huu ndo  ujumbe aliouandika Jackie Cliff kwa Martin Kadinda ikiwa atakufa.

Martin Kadinda na Jackie Clif
Jackie Cliff na Martin Kadinda ambae ni meneja wa mwigizaji Wema Sepetu ni marafiki wa siku nyingi ambao wamekua wakionekana pamoja kwenye matukio mbalimbali ndani ya Dar es salaam.
Kutokana na ukaribu wao kama Marafiki pamoja na hili tukio lililomtokea Jackie huko Macao kwa kukamatwa na dawa za kulevya, hii status ya BBM imeonganishwa fasta na kuonekana kama ndio kitu cha mwisho Jackie alichokisema kuhusu maisha yake.a3853fb3862d450baca5a4282c0c0d81Martin Kadinda amezungumza exclusive na millardayo.com na kusema ‘hii status kweli ni Jackie aliniandikia lakini sio ya leo, wengi wanadhani ndio kaiandika juzi lakini ukweli ni kwamba aliiandika siku nyingi sana tena hakuwa kwenye matatizo yoyote, kaiandika March 15 2012 ila blogs ndio zimeiunganisha na tukio la juzi’
‘Alisema vitu kadhaa vifanywe akifa na ameguswa na mstari mmoja wa Biblia kwamba ‘inabidi binadamu kukaa tayari wakati wowote maana hatujui siku wala saa’ na kuongeza kuwa kama akizikwa Iringa atapenda azikwe chini ya mti mkubwa wenye kivuli lakini kama atazikwa Dar, msiba uwekwe eneo la ndani lenye AC maana anajua rafiki zake ni watu wenye mashauzi’ – Martin
Jackie Cliff
Stori zote za town na zisizo za town, michezo, muziki, movies, vichekesho, siasa, maisha na stori nyingine zote zinapatikana on millardayo.com hivyo unaweza kuwa karibu na mtu wako wa nguvu kupitia facebook twitter na instagram kwa jina la Millard Ayo ili kuwa wa kwanza kupata stori zote zinazotokea.
source:milard ayo

0 comments: