Alichoandika Micheal Carrick baada ya kutemwa timu ya taifa


carrick_1716041aMuda mchache baada ya kocha Roy Hodgson kutangaza kikosi cha timu ya taifa ya England kitakachokwenda Brazil, mchezaji wa klabu ya Manchester United aliyeachwa Micheal Carrick amezungumza kupitia mtandao wa Twitter.
Carrick ambaye ameachwa na nafasi yake kuitwa kiungo Jordan Henderson wa Liverpool, amesema amesikitikishwa na kuachwa na imemuumiza sana kuikosa michuano ya kombe la dunia, lakini ataishangilia kwa moyo mmoja timu yake itakapokuwa inapambana nchini Brazil.
carrick

0 comments: