Solange mdogo wake beyonce amefuta picha zake na Beyonce insta akaacha hii tu, tazama alichofanya Beyonce
Kwa wale mnaofatilia stori za mastaa, ikiwa ni chini ya saa 48 toka iripotiwe kwamba Solange ameziondoa kwenye page yake ya instagram picha alizopiga na dada yake yaani Beyonce, B amejibu kwa kufanya maamuzi ya kuweka kumbukumbu za hizi picha nne alizopiga na Solange.
Mwanzoni ilionekana ugomvi ni kwa Solange na Jay Z ila kuna kitu kinaendelea manake uamuzi wa Solange kufuta picha za Beyonce kwenye insta yake umekuja baada kusambaa kwa video ikimuonyesha yeye (Solange) akimpiga Jay Z kwenye lift ya hoteli huku Beyonce akiwa pembeni akishuhudia bila kuingilia kati hata kwa kumzuia Solange.
Hii
ndio picha pekee Solange aliyokua kaibakiza kwenye instagram yake
lakini sasa hivi haionekani na kuna uwezekano ameshaifuta tayari.
‘Good morning’
Baada
ya Solange kuonekana akimpiga Jay Z kwenye lift zilitoka stori za
chinichini kwamba Rihanna ndio chanzo cha yote ambapo Beyonce
amezikanusha hizo stori kwa kuweka picha akiwa na Rihanna kuonyesha
kwamba kila kitu kiko poa.
0 comments: