Picha 6 za H.baba akiwa kwenye kaburi la Cool James ‘Mtoto wa Dandu’
H.babakutoka Mwanza wikiendi iliyopita amefanya ziara ya
kutembelea familia ya James Dandu ambayo iko Mwanza ambapo pia alifika
mpaka lilipo kaburi lake Ngudu,Kwimba hapo H.baba alipalilia pamoja na
kutoa heshima zake kwenye kaburi la Muasisi huyu wa tuzo za Tanzania.
Mbali na kuwa muasisi tu Cool James ambaye alifariki Agost 2002
alikua ni miongoni mwa wasanii wa kwanza kuutangaza muziki wa Bongo
Fleva nje ya nchi,Hizi ni picha baadhi ambazo zinamuonyesha H.baba akiwa
na familia pamoja kaburi alilozikwa James Dandu.
0 comments: