Roma atoa sababu za kwanini hutoa wimbo mmoja kwa mwaka
Rapper Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki& amesema kile kinachoonekanan kama
ukimya wake kinatokana na desturi aliyojiwekea tangu aanze muziki wa kutoa wimbo mmoja
kwa mwaka.
Akizungumza na Bongo5 leo, Roma amesema ukiona yupo kimya katika muziki ujue anafanya
shughuli za kiujasiriamali ambazo ni tofauti na muziki.
Mwaka jana hakukuwa na kimya chochote kwa mtu anayemjua Roma kwa miaka yote,
amesema Roma. Roma kwa mwaka anatoaga wimbo moja. Kwahiyo mtu yoyote ambaye ana ‘judge’
kwanini Roma alikuwa kimya, ujue huyo kamjua Roma juzi.2007 ilitoka nyimbo ya kwanza, 2008
nyimbo ya pili, na nyimbo sita, kwahiyo kila mwaka natoaga nyimbo moja,sijawahi kutoa
nyimbo mbili kwa mwaka. Kwa mwaka jana ni 2030. Nilikuwa kimya kwasababu ndio nyimbo
iliyokuwa inachezwa.Na mwaka huu nitatoa nyimbo moja nanitakuwa kimya mpaka mwakani ndio
kawaida ya Roma.
Nimeandaa nyimbo kama sita ndani ya ‘Tongwe records’ sema ni kuchagua nitoe nyimbo gani
kwa mwaka huu. Sema nilikuwa kimya kidogo kutokana na majukumu ya maisha.Kama kawaida ya
Roma ni nyimbo moja kwa mwaka, hata wimbo wangu 2030 ulitoka 28/12/2012. Lakini wimbo huu
ni wa mwaka 2013 ndio maana ulipata air time nzuri 2013,” aliongeza.
Katika hatua nyingine, Roma amesema mwaka huu anatarajia kurudi shule baada ya kuhitimu na
kushindwa kuendelea kutokana na muziki.
Mimi ni mjasiriamali pia najarajia kurudi shule hivi karibuni,kwasababu nilihitimu
nikashindwa kuendelea,ila mwaka huu nadhani suala la kurudi shule ni miongoni mwa mikakati
yangu kwa mwaka huu.
0 comments: