hili ndilo Tamko la TFF kuhusu tiketi za Ki-elektoniki.
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) leo limetangaza kusitisha matumizi ya tiketi za
elektroniki kwenye viwanja vyote vyenye huduma hiyo ili kutoa fursa ya
kufanyika tathmini ya kina kabla ya kuendelea tena.
Akitangaza uamuzi huo Afisa Habari wa TFF Boniface Wambura
amesemaUamuzi huo umefikiwa kwa kuzingatia sababu mbalimbali baada ya
kikao kati ya Sekretarieti ya TFF na maofisa wa benki ya CRDB
kilichofanyika jana (Februari 3 mwaka huu) katika ofisi hizo za
Shirikisho la soka.
Tathmini hiyo inafanyika ili kubaini changamoto zilizojitokeza na
kuzitafutia ufumbuzi kabla ya kuendelea tena na matumizi hayo, kubwa
ikiwa ni hadhari iliyotolewa na vyombo vya Usalama juu ya misongamano
inayotokea uwanjani kutokana na kutokuwepo mtiririko mzuri wa uingiaji.
Tayari zipo changamoto za wazi ikiwemo uelewa wa washabiki wa jinsi
ya kununua na kutumia tiketi hizo, milango michache ya kuingilia
uwanjani na washabiki wengi kununua tiketi dakika za mwisho hivyo
kuchangia misongamano.
Source:milard ayo
0 comments: