Picha 7 za mwigizaji Lulu Mahakamani jana
jana February 17 kutoka Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam mwigizaji
Elizabeth Michael maarufu Lulu alikuwa akisomewa shitaka lake la kumuua
bila kukusudia msanii mwenzake wa maigizo Steven Kanumba April 07 2012
Vatican Sinza Dar es salaam.
Akisoma maelezo ya awali wakili wa serikali Monica Mbogo
mbele ya Jaji anayesikiliza kesi hiyo Rose Teemba, amesema siku ya tukio
kulikuwa na ugomvi kati ya marehemu na mshtakiwa na baadaye mshtakiwa
aliondoka usiku wa saa sita baada ya marehemu kuanguka chumbani ambapo
alfajiri ya february 07 saa 11 alfajiri Lulu alikamatwa eneo la Bamaga.
Wakili
Peter Kibatala ambaye anamtetea Lulu amesema wameridhishwa na sehemu
kubwa ya maelezo ya awali ya mteja wao ambapo kesi hiyo imeahirishwa
mpaka itakapopangwa tena huku kila upande ukitarajia kuleta mashahidi
watatu.
Wakili Kibatala ameongea na millardayo.com na kusema
>>> ‘leo kulikua na hatua mbili za kisheria huku ya kwanza
ikiwa ni Mshtakiwa kusomewa shitaka na anasema kama anakiri au anakataa
ambapo leo mshitakiwa amekataa shitaka, hatua nyingine ni kukubaliana
kwa pande mbili za Utetezi na mashtaka kuhusu maeneo gani ya kishahidi
na kisheria ambayo tunakubaliana nayo na yale tusiyokubaliana, huu ni
utaratibu wa kisheria kuhakikisha kesi zinachukua muda mfupi’
‘Hayo ndio tuliyofanya leo ambapo kesi itaendelea kwa
ratiba za Kimahakama, sisi kazi yetu kwa sasa ni kulinda maslahi ya
mteja wetu Lulu… leo kisheria ni ile siku ya mshtakiwa kusomewa kosa
ambapo sisi tumelikataa na baada ya hapo tukafanya maelezo ya awali ili
baada ya hapo Mahakama iweze kupanga ratiba ya kesi kutokana na vitu
gani tunabishania na tusivyobishania’
0 comments: