Amboni Tanga: Askari Polisi wapambana na majambazi wenye silaha za moto




Tanga kumenuka, magaidi wenye silaha nzito wanapambana na askari polisi muda huu. Askali wa jeshi la wananchi wameingilia kati na silaha za kisasa. Sasa hivi wanaelekea kwenye mapango ya Amboni.


Kuna taarifa nimezipata muda sio mrefu zinasema polisi wanarushiana risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni magaidi.

Inasemekana walienda kumkomboa mwenzao aliyekamatwa na polisi. Polisi watatu wamejeruhiwa na wameomba msaada toka JWTZ.
Hadi sasa taarifa kutoka mkoani Tanga zinaeleza kuwa askari wanne wa Jeshi la Polisi Tanzania wamejeruhiwa katika mapambano dhidi ya vikundi vya kihalifu (kigaidi) katika eneo machimbo ya Amboni mkoani humo.

Taarifa zaidi zinasema askari hao wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga kwa matibabu zaidi na kuna watu wawili ambao wamekamatwa kuanzia jana hadi sasa wakihusishwa na tukio hilo.

Aidha, mmoja wa Askari waliopo katika eneo la tukio amesema mapema leo asubuhi Helkopta ya Polisi ilinusurika kudunguliwa na vikundi hivyo vinavyosadikiwa kuwa viko zaidi ya vinne.

Pamoja na ulinzi kuimarishwa kila kona ya eneo hilo imeelezwa kuwa Kamanda wa Polisi mkoani Tanga atatoa taarifa ya tukio hilo saa 15:00pm
.
UPDATES II:
Pango limevunjwa kwa kutumia mizinga, na hatimae jamaa wametoroka hakuna aliekamatwa, Sergeant Kajembe wa JWTZ aliepigwa risasi ya Tumbo ameshafariki Dunia, majeruhi waliopo hospital ni PC mmoja wa FFU, Sergeant wa JWTZ aliejeruhiwa sikio, Corporal alijeruhiwa mguu.

Askari wote wameshatawanyika eneo la Tukio na walichokuta ni Pikipiki, baiskeli, vyakula na nguo.









UPDATES:

Yapata wiki moja Polisi walimkamata mtuhumiwa mmoja anajulikana kwa jina la Master ambae inasemekana ndiye aliyekuwa akiratibu uporaji wa silaha vituo vya polisi na polisi wenyewe. Matukio haya yametokea kule Ikwiriri Rufiji Pwani baada ya kituo kuvamiwa na Tanga Chumbageni kwa askari kuporwa silaha wakiwa katika doria.

Katika kutumia weledi wao wa kupata habari, ililazimika sasa polisi waende eneo ambalo mtuhumiwa anasema ndiko silaha wanazopora zilipofichwa. Alieleza silaha wanaficha maeneo ya Amboni ambako Wachina waliojenga barabara ya Horohoro waliweka kambi. Kwa hiyo magaidi hayo hayapo mapango ya Amboni tunayoyafahamu.

Baada ya kufika eneo la tukio mtuhumiwa akiwa na pingu alijirusha kwenye pango hilo huku polisi wakiwa wanashangaa nini kimetokea. Ikumbukwe mtuhumiwa huyo alikuwa na pingu. Baada ya mtuhumiwa tu kutua chini au kiliposikika kishindo basi haikupita muda mvua ya risasi ilianza kunyesha kuelekea polisi walipo pamoja na mabomu ya kurusha kwa mikono. Bomu mojawapo lilifanikiwa kumjeruhi askari polisi mmoja ambaye ameshonwa nyuzi kama kumi na moja hivi. Kwa hiyo hakuna polisi aliyekufa kwenye tukio hilo.

Baada ya kuona hali imekuwa ngumu ilibidi OCD aliyekwenda kwenye tukio kuomba msaada zaidi kwa FFU Tanga. Napo hali ikawa tete, ndipo ilipolazimu kuomba msaada kutoja Jeshi la Wananchi Tanzania.

Kama uelewevyo kuomba Jeshi la Wananchi kuingilia kati na lazima CDF atoe kibali na ithibitike kuna ulazima.

Hatimaye saa tisa za mchana kibali kilipataka na Jeshi la Wananchi kwenda eneo la tukio. Walipofika waliona kuna ulazima wa kutumia silaha nzito ili kulifumua pango hilo ambalo ili kujua kilichopo. Kuanzia hapo mizinga imekuwa ikisikika maeneo hayo ishara ya kwamba wanaume wapo kazini.

Katika kuongeza nguvu kikosi maalumu kimeongezwa kutoka Dar ili kuhakikisha hali inakuwa salama.

Hadi leo asubuhi bado mizinga ilikuwa ikisikika licha ya kwamba saizi haisikiki tena.

Lengo la hao Al Shabab inasadikiwa ni kutoka kuwakomboa wenzao ambao wamefungwa au wapo Magerezani. Kwa mantiki hiyo, sakata kubwa lipo katika ulinzi wa Magereza ambapo wanasema ni wakati wa kulipa kisasi makubwa ambayo waliyataja ni Gereza Lilungu lililopo Mtwara, Gereza Arusha na Gereza Segerea lililopo Dar.

Pamoja na hayo bado ukweli unabaki wazi wanaweza kuvamia gereza lolote ili kutimiza malengo yao.

Ni jukumu sasa la vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha hali haiwi alijojo.

Mungu Ibariki Tanzania.


sorce:jamii forum

0 comments:

Matokeo Kidato cha Nne 2014: Sekondari ya Kaizirege yaongoza


Shule za sekondari za binafsi zaongoza 10 bora matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam,Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA),Dk.Charles Msonde amesema katika matokeo ya kidato cha nne ya mtihani wa mwaka jana ufaulu umeongezeka kwa asilimia 12.67 ikilinganishwa na mwaka 2013.

Katika matokeo hayo msichana wa shule ya sekondari ya Baobab ,Nyakaho I. Marungu ndio aliyeongoza mtihani huo na kufatia wavulana.

Shule za Sekondari za St.Fransis ya mkoani Mbeya wanafunzi sita na Feza wanafunzi nane na kufanya shule hizo kuingia katika 10 bora kwa kutoa idadi wanafunzi wengi ikilinganishwa na shule zingine.

Msonde amasema matokeo hayo yanatokana na mfumo mpya wa GPA kwa kuangalia masomo saba hivyo ufaulu umetokana na mfumo huo.


Bofya hapa

Jiridhishe kwa kutembelea NECTA

Siku hizi hakuna Divisions, na tafsiri ya GPA ni hii hapa kwenye jedwali, Distinction ndio kama Division I ukipenda.

http://www.necta.go.tz/files/utaratibu_wa_kutunuku.pdf


DISTINCTION MERIT CREDIT PASS FAIL
GPA 3.6 - 5.0 2.6 - 3.5 1.6 - 2.5 0.3 - 1.5 0.0 - 0.2

Qualifying Test (QT): Tembelea HAPA

0 comments:

Mbinu 20 za kufufua penzi lenu leo siku ya valentine day


Image result for love
1.Badilisha mavazi yako .
Ikiwa bidhaa za kampuni unayoipenda zinabadilika baada ya miaka michache ili kupata umaruufu kwa wateja wake,pia wewe badilisha sura yako kwa kubadilisha mavazi na mfumo wa nywele ili umfurahishe mpenzi wako.
Hata kama umekuwa ukipendeza kwa mavazi yako, mpenzi wako tayari amekuzoea hivyo.
Nunua nguo mpya, chupi mpya, jaribu mtindo mwingine wa kutengeneza nywele ndiposa mpenzi wako akuone kama mgeni vile.
2. Hamia nyumba mpya
Ukiwa umekuwa ukiishi katika mtaa mmoja kwa miaka mingi ,badilisha maeneo yako.
Gura kwenda kwenye mtaa mpya, hili litakusaidia Kubadilisha mazingira na itaisisismua akili na kufurahia mukiwa pamoja.
3. Badilisha mfumo wa chumba chako cha kulala.
Panga vitu upya,ondoa vitu za kitambo,nunua vitu vipya,paka rangi tofauti tofauti kwenye ukuta wako.
Chumba cha kulalia kinapaswa kuwa cha kuvutia mno, badilisha mipangilio ya chumba chako mukiwa pamoja na mpenzi wako ndivyo nyiyi wote mumiliki mabadiliko hayo.

4. Omba msamaha nawe umsamehe.
Ni vigumu kuwa na urafiki wakati masuala tata kati yenu hayajatatuliwa.
Usipuuze maswala ambayo ni kawaida katika uhusianio,upendo wa dhati sio eti kwa sababu hamgombani wewe na mpenzi wako
Upendo wa dhati ni uwezo wa kusuluhisha matatizo kati yenu.
Omba msamaha wakati umekosea nawe msamehe wakati umekosewa.
5. Endeni mjivinjari kwa tarehe
Endeni likizo au tokeni nje pamoja.
Mkiwa nyote kwenye kwenye mazingira mapya inaweleta nyote pamoja.
6.Kataeni hamu ya kutizama picha za kujamiana.
Watu wengi wanaohusiano hudhani kuwa kuangalia picha hizo za kujamiana ni kitu kizuri ilhali ni jambo hatari sana.
Jiulize mbona watu huangalia picha hizi?
Kwa ajili ya kusisimua hali yao ya ngono?.
Kutegemea picha hizi kusisimua fataki kati yenu inamyang'anya mpenzi wako mamlaka ya kukusisimua mwenyewe.
Je inammanisha kuwa mpenzi wako hawezi kukusisimua?
Kama ni hivyo picha hizi hazisaidi kutengeneza hali zinaharibu.
Picha hizi zinafanya mapenzi yawe duni ilhali ni mmoja wapo wa kuwa na mapenzi.
Rudisha mapenzi na uwacha picha hizo mbaya ndiposa mpenzi wako aweze kujisalamisha kwako na ni jukumu lenu kusisimuana hisia kali za mahaba ile umruhusu awe spesheli kwako nawe kwake.
7. Jisalimishe upya
Kama fataki katika yenu yamekuwa yakididimia tatizo ni lenu.
Je unampenda kama awali?
Je unanipenda kweli?
Ondoa hofu hizo kwa kumhakikishia penzi lenu.
Hii ndiyo sababu wapenzi husherekea penzi lao.
8. Weka mtoto mbali na maswala yenu ya Huba.
Ni vizuri kuwa na watoto na kuwa karibu nao lakini wakti mwengine ni vyema watoto kuwa mbali na wazazi ili waweze kuwa na mda wao wa kipekee .
Tunza watoto kutokana na penzi lenu, penzi lenu likiingiiliwa kati basi uwezo wenu kama wazazi utaadhirika.
9. Epuka kuumiza mwenzako
Punguza visa vya kumuudhi na kumumiza mwenzako.
Roho iliyoumizwa ni vigumu kupenda.
10. Mbusu mpenzi wako zaidi.
Mabusu huleta watu pamoja.
Unavyo mbusu zaidi ndivyo munavyo chochea penzi.
11. Omba
Mungu anajali kuhusu penzi lenu na ndoa yenu.
Ombeni kwa pamoja kuhusu shida za penzi lenu.
12. Tenga wakati wa Faragha
Tenga wakati mahsusi kwa mpenzi wako.
Wanandoa wengi huwa na wakati mgumu sana kutenga muda maalum kuwa na wapenzi wao kutokana na majukumu ya maisha kama vile kazi safari watoto na kadhalika lakini
Jitahidi uweke kando muda maalum ambao utakaa karibu naye msemezane
Mkumbatiane mkumbushane haswa mlikotoka na mnakokwenda .
Ni muhimu sana.
13. Usilete majukumu yako ya kikazi nyumbani.
Ni vyema kufanya kazi ili kujipatia riziki yako na familia yako lakini kazi hiyo isalie kule afisini wala isiletwe nyumbani kamwe.
Usije na kazi yako ndani ya chumba chenyu cha kulala au ufanye mpenzi wako ahisi kuwa unamnyanyasa kwa sababu licha ya kuwa ulimuuowa mpenzi wako lakini umeoleka kwa kazi yako.
14. Weka teknolijia mbali
Teknolojia ni nzuri maanake inakupasha yanayojiri papo hapo .
Pia inawakutanisha hata mkiwa mbalimbali ,lakini ukiwa na mpenzi wako mbona usiiweke hiyo simu ama Kompyuta mbali ?
Mpenzi wako anataka kuongea nawe,kukubusu,kukumbatia kuwa karibu yako anataka kuisikia sauti yako lakini macho yako yanijishughulisha na kuongea kwa simu,mtandao wa kijamii ama unachapisha ujumbe .
Je nayeye akianza kuienzi kompyuta yake kuwasabahi jamaa na marafiki kwenye mitandao ya kijamii kutakuwepo na ndoa ?
Ukiwa nyumbani na mpenzi wako jiepushe na Teknolojia .
15. Chezeni pamoja
Kucheza pamoja kunaimarisha mahaba.
Haijalishi kama mpenzi wako anajua kupiga densi zaidi yako au la , Mkiwa pamoja weka mziki anaoupenda kisha mwite aje mpige naye rhumba,salsa Bongo flava, reggae ,hip hop hata Chakacha kama ni mwenyeji wa pwani !
Chezeni miili yenu ikigusana!
16 Kaeni msemezane
Mkiwa kitandani na mpenzi wako mnazungumza ?
Unamwambia nini kitandani ?
Unazungumzia kuhusu madeni yako?
Usidhubutu ,mwambie kuhusu mahitaji yenu ya kimahaba ,mwambie unampenda na kuwa haujui ungelikuwa wapi bila yeye .
17. Andikianeni barua za kimapenzi.
Mwandikie barua za kimapenzi na uiache kwenye gazeti au kwenye tarakilishi ,kitu ambayo itamfanya afurahie,kutoka kwa mwandiko wako.
18. Puuza watu ambao watakuvuruga amani kati yenu
Hao watu wanaokutongoza kupitia kwenye mitandao ya kijamii ima ni Facebook,WhatsApp wazuie wasikutumie ujumbe wa moja kwa moja.
Ni mahasidi hao,wala hawakupendi Ng'ooooo!!!!
Wao wangalikupenda kweli hawangejaribu kukuletea huzuni kwa kuvunja penzi/ndoa yenu.
Kujihusisha nao inapunguza makali ya penzi lenu ukidanganyika kuwa unapendwa ilhali ni Wanafiki tu
19.Nunua marashi mapya
Mnunulia mpenzi wako marashi yanayonukia vyema yatakayo fanya mpenzi wako afurahie kuwa nawe.

20.Jiachilie
Kuwa na uwazi wa mawazo ukiwa na mpenzio
Jaribu njia tofauti za kufanya mapenzi
Zungumzeni kama ambao mnaigiza sinema za mahaba
Mchezee shere
Mtanie mpenzi wako



0 comments:

unauhakika unalala vy kutosha utafiti kuhusu usingizi huu hapa



Baadhi ya watu hutanabahi wanapokuwa hawajapata usingizi wa kutosha,lakini ni wa kutosha kwa kiasi gani? Utafiti uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani, unapendekeza kuwa jibu la swali hilo, hutegemeana na umri wako!
Ukosefu wa kawaida wa usingizi,unywaji wa pombe,ama vimiminka vyenye kuamsha hisia za mwili ,kama kahawa,vichechemua mwili,usihesabu kengele ya saa asubuhi yenye kuashiria muda wa kuamka na jua lasiku,hivi vyote vinaingilia utaratibu wa mwili kwa kawaida hujulikana kama saa asili.
Kitengo cha utafiti kutoka nchini Marekani kijulikanancho kama US National Sleep Foundation (NSF), kilichoko Arlington, huko Virginia, kinaeleza kuwa maisha ya mtu mzima huonesha mahitaji ya usingizi,lakini kuna maelezo zaidi kulingana na umri ulionao.
Watoto wachanga wenye umri kati ya 0 hadi miezi mitatu wao wanapaswa kulala kati ya saa 14 hadi 17 kila siku,lakini hata akilala muda wa saa 11 hadi 13 inaweza kuwa sawa.lakini inashauriwa kulala zaidi saa 19.
Watoto wenye umri wa miezi 4 hadi 11 muda wa kulala kwa watoto wa umri huo unashauriwa kuwa kati ya saa kumi na mbili hadi kumi na tano,laikini walau alale kwa saa kumi inatosha sana,na si sawa tena haishauriwi mtoto alale kwa zaidi ya saa kumi na nane.
Walio na umri wa mwaka mmoja hadi miaka miwili wao wanashauriwa kulala kati ya saa kumi na moja hadi kumi na nne ,lakini muda uliokubalika ni saa tisa hadi kumi na sita.Wale wanaotarajiwa kuanza shule wenye umri wa miaka mitatu hadi mitano, watalaamu wanashauri walale si chini ya saa nane ama zaidi ya saa kumi na nne .Wanafunzi wa shule za awali wenye umri wa miaka sita hadi kumi na sita wao wanashauriwa kulala kwa saa tisa hadi kumi na moja,na kiafya endapo watalala chini ya saa saba ama zaidi ya saa kumi na mbili haishauriwi kiafya.Watoto wanaopevuka wenye umri wa miaka kumi nan ne hadi kumi na saba saa wanazo shauriwa kulala ni saa nane hadi kumi. Lakini NSF wanaonya wasilale zaidi ya saa kumi na moja ama chini ya saa saba.Wenye umri wa kati ,nazungumzia miaka kumi na nane hadi ishirini na tano ,inashauriwa watu wa umri wa kati walale saa saba hadi tisa ,lakini isiwe chini ya saa sita na si zaidi ya saa kumi na moja.Watu wazima wenye umri wa miaka ishirini na sita hadi sitini nan ne ni sawa na wale waumri wa kati hapo juu.Na wale wenye umri wa miaka sitini na tano na zaidi kwa afya zaidi, muda wa kulala ni saa saba hadi nane kwa siku lakini si chini ya saa tano ama zaidi ya saa tisa.
Wataalamu wa usingizi NSF wamechapisha orodha ya maelezo ya kuboresha kiwango cha usingizi zaidi.
Kwanza na zaidi ya hapo wanasema kwamba usingizi ama kulala kunapaswa kupewa kipaumbele,lakini wataalamu hao wanasema kwamba dondoo hizi zifuatazo nazo ni muhimu kwa afya na usingizi wako.
Zingatia muda wako wa kulala,hata mwishoni mwa juma.Buni namna na mbinu za kupumzika vyema zaidi iwe kama ibada iso badilika badilika. Fanya mazoezi kila sikuHakiki masula ya kiwango cha joto chumbani nah ii ikiwa ni pamoja na sauti pamoja na taa za chumbani.Lala katika godoro linalokupa raha na starehe na hata mito nayo pia ikupe pumziko .Epuka vinywaji vizuiavyo usingizi kama kahawa na pombe.Zima vifaa vya umeme.

0 comments:

uzinduzi wa video #Vuvula na #Kaunyaka Escape 1 Dar es Salaam jana






.
.
Usiku wa Feb7, Madee, Chege na Temba wamezindua video mpya za single zao ziitwazo ‘Vuvula’ & ‘Kaunyaka‘, video hizo mbili zimeongozwa na Adam Juma.
Uzinduzi huo ulifanyika kwenye ufukwe wa Bahari ya hindi, Escape 1 Dar es Salaam.
Wasanii waliotoa burudani ya nguvu kwenye uzinduzi huo akiwemo Barnaba, Vanessa Mdee, Julio, Shaa, Dogo Janja, Raymond kutoka Tip Top Connection na wengineo.
.
Chege na Mh. Temba.
Ads by Cinema-Plus-1.8cAd Options
.
Chege.
.
Yamoto Band.
.
.
Ad Options
.
.
.
Dogo Asley.
.
Vanessa Mdee.
Ads by Cinema-Plus-1.8cAd Opt
.
.
.
Barnaba na Vanessa Mdee.
.
Jux.
s by Cinema-Plus-1.8cAd Options
.
Shaa.
.
Julio.
.
Dj Tass kutoka Magic FM.
.
Dj K U kutoka Times FM.
.
Dj Romy Jons.
.
Professor Jay.
.
Madee.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
credit:milard ayo

0 comments:

JAY Z NA KANYE KWENYE Roc Nation Pre-GRAMMY Brunch in LA

Pics from the Roc Nation Pre-Grammy brunch in LA today. Kim K, Kanye, Jay Z, Gayle King, Kelly Rowland, Big Sean and others. More pics after the cut...



 

0 comments:

JAY Z NA KANYE KWENYE Roc Nation Pre-GRAMMY Brunch in LA

Pics from the Roc Nation Pre-Grammy brunch in LA today. Kim K, Kanye, Jay Z, Gayle King, Kelly Rowland, Big Sean and others. More pics after the cut...



 

0 comments:

NYUMBA YA JUX INAONESHA DHAHIRI MZIKI UNALIPA

jux2
Jux mjengo

0 comments: