Serikali ya Tanzania imethibitisha mradi wa Treni za juu kama hizi kujengwa Dar hivi karibuni.


Screen Shot 2014-05-15 at 4.52.21 PM
Umekua ni usafiri mwingine mzuri na wenye starehe yake kama ukipata nafasi ya kuutumia kwenye nchi zilizoendelea kama Marekani, Uingereza Dubai na kwengineko ambako kuna watu wengine wanategemea sana kuutumia na kuacha magari yao nyumbani na kujikuta wamewahi town na kumaliza shughuli zao manake hamna foleni.
Dar es salaam likiwa jiji la tisa kwa ukuaji duniani huku kwa Afrika likishika nafasi ya tatu, limekua na foleni kubwa ambazo mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) inasema huwa kila siku inapatikana hasara ya shilingi BILIONI TATU kutokana na foleni Dar es salaam.
Screen Shot 2014-05-15 at 4.53.09 PM
Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe ameongea na TBC1 na namnukuu akisema ‘mradi unaanza wakati wowote mapema iwezekanavyo manake wenzetu tayari wanazo pesa hivyo ni sisi kukimbia tuanze mara moja huu mradi, barabara za juu za treni zinatengenezwa viwandani moja kwa moja hivyo kazi ni kuzisimika tu barabarani ndio maana haitochukua muda mrefu kukamilika’
Elisha Elia alimuuliza Mwakyembe… Je umeme wa bongo tunavyoufahamu na historia yake utafaa kuuwezesha usafiri huo wa Treni kufanya kazi yake? manake treni hizi za kasi zinatumia umeme.
Akajibiwa ‘hawatotumia umeme wa TANESCO, watatumia umeme wa solar na vyanzo vingine vya umeme ili isitokee treni ikasimama katikati manake umeme ni lazima uwepo kwa saa 24′
Screen Shot 2014-05-15 at 4.53.27 PM
Kazi hii ya ujenzi wa barabara za juu za treni na treni zenyewe Dar es salaam itafanywa na jopo la wawekezaji ambao tayari wameshakubali kuwa tayari kuifanya hii kazi kwa kuanzia Dar es salaam, baadae Arusha kisha Mwanza na kwa Dar es salaam mradi huu kwa kuanzia utatoa ajira kwa zaidi ya watu elfu moja.
credit to:milard ayo

0 comments:

Taarifa kuhusu kutangazwa kwa kocha mpya wa Man Utd


giggs-van-gaal 
Wiki kadhaa baada ya kumtimua kocha David Moyes klabu ya Manchester united wanakaribia kumtangaza kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis van Gaal kuwa meneja mpya wa timu hiyo.
Mholanzi huyo tayari ameshakubali kuchukua madaraka ya ukocha Old Trafford lakini bado ana kazi ya kuiongoza Uholanzi kwenye michuano ya kombe la dunia na maandalizi ya kujiandaa na michuano hiyo yamesababisha dili lake na United kuchelewa kukamilika.
Mwanzoni iliripotiwa kwamba angetambulishwa mwishoni mwa wiki hii lakini badala yake ameendelea kubaki nchini Uholanzi na inaaminika sasa atatambulishwa wiki ijayo baada ya mchezo wa kirafiki.
Jana Ryan Giggs ambae ameshika madaraka ya ukocha kwa muda alisafiri mpaka Uholanzi ambapo alikutana na Van Gaal mjini Noordwijk kwa ajili ya kuzungumza juu ya Giggs kupewa madaraka ya kocha msaidizi pamoja na mipango ya usajili msimu ujao.

0 comments:

Solange mdogo wake beyonce amefuta picha zake na Beyonce insta akaacha hii tu, tazama alichofanya Beyonce


Screen Shot 2014-05-15 at 6.10.44 AM
Kwa wale mnaofatilia stori za mastaa, ikiwa ni chini ya saa 48 toka iripotiwe kwamba Solange ameziondoa kwenye page yake ya instagram picha alizopiga na dada yake yaani Beyonce, B amejibu kwa kufanya maamuzi ya kuweka kumbukumbu za hizi picha nne alizopiga na Solange.
Mwanzoni ilionekana ugomvi ni kwa Solange na Jay Z ila kuna kitu kinaendelea manake uamuzi wa Solange kufuta picha za Beyonce kwenye insta yake umekuja baada kusambaa kwa video ikimuonyesha yeye (Solange) akimpiga Jay Z kwenye lift ya hoteli huku Beyonce akiwa pembeni akishuhudia bila kuingilia kati hata kwa kumzuia Solange.
Screen Shot 2014-05-15 at 6.25.45 AM
Screen Shot 2014-05-15 at 6.34.29 AM
Hii ndio picha pekee Solange aliyokua kaibakiza kwenye instagram yake lakini sasa hivi haionekani na kuna uwezekano ameshaifuta tayari.
Saa kadhaa baada ya picha zake kufutwa na Solange, Beyonce alipost picha 4 akiwa na Solange ndani ya saa 17 huku moja tu ndio ikiwa na caption ya ‘good morning’ ila nyingine hajaandika kitu.
Screen Shot 2014-05-15 at 6.30.27 AMImeripotiwa kwamba hakuna maelewano mazuri kati ya ndugu hawa wawili Beyonce na mdogo wake Solange.
Screen Shot 2014-05-15 at 6.30.41 AM
‘Good morning’
Screen Shot 2014-05-15 at 6.37.22 AM
Baada ya Solange kuonekana akimpiga Jay Z kwenye lift zilitoka stori za chinichini kwamba Rihanna ndio chanzo cha yote ambapo Beyonce amezikanusha hizo stori kwa kuweka picha akiwa na Rihanna kuonyesha kwamba kila kitu kiko poa.

0 comments:

Diamond amechaguliwa kwenye hizi tuzo za BET Marekani.


BET DIAMOND PLATNUMZ 2014 2
Ilikua stori kubwa pale Diamond Platnumz alipotangazwa kushiriki kwenye tuzo za MTV Base (Mama Awards) kikiwa ni kituo kingine kikubwa cha burudani Afrika.
Leo hii Diamond Platnumz ameingia kwenye stori nyingine kubwa ya dunia baada ya kuchaguliwa kushiriki kwenye tuzo za Television kubwa ya Marekani ya BET ambapo yupo kwenye kipengele cha wanaogombea BEST INTERNATIONAL ACT AFRICA.
Anaigombea hiyo tuzo na Davido wa Nigeria, Mafikizolo wa South Africa, Tiwa Savage wa Nigeria, Toofan na Sarkodie wa Ghana. the OFFICIAL nominees 2014!….
BET kupitia page yao ya twitter waliandika kuthibitisha kuchaguliwa kwa Diamond na kumpongeza akiwa pia ni msanii pekee wa Afrika Mashariki kwenye tuzo hizi za mwaka huu.
BET DIAMOND PLATNUMZ 2014

0 comments:

Baada ya tetesi za Kipre Tchetche kwenda Yanga –haya ndio majibu ya Azam


mg 6
Karibia magazeti yote ya michezo leo hii yameripoti taarifa za mchezaji kimataifa wa Ivory Coast anayekipiga Azam FC kuwa mbioni kwenda Yanga.
Lakini mchana huu kupitia akaunti yao rasmi ya mtandao wa Facebook klabu ya Azam FC imetoa taaifa ifuatayo:
azam copy

0 comments:

FEDHA FEKI ZACHANWA LIVE NJIA PANDA CLOUDS FM


Kama ulikuwa makini kusikiliza kipindi cha njia panda jana kilichokuwa kikiongozwa na Dr. Isaac Maro na kusikiliza kisa na mkasa uliomkuta msimuliaji aliyepachikwa jina la bandia 'Baraka' (Kwa ajili ya kulinda usalama wake), sasa zile pesa zilizokuwa zikiongelewa kuwa ni feki huu ni mfanowe. 
Kisha Pesa hizo feki zilichanwa chanwa live ili kudhihirisha umma kuwa Njia panda na Clouds Fm haiungi mkono biashara haramu ya fedha bandia.

0 comments:

Alichoandika Micheal Carrick baada ya kutemwa timu ya taifa


carrick_1716041aMuda mchache baada ya kocha Roy Hodgson kutangaza kikosi cha timu ya taifa ya England kitakachokwenda Brazil, mchezaji wa klabu ya Manchester United aliyeachwa Micheal Carrick amezungumza kupitia mtandao wa Twitter.
Carrick ambaye ameachwa na nafasi yake kuitwa kiungo Jordan Henderson wa Liverpool, amesema amesikitikishwa na kuachwa na imemuumiza sana kuikosa michuano ya kombe la dunia, lakini ataishangilia kwa moyo mmoja timu yake itakapokuwa inapambana nchini Brazil.
carrick

0 comments:

PICHA 40 ZA KIWANDA KIKUBWA CHA SARUJI KULIKO VYOTE DUNIANI CHA DANGOTE, NIGERIA ZIPO HAPA

 Kiwanda kikubwa zaidi cha saruji kuliko kingine chochote duniani cha Dangote Cement Obajana Plant kutoka angani. 
 
  Kiwanda kikubwa zaidi cha saruji kuliko kingine chochote duniani cha Dangote Cement Obajana Plant kutoka angani
 Sehemu ya kijiji jirani na kiwanda hicho
 Kwa mbele ni malori yaliyopanga foleni kwenda kubeba saruji kiwandani hapo
 Nyumba za wafanyakazi pamoja na mkanda wa kusafirisha mali ghafi toka machimboni
 Machimbo ya kiwanda cha saruji cha Dangote
 Malori zaidi yakiwa yanangoja zamu ya kwenda kupakia mzigo kiwandani
 Ulinzi ni wa uhakika
 Ndege binafsi za Dangote zikiwa zimepaki katika uwanja binafsi wa kiwanda hicho
 Alhaj Dangote akiongea na mkuu wa polisi wa eneo hilo akiwa na binti yake Halima na mameneja wa kiwanda
 Alhaj Dangote akiongea na Dada Esther, mmoja wa wasaidizi wake katika ujenzi wa kiwanda cha Mtwara
 Sehemu ya mkanda wa kusafirisha mali ghafi toka machimboni hadi kiwandani
 Sehemu ya malori yanayofanya kazi kiwandani hapo
 Sheli ya kiwanda
 Malori kazini
 Sehemu ya machimbo
 Kisima kirefu cha maji
 Sehemu ya kiwanda
 Silo na maghala ya malighafi
 Moja ya benki 13 zilizofunga kambi kiwandani hapo
 Tawi la benki ya Access kiwandani hapo
 Sehemu ya  maegesho ya malori
 Mkanda wa malighafi
 Sehemu ya kituo cha kuzalishia umeme
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kichina wakkitoka kupata mlo wa mchana
 Malori yakiwa tayari kupeleka mzigo kunakohusika
 Mixer
 Seehemu ya kiwanda
 Mmoja wa wasimamizi wa wafanyakazi kiwandani
 Taswira ya sehemu ya kiwanda
 Kiwanda
 Foleni ya maori kuelekea kiwandani kubeba mzigo
 Sehemu ya kiwanda
 Ndani ya ghala la malighafi
 Mkanda wa kuchukua malighafi toka machimboni
 Bango la uzinduzi wa awamu ya kwanza na ya pili
 Wahandisi wakifuatilia kila hatua ya uzalishaji kidigitali
 Mitambo ya kufuatilia uzalishaji
 Mhandisi kazini
 Baadhi ya wafanyakazi waandamizi
 Baadhi ya wafanyakazi baada ya kumaliza shifti
Alhaj Aliko Dangote akiwapa maelekezo rubani na mhudumu wa ndege yake binafsi katika uwanja wa ndege wa kiwanda chake cha saruji cha Obajana

0 comments: