Picha: Wasanii wa Kili Music Tour wawalivyowasili Songea
Wasanii watakaopanda jukwaani katika tamasha la ziara
ya Kili Music Tour wamewasili Songea asubuhi ya leo kwa ajili ya
onyesho hilo. Wasanii hao walioongozana na meneja wa Kilimanjaro Premium
Lager, George Kavishe waliwasili kwa ndege maalum wakitokea mkoani
Dodoma ambako jana walishiriki shughuli ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais
Jakaya Mrisho Kikwete. Baada ya kuwasili uwanjani moja kwa moja ya
wasanii hao walienda Jogoo FM ambako walifanyiwa mahojiano kabla ya
kwenda uwanjani kufanya majaribio ya sauti na jukwaa na baadae kwenda
hotelini kwa ajili ya kupumzika kabla ya show kuanza. Hizi ni baadhi ya
picha:
Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager George Kavishe alikuwa rubani msaidizi
Henry Mdimu aliamua kuonyesha anavyomsubiria kwa hamu Shilole
Linex akishuka kwenye ndege
Malkia Khadija Kopa akishuka kwenye ndege iliyowaleta wasanii toka Dodoma
Mwasiti akishuka kwa umakini ngazi za ndege
Diamond Platnumz akiteta jambo na Ommy Dimpoz huku akishuka kwenye ndege
Pozi kwa pozi kwenye ngazi za ndege
Shilole
Ben Pol akipokelewa na Innocent Nganyagwa ambaye ndiye msimamizi wa wasanii katika
Kili Tour
Gnako Warawara
Safari ya kutoka nje ya uwanja
Mwasiti akiwaongoza wenzake kutoka nje ya uwanja
Diamond akitoka jengo la abiria waliowasili
GNako akiingia ndani ya Tour Bus
Linex
Ben Pol Akiingia kwenye basi
Nikkki wa Pili na wasanii wengine ndani ya Jogoo FM
Ommy Dimpoz akihojiwa ndani ya Jogoo FM
0 comments: