HII TAARIFA NYINGINE YA YULE MTOTO WA MIAKA 4 AMBAYE AMEISHI KATIKA BOKSI KWA MIAKA 4 MANISPAA YA MOROGORO, BASI MIFUPA YAKE VIMEVUNJIKA.

 

POLISI mkoani Morogoro, inaendelea kuchungua kilichotokea mpaka mtoto mkoani hapa (jina limehifadhiwa), akateswa na mzazi mlezi kwa kuwekwa katika boksi tangu akiwa na miezi tisa, mpaka alipotimiza miaka minne. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul, amesema, baba mzazi wa mtoto huyo, Rashid Mvungi ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro alitakiwa kwenda kutoa maelezo kituoni leolakini hakutokea.

Kamanda Paul alisema jana kuwa, walimtafuta mzazi huyo kwa simu ili kumkumbusha umuhimu wa kufika Polisi kutoa maelezo, lakini simu zake zilikuwa zimezimwa.

Gazeti hili lilifika kwa mwajiri wake katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, ambako hakuwepo kwa kuwa aliaga kwamba amekwenda katika Kituo cha Ustawi wa Jamii, alikodai kuwa aliitwa.

Hata hivyo, gazeti hili lilipofika katika ofisi hiyo, lilihakikishiwa Ofisa Ustawi wa Jamii, Oswin Ngungamtitu, kuwa Mvungi hakuwa amefika katika eneo hilo, wala hakukuwa na mwito wa yeye kufika katika ofisi hiyo.

Katika tukio lingine la kutia shaka, gazeti hili lilipohojiana na Mvungi katika nyakati tofauti juzi, alitoa taarifa mbili tofauti, kuhusu sababu za kumuacha mwanaye kwa mama mkubwa wake, Mariam Said, aliyemuweka katika boksi kwa zaidi ya miaka mitatu.

Katika mahojiano ya awali, Mvungi alidai baada ya mzazi mwenzake, Mwasiti Ramadhan kufariki dunia, alishindwa kumchukua mtoto wake kwa sababu tayari alishakuwa na mke.

Alidai kwa kuwa alikuwa ameoa, alikubaliana na upande wa pili wa familia ya marehemu, kuwa mwanaye huyo alelewe na mama yake mkubwa, Mariamu.

Katika mahijiano na mwandishi mwingine wa gazeti hili juzi hiyo hiyo, Rashid alidai mwanae huyo alichukuliwa na Mama yake mkubwa ili kumlea akiwa na umri ndogo na mara zote alikuwa akipeleka fedha za matumizi.

Alidai kwa mara ya mwisho alimwona mwanae huyo miezi miwili iliyopita akiwa na afya ya kuridhisha, wakati taarifa zilizotolewa na Mariam, zilidai kuwa mtoto huyo hajaogeshwa tangu Julai mwaka jana.

“ Kila nikienda kumwona nyumbani kwao sikubahatika kumwona , nilikuwa nikiambiwa amelala ama ametoka na watoto wezake...isipo kuwa miezi miwili iliyopita,” alidai Rashid kauli inayoonesha kuwa mtoto huyo alikuwa akitoka na wenzake wakati majirani walitoa ushahidi kuwa hawakuwahi kufahamu uwepo wa mtoto katika nyumba hiyo.

Taarifa kutoka katika Hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro, zimeeleza kuwa baada ya uchunguzi wa awali wa afya ya mtoto huyo, alibainika kuwa na niumonia, ulegevu wa viungo ikiwa ni pamoja na baadhi ya mifupa katika mwili wake kuvunjika.

Daktari Mshauri wa watoto, Hores Msaky alipozungumza na gazeti hili jana, alisema walimpokea mtoto huyo juzi alikuwa katika hali ya uchafu usio wa kawaida.

Msaky alisema waliamua kumfanyia vipimo vya awali pamoja na picha za X ray, wakagundua kuwa mifupa yake si ya kawaida, inaonekana imevunjika ingawa hawajajua nini kimemvunja.

“Tunachokifanya hivi sasa ni kujaribu kujua tatizo hilo limetokana na nini,” alisema daktari huyo Hata hivyo Msaky alisema kuwa hospitali hiyo haina vifaa vingi vya kupimia mifupa, hivyo imeshauriwa apelekwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi zaidi .

Muandishi wa habari hizi alifanikiwa kuingia wodi aliyolazwa mtoto huyo na kumkuta akiwa amechangamka, na alipoulizwa anaendeleaje alisema anasikia maumivu katika sehemu ya kifua .

Mtoto huyo alikuwa akidhulumiwa haki yake ya utu na kuteswa kwa zaidi ya miaka mitatu, kwa kufungiwa ndani ya boksi kama mnyama, ili asiamumbukize mama mlezi virusi vinavyosababisha Ukimwi.

Unyama huo wa kusikitisha, ulikuwa ukifanyika muda wote huo kwa mtoto huyo Morogoro mjini katika mtaa wa Azimio bila kuripotiwa popote, huku wakazi na majirani wa nyumba hiyo wakisikia akikohoa na kulia usiku, na baba yake mzazi akiendelea na maisha kwa kumuogopa mkewe. Wakizungumza na gazeti hili juzi majirani hao walidai Mariam alihamia katika nyumba hiyo mwaka 2010, lakini hawakuwahi kumuona akiwa na mtoto.

Hata hivyo majirani hao walikiri kwamba walikuwa wakisikia mtoto akikohoa na kulia hasa nyakati za usiku, lakini walikuwa na wasiwasi kuwa huenda mtuhumiwa alikuwa mshirikina anayefuga watu waliouawa kishirikina au kwa jina linguine misukule.

Hatimaye juzi mateso ya mtoto huyo yalipungua, baada ya msamaria mmoja kupata taarifa sahihi, kwamba ndani ya nyumba hiyo kuna kiumbe asiye na hatia aliye katika mateso na kutoa taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Dia Zongo.

Zongo akiwa katika kazi za kawaida katika mtaa huo, alipata taarifa kutoka kwa majirani kuwa kuna mwanamke, Mariamu Said, amemficha mtoto ndani ya boksi na hamfanyii usafi wala kumtoa nje.

Baada ya kupata taarifa hizo, Zongo alimtafuta mwenyeji wake, Mwenyekiti wa mtaa huo, Tatu Mgagalana na kuongozana naye hadi kwenye nyumba hiyo ambapo walimkuta mtuhumiwa, Mariamu na kuanza kumuhoji kuhusu tuhuma hizo.

Kwa mujibu wa Zongo, wakati mtuhumiwa akijibu maswali aliyoulizwa huku akibabaika, ghafla mtoto huyo alipiga chafya na kuanza kukohoa hali iliyowapa wasiwasi na kuamua kuingia chumbani kwa Mariamu kwa nguvu, hatua iliyomuokoa mtoto huyo kutoka katika mateso ya zaidi ya miaka mitatu.

Ofisa huyo na mwenyeji wake walimkuta mtoto huyo ametapakaa uchafu uliotokana na kinyesi na mkojo, kwa kuwa boksi hilo lilikuwa chumba chake cha kulala, meza yake ya chakula na maji na choo kwa ajili ya haja ndogo na kubwa.

source:HABARI LEO

0 comments:

hii ndo List ya waigizaji matajiri duniani,



Wapenzi wengi wa filamu duniani watakuwa wanalitambua jina lake ambapo kwa Tanzania ni maarufu zaidi uswahilini lakini duniani ndio anatajwa kuwa muigizaji anayejulikana zaidi.
Jina lake ni Shahrukh Khan ambae ni mwigizaji wa filamu kutoka India ambapo jana ametengeneza headlines baada ya kutajwa na jarida la maswala ya fedha la Wealth-X la Singapore ndio mwigizaji tajiri zaidi Asia pia anashika nafasi ya pili duniani nyuma ya comedian Jerry Seinfeld ambaye ana utajiri wa dola za kimarekani milioni 820.
Jerry Seinfeld
Jerry Seinfeld
Khan ambaye ni maarufu kwa jina la Kingh Khan ana utajiri wa $600m akiwa kawazidi waigizaji wakubwa Hollywood kama Tom Cruise mwenye $480 million, akiwafuatia na Johny Depp na Tyler Perry ambao wote wana $450 million.
srk-tom-johnny 
Listi hiyo imechanganya waigizaji washindi wa tuzo za Academy kama Jack Nicholson ($400 million), Tom Hanks ($390 million) na Clint Eastwood ($370 million) Nicholson ni namba 6 akifuatiwa na Hanks, Bill Cosby, Eastwood na Adam Sandler.
credit to:milard ayo

0 comments:

matukio mbali mbali kwenye uzinduzi wa Airtel huduma ya SWITCH ON,Wakiwemo Dimpoz,vannessa,barnaba na wengine kibao

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel jana ilizindua huduma kabambe ya Intaneti itakayojulikana kama SWITCH ON. Huduma hiyo ni maalum kwa watumiaji wa huduma za Interneti Tanzania ambapo sasa wateja wa Airtel wataweza kufuruhai huduma ya kipekee ya vifurushi vya data/intaneti maalum kwa simu na mahitaji ya kila mteja.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel  Tanzania Bw, Levi Nyakundi alisema “ ulimwengu wa leo matumizi ya huduma za intaneti/data au mtandao hayaepukiki, ukitaka kujua kinachoendelea duniani kwa haraka basi intaneti ndio suluhisho au jawabu linapopatikana, lakini kumekua na changamoto nyingi sana hasa pale tunapohitaji intaneti bora ya kutuwezesha kufanya fasta mawasiliano na tuwapendao au tunapotaka kuunganishwa na taarifa za mambo muhimu yanayoendelea dunia kote, inawezekana kila wakati umekua ukijiuliza ni MB au GB au kifurushi gani kitakuwezesha kufanya mambo yako kuwa poa zaidi, hili ndilo lililotusukuma Airtel kukuletea wewe mteja wetu huduma hii ya kisasa na ndio maana tunakuambia SWITCH ON”

“Ukiwa na Airtel ‘SWITCH ON’ watumiaji wa huduma za Intaneti Tanzania sasa wanakila sababu yakufurahia kujipatia huduma bora zaidi kwa gharama nafuu na kufanya chaguo la kufurushi utakacho MAALUM kwa simu yako. Hii ni huduma inayoenda na wakati, inazingatia utamaduni wetu kwa kuwa ni ya kukutoshelezea hitaji lako, na gharama ni nafuu kuliko zote huku ikikuhakikishia mteja Non-stop intaneti - yaani fulu makamuzi kwa wewe mtumiaji kutokupimiwa. Huduma hii ya pia inamuwezesha mteja kuwa na chaguo la kifurushi iwe kwa SIKU, WIKI au MWEZI”

“Airtel Tanzania tumejipanga zaidi kuhakikisha tunaendelea kuwa wabunifu na kuwapatia huduma bora ya mawasiliano ya internet. Tutaendelea kufanikisha  hili kwakuwa Airtel Yatosha, Airtel Money nusu gharama, au Bure Pack ni vielelezo vya huduma bora na nafuu tunazowapatia wateja wetu kwa sasa na kuwafaidisha wateja kila siku. Hivyo leo hii SWITCH ON nimuendelezo wa kuwahudumia watumiaji wa Internet nchini Tanzania kwa kuwapa wanachokitaka bila kikwazo yaani Fulu makamuzi” aliongeza Nyakundi 

 Kwa upande wake Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo akielezea jinsi ya kutumia huduma hiyo alisema “Ni rahisi sana mteja wetu kujiunga, unatakiwa tu kupiga *148*22# ikiwa tu una simu yako yenye uwezo wa kutumia intaneti /Data kisha utaweza kujichagulia aina ya kifurushi kinachokufaa kutokana na mahitaji yako kwa kuwa vifurushi ni maalum kwa simu au kifaa utakachotumia yaani iwe unasimu ya Feature phone, au Simu mpapaso (Smart phone au Tablet sisi Airtel tumekuwekea kifurishi cha intaneti maalum kwa kila simu”

‘Vilevile kwa wale wateja wote wa Airtel wanaotumia huduma ya Airtel Yatosha pia bado wananafasi ya kujiunga na vifurushi vya intaneti vya Yatosha na ikiwa wamemaliza Data /intaneti na wanapenda kujiunga na Data pekee basi wanaweza pia KU-SWITCH ON na kuendela na makamuzi” alimalizia kusema Prisca. 
Mabalozi wa Huduma mpya ya Airtel,Ney wa Mitego,Vannessa Mdee na Barnabas wakiwa wameshikilia mabango yenye kuonyesha namba ya kujiunga na huduma hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wake uliofanyika jana usiku kwenye kiota cha Maraha cha Club Rouge ndani ya Hoteli ya Hyatt Agengy The Kilimanjaro,Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel  Tanzania, Levi Nyakundi akizungumza na wadau mbali mbali (hawapo pichani) waliohudhulia hafla hiyo ya uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel kwa watumiaji wa Internet hapa nchini ijulikanayo kama SWITCH ON.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni Balozi wa huduma hiyo mpya ya Airtel,Barnabas akitoa burudani kwa wadau waliofika ukumbini hapo.
Ney wa Mitego 
Vannessa Mdee na madansa wake ndani ya nyumba.
DJ Choka alipewa wasaa wa kuielezea simu mpya aina ya Samsung s5 ambayo ilishindaniwa na wadau mbali mbali waliokuwepo ukumbini hapo.
DJ Zerro akifanya vitu vyake.
Wadau mbali mbali wakifatilia uzinduzi huo kwa umakini mkubwa.

0 comments:

+++++BREAKING NEWZ****Wakati matokeo rasmi yakisubiriwa kutangazwa,huyu ndiye Waziri aliyejiua Malawi.


http://mwnation.com/wp-content/uploads/2013/09/kanyama.jpg

Ingawa matokeo rasmi bado hayajatangazwa nimepata taarifa kuwa Waziri wa serikali za mitaa nchini Malawi Godfrey Kamanya,amejiua baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu siku ya Jumanne.
Waziri huyo alijipiga risasi nyumbani kwake baada ya kupata taarifa za kushindwa,Matokeo ya kura bado hayajatangazwa rasmi katika kile kinachosemekana kuwa uchaguzi wenye ushindani mkali sana.
Afisa mkuu wa uchaguzi amesema kuwa mfumo wa elektroniki umeharibika na maafisa wanatumia matokeo kwa njia ya barua pepe(email).

1 comments:

haya ndiyo yaliyomkuta rapper Fabolous? amepata ajali saa kadhaa zilizopita.

Screen Shot 2014-05-22 at 12.33.35 PM
Fabolous ambae ni Rapper wa longtime kwenye chati za muziki duniani ambae amewahi kuja kufanya show Tanzania, amepata ajali huko Queens New York Marekani.
Baada ya ajali hiyo Fab amemshukuru Mungu kwa kumuepusha yeye dereva wake na madereva wawili wa lori kutoka salama na kusema hii ndio mara yake ya kwanza kupata ajali ya gari, imemshtua na imemuonyesha jinsi mambo yanavyoweza kubadilika haraka so ‘Live, Love, & Celebrate Life. #Blessed’ alimalizia kwa kuandika hivyo.

1 comments:

HII NDIO SEHEMU AMBAYO TIMU YA ARGETINA YA MESSI ITAKAPOWEKA KAMBI KIPINDI CHA KOMBE LA DUNIA BRAZIL


sehemu ya uwanja wa kufanyia mazoezi wa Argentina (Vespasiano) nchini brazil
Foto: Paulino Menezes/Portal da Copa/ME
uwanja wakufanyia mazoezi

sehemu yakufanyia mazoezi




 
sehemu yakufanyia mazoezi

sehemu yakupumzika


sehemu yakulia chakula



prepared by mekuinnocent.blogspot.com

0 comments:

MB DOG -- MBONA UMENUNA (OFFICAL VIDEO)

0 comments:

MB DOG -- MBONA UMENUNA (OFFICAL VIDEO)

0 comments:

hivi ndivyo walemavu walivyofunga barabara dar jana

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEirYG9Pl01JA-vPCHJjyDtNesWG2t8Qh5xGRy3P1ewbw4fGAehD5dwdGBFjaMr31rawBu1MRo8_2Wxape1G7SedkpeUJEk3aWPv3DPadRK_xbtjrZe9ZdR_6MkjkrC2zq_j7yy2LvXCiKE/s1600/1.JPG



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh8hkADrPVdl99p26rp6x_4uTwuPFbbzaeIeKf5hBOXrpl0y1kA_zsdRnmQDC88-niEDwcQ0h46vQOffOb6Lx3nvxUHxP3MNq5ZcOWuRMknHlPddcqghcJ-Eu5uv4Ec4OMUCA3RlEVz6jM/s1600/3.JPGhttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhVBr4YQq01qse9krJmyiDKsrgKam1UQpLTNUYb2cNDkg6LS16AD7gKt8nlnJ36TRIC4_fupK4lMBsYRVIXlAX1cj9OYXAnNZjFhHN4fB5iW56kB-fL5wrRc8zWpca0fBBc6gBWEf0JbTs/s1600/dc8b9aba72c6e10174ec52ed4366bc01+(1).jpghttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjqbKoDtual9tOL24Q4t53IMbknw2cxcJ9h8tnU5sXrRipSSvve3DJPlxLfMp2rFQiirjIgjUgNC31HRPP9kIVMORJo_OpmvL6bl75pK3561VgZc6OIbC4N0gEXJurW33V-phhp56prkjs/s1600/2.JPGhttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg7DJK8YME5VY4jrw7UiJ8Da9sdIK_d1xuotaJdZsEDRnHSdJVpMGAAbd58puN1lGH6WOde9tRCUVY3YLrZ9klunmGlR0CzxFixKuFLQjzi5H7WbHjoDPwhEvf_U6ihw428AfrgJ21IM_Y/s1600/4.JPGhttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj__LQYM-AdZrX-w-L01_i5ibu7qLu1_MPCR21BZ-idQ8u5XOh7LCxUDoU4qmcQlaYnrA7_dNk__PKYzhR-iYuCIxaR-lmUNAQ5CX3wrukOBlC9QpBMLUrzbuoVqtIrNOd0-VTEmExGiK0/s1600/378a0fd39aa76ece2d2fc591c5ea3a74.jpg

0 comments:

Hii ndiyo safari ya mwisho ya Muongozaji na Muigizaji Adam Kuambiana.


Home » Ent. » Hii ndiyo safari ya mwisho ya Muongozaji na Muigizaji Adam Kuambiana.


29msiban 
Mei 20 saa 9 alasiri ndiyo safari ya mwisho ya Muongozaji na Muigizaji kutoka kiwanda cha filamu Tanzania Adam Philip Kuambiana ambaye amepumzishwa kwenye makaburi ya Kinondoni,mahali ambapo pia amezikwa Muongozaji mwingine na Muigizaji Steven Kanumba.
26msibanUjumla wa watu waliojitokeza ni wengi sana hasa wasanii wa filamu ambao asilimia kubwa wamejitokeza kumzika Adam Kuambiana,hizi ni baadhi ya picha za kuanzia Leaders wakati wa kutoa heshima heshima za mwisho mpaka anazikwa kwenye makaburi ya Kinondoni.
1msiban
2msiban
7msiban
9msiban
11msiban
12msiban
18msiban
17msiban
20msiban
21msiban
22msiban
23msiban
24msiban
25msiban
26msiban
42msiban
38msiban
37msiban
34msiban
27msiban
43msiban
78msiban
79msiban
83msiban
84msiban
90msiban
89msiban
88msiban
87msiban
85msiban
91msiban
93msiban
95msiban
98msiban
101msiban
107msiban
1msiban
4msiban
5msiban
7msiban
13msiban
12msiban
11msiban
10msiban
16msiban
17msiban
18msiban
19msiban
20msiban
26msiban
25msiban
24msiban
22msiban
21msiban
27msiban
30msiban
31msiban
32msiban
41msiban
40msiban
37msiban
36msiban
34msiban
42msiban
44msiban
46msiban
48msiban
50msiban
57msiban
56msiban
55msiban
54msiban
51msiban
58msiban
61msiban
62msiban

63msiban
65msiban
66msiban
67msiban
70msiban
72msiban
76msiban
107msiban
91msiban
90msiban
101msiban
85msiban
84msiban
83msiban
79msiban
78msiban
93msiban
95msiban




 98msiban
source:milard ayo

0 comments: