Picha 40 za jinsi ilivyokua kwenye mwaliko wa WEUSI usiku wa April 30 2014
Kampuni ya WEUSI ambayo ina wasanii kama Joh Makini, Nikki wa II na G Nako ilifanya ile party isiyokua na kiingilio bali kadi maalum kwa kila aliealikwa ili kuitazama kwa mara ya kwanza video mpya ya ‘gere’ ambayo ilifanywa Nairobi Kenya wiki kadhaa zilizopita.
Watu mbalimbali wakiwemo kutoka kwenye makampuni makubwa Tanzania na Mastaa mbalimbali walijitokeza kwenye hoteli ya Mediterano Kawe Dar es salaam.
Mwimbaji anaesifika kwa voco na kiwango cha kipekee HISIA, aliwahi kuiwakilisha Tanzania Tusker Project Fame
Sehemu tu ya watu wakiitazama video yenyewe ambayo ilibidi irudiwe kuonyeshwa baada ya watu kunogewa na kutaka kuitazama zaidi
Baada ya video kutazamwa WEUSI walifanya show na hapa ni G Nako akicheza na V Money a.k.a Vanessa Mdee
0 comments: