

“Hausigeli alijaribu kumuuliza sababu ya kilio chake lakini Wastara hakumjibu kitu, aliendelea kulia bila kikomo,” kilisema chanzo hicho.
Inadaiwa kuwa baada ya kutojibiwa kitu, hausigeli huyo alitoka na kumfuata Amanda ambaye alikuwa katika chumba kingine na kumweleza hali aliyomkuta nayo Wastara chumbani humo.

AMANDA APATWA NA MSHTUKO
Baada ya kuingia chumbani kwa Wastara, Amanda alipatwa na mshtuko mkubwa alipomkuta shoga’ke akiwa na baadhi ya vidonge mkononi na kumuuliza kisa cha kutaka kumeza vidonge hivyo.
“Wastara alimwongopea Amanda kwamba vidonge hivyo ni kwa ajili ya kujitibia mguu wake lakini Amanda hakukubaliana na maelezo hayo baada ya kuiona chupa ya bia iliyokuwa pembeni, kwa kuwa anafahamu Wastara siyo mnywaji wa pombe, ndipo alipobaini lengo lake la kutaka kujiua,” chanzo kiliendelea kushusha data hizo.

Chanzo hicho kimesema kuwa Amanda alimpatia huduma ya kwanza shoga’ake huyo kwa kumnunulia maziwa na kumpeleka katika dispensari ya karibu ili kupata matibabu zaidi ya kuondoa sumu ya vidonge alivyovimeza.

SABABU ZA KUTAKA KUJIUA
Kwa mujibu wa chanzo kingine cha habari, Wastara alitaka kukatisha uhai wake kutokana na kuchoka kunyanyapaliwa, kudhalilishwa na kutongozwa mara kwa mara na wanaume, hali ambayo imekuwa ikimfedhehesha mbele ya jamii.

Chanzo hicho kimesema kwamba kabla ya tukio hilo, Wastara alikuwa akilalamika kudhalilishwa na watu anaowadai fedha zake ambao hawataki kumlipa haki yake.
“Kuna watu wengi ambao Wastara anawadai lakini wanamsumbua kwa kumuona ni mwanamke asiye na nguvu na wengine wanatumia mwanya huo kumtongoza, mwenyewe anaamini haya yote yanatokea kwa kuwa Sajuki hayupo,” kimetoboa chanzo hicho.

Habari zaidi zinadai kwamba hivi sasa Amanda anaendelea kumwekea ulinzi wa karibu Wastara ili asiweze kuchukua uamuzi mbaya wa kukatisha maisha yake.
Baada ya kuyapata madai hayo, mwandishi wetu alimpigia simu Wastara ili kupata undani wa tukio hilo lakini kwa muda mrefu simu yake ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa.
Jumapili iliyopita Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Amanda ili kuweza kupata ukweli wa madai hayo na kumuuliza kama bado yupo kwa Wastara.

HUYU HAPA AMANDA
“Wastara amepatwa na matatizo, kwa kuwa ni rafiki yangu ambaye aliwahi kunisaidia siku za nyuma niko naye kumfariji…” alisema Amanda.
Risasi Mchanganyiko: Hivi amepatwa na matatizo gani?’
Amanda: Ya kawaida tu.
Risasi: Inadaiwa kuwa amekunywa sumu?
Amanda: Miye siyo msemaji wake, ila elewa kuwa amepatwa na matatizo, si umpigie kwenye simu yake uzungumze naye?
Risasi: Simu yake haipokelewi ! Kama uko naye karibu nipe basi nizungumze naye?
Amanda: (kimya kidogo halafu)… Siko naye hapa.
Risasi Mchanganyiko: Wewe uko kwa Wastara tangu lini?
Amanda: Nina muda kiasi kwa kuwa kuna kazi tulikuwa tunataka kufanya.
Baada ya kuachana na Amanda, jioni ya Jumapili iliyopita Risasi Mchanganyiko lilimtafuta tena kupitia simu yake ya kiganjani Wastara na kumpata.
Wastara: Haloo
Risasi Mchanganyiko: Naongea na Wastara…?
Wastara: Eeeh ndiyo miye.
Risasi Mchanganyiko: Pole na matatizo.
Wastara: Asante, lakini nazungumza na nani?”
Risasi Mchanganyiko: Mwandishi wa habari wa Global Publishers, nasikia umekunywa sumu kwa lengo la kutaka kujiua….
Hata hivyo, upande wa pili wa simu haukuwa tena hewani, mlio wa kukatika kwa simu hiyo ulisikika.
Jitihada za kumpigia simu Wastara ziliendelea lakini hazikuweza kuzaa matunda kwani iliita bila ya kupokelewa na baada ya muda simu yake haikuwa ikipatikana tena.

TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2008, Wastara kabla ya kufunga ndoa na Sajuki alipata ajali ya pikipiki iliyosababisha kukatwa mguu na kuwekwa mguu wa bandia.
Mwaka 2009, Wastara na Sajuki walifunga ndoa ya kihistoria na kuwavutia watu wengi.
Lakini Januari 2, 2013, staa huyo alipata pigo la kufiwa na mumewe huyo baada ya kumuuguza kwa muda mrefu na kuzua simanzi kwa watu wengi.

CREDITS: GPL

0 comments:

PICHA 13 ZIPO HAPA: ZA MAGARI YA GOOGLE YASIYOTUMIA DEREVA HUJIENDESHA YENYEWE














0 comments: