Huyu ndio Mwanamke ‘mzungu’ anaedai kufa na kwenda mbinguni kisha akarudi duniani

Mary
Kituo cha TV cha CNN ambacho kimeshinda tuzo kutokana na ubora wa kazi ya kutangaza habari wanayoifanya toka kuanzishwa kwake mwaka 1980, kimetoa ripoti ya Watu watatu wenye ushuhuda wa maisha yao ambao walikufa na kuacha miili yao duniani, kisha wakaenda mbinguni na kurejea tena duniani ambapo huyu hapa chini ni mmoja wao.
Mwanamke huyu Daktari aitwae Mary raia wa Marekani January mwaka 1999 alimchukua mume wake na kumzawadia safari ya kwenda Chile kusherehekea birthday yake ambapo walipofika nchini humo wakiwa na mpango wa kukaa kwa siku kadhaa walifanya kila walichopanga kufanya kwa siku hizo hivyo ikawa imebaki siku moja,yani siku ya mwisho ambayo mume wake aliamka akiwa anaumwa mgongo hivyo hakuweza kwenda kutembea na hizo boti mtoni kama kawaida yao.
Yani kuna zile boti ndogo za mtu mmoja mmoja ambazo unaingia unanyoosha miguu yako kwenye sehemu ya mbele alafu unaanza kuliendesha mwenyewe.
Katherine Brady
Kwa sababu mume alikua anaumwa mgongo, mke aliamua kwenda kutembea mwenyewe na boti siku ya mwisho… hata hivyo haikua sawa kwake pia, alikua kama anasitasita lakini akaenda hivyohiyvo alafu akatembea na boti kwenye sehemu yenye maporomoko makubwa ya maji, yenye umbali wa futi 10 mpaka 15 ambako boti yake ilizama kwenye moja ya maporomoko na akajikuta amekwama katikati ya miamba chini ya maji.
Anasema alikua na uhakika kwamba anakufa kwa sababu alikaa muda mrefu kwenye maji hivyo akaamua kumuachia Mungu kila kitu na bada ya hapo tu akahisi kama muujiza, kuna nguvu imemkumbatia na ikawa inamuhakikishia kwamba kila kitu kitakua sawa kwa upande wa mume wake na watoto, hapo ndio akaamini mtu ambae anaamini ni Yesu Kristo alikua amemkumbatia.
mary 8
Akawa anajiuliza maswali kuhusu hiki kitu ambacho ni cha ajabu kwake, alipoulizwa na Mtangazaji kama alikua anajitambua wakati akiwa mikononi mwa Yesu, Mama huyu amekiri ndio alikua anajitambua mpaka alikua anaona maji na bado pia alikua amebanwa kwenye boti.
Ghafla kila kitu kilibadilika akaona malaika wanajadiliana na Yesu, akaona wale waliokua wanamtafuta wameshaona jiwe ambalo halijukani lilitokea wapi ila halikuepo mwanzoni na kisha wakamuona yeye baada ya kulifata hilo jiwe, akasaidiwa na kutolewa akiwa ameshabadilika rangi kabisa.
heaven and back 2
Kwa kawaida binadamu akikaa kwenye maji kwa dakika 10 anakufa ila yeye alikaa kwa dakika 30 lakini akatoka akiwa hai lakini alikua ameshabadilika rangi na kuvimba mwili pia ambapo anasema katika mazungumzo yake na Yesu, kuna malaika mmoja alimwambia kwamba mtoto wako atafariki siku kadhaa zijazo, na kweli mtoto alifariki wakati akiwa kwenye michezo.
Kabla ya hapo mama huyu alikua anasita kumwambia mume wake lakini mtoto alivyofikisha miaka 18 ndio ikabidi amwambie kuhusu hizo habari za kifo.
Umemuamini huyu mama na hii stori yake?
source:milard ayo

0 comments: