kama wewe ni shabiki wa Manchester United hii taarifa inakuhusu
Klabu ya Manchester United imewaonya mashabiki wake kuwa wanalazimika kununua tiketi kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kombe la FA dhidi ya Cambridge United na wakishindwa kufanya hivyo watapata adhabu .
Klabu hii imewaandikia mashabiki wake ambao bado hawajalipia tiketi za mchezo huo barua maalum ikiwataka waharakishe kununua tiketi na wakishindwa kufanya ghivyo watazuiwa kuingia uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Sunderland .
Mashabiki
wa United wanaonunua tiketi za msimu wamelazimishwa kununua tiketi za
mchezo wa marudiano wa kombe la FA kati ya United na Cambridge .
Uongozi wa United umesema kuwa hatua hii ya kuwatishia mashabiki kununua tiketi ni moja kati ya sheria ambazo amshabiki hukubaliana nazo kama masharti ya msingi ya kuwa mnunuzi wa tiketi za msimu .
Endapo
mashabiki hao hawatanunua tiketi watazuiwa kuingia uwanjani kwenye
mchezo dhidi ya Sunderland kwenye ligi kuu ya England .
United ilitoka sare ya 0-0 na Cambirdge hali iliyolazimu mchezo huo kurudiwa jumanne ijayo kwneye uwanja wa Old Trafford.
source:milard ayo
0 comments: