NEY WA MITEGO, "KATI YA WATU WALIOWAHI KUNIKOSEA SANA NI OSTAZ JUMA" STORI NZIMA HAPA
Ingawa wasanii wengi walilaani kitendo hicho, rapper wa Manzese, Nay wa
Mitego yeye aliiambia Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm kuwa kitendo
alichokifanya Ostaz Juma kupost picha zinazomuoenesha PNC akimpigia
magoti, kwa upande wake amemkosea yeye hata kuliko PNC mwenyewe.
“kumpigia mtu magoti kwa ajili ya kuomba msamaha ni sahihi. Lakini kuna
upigiaji wa magoti mwingine ambao baadae unaweza kuonesha picha mbaya
kuwa umedhamilia kumdhalilisha. Halafu Ostaz Juma hana nidhamu halafu ni
mtu ambaye hajitambui. Vijisenti anavyovipata nadhani ndivyo vinampa
jeuri ya kudhalilisha wasanii wenzetu, sio kitu kizuri.
Mimi tangu nilipoona hizo picha nilisema siwezi kumpenda hata siku moja,
hata salamu yangu siwezi kumpa. Siwezi kumheshimu hata kidogo.
Nitamdharau kuliko kitu chochote, kuliko mtu yeyote aliyewahi kunikosea
sana. Ila katika watu ambao waliowahi kunikosea, nafikiri mimi Ostaz
Juma amenikosea kupita maelezo. Kuliko alivyomkosea PNC mwenyewe.”
By TimesFm
By TimesFm
0 comments: