picha: Kili Music Tour Songea ilivyobamba
Wakazi wa Songea wanashuhudia burudani toka kwa wakali wa muziki
nchini katika Kili Music Tour ambayo inaendelea hivi sasa uwanja wa
Majimaji. Hiki ndicho kinachojiri hivi sasa.
Mashabiki wakiendelea kukata tiketi za kuingia uwanja wa Majimaji
Bia moja ya bure kwa kila shabiki anaekata tiketi ya kuingia ndani
Eneo maalum la vinywaji na vyakula kwa mashabiki waliojitokeza uwanjani
Tayari mizuka ya Kili Music Tour imeanza uwanja wa Majimaji
Eneo la backstage litakalotumiwa na wasanii
Dullah na Zembwela wanaendelea kufanya amsha amsha kwa kuwapatia mashabiki bia za bure
Kili Music Tour Songea inafunguliwa nae Shilole
Backstage: Ben Pol akisubiri kupanda jukwaani
Malkia wa mipasho Khadija Kopa akiwarusha roho maelfu waliojitokeza uwanja wa Majimaji
Mashabiki wakiendelea kushangweka na rusha roho ya malkia wa mipasho
Backstage: Profesa Jay na Ben Pol
Mwasiti jukwaani na mmoja ya mashabiki waliopata bahati ya kuitwa kuimba nae
Linex mjeda akiwarusha mashabiki na nyimbo zake kali
Backstage: Meneja wa Kili George Kavishe akiwa na Joh Makini pamoja na Ommy Dimpoz
Zamu ya mkali wa R&B Ben Pol kuwaimbisha mashabiki
Dimpoz Pozi kwa pozi akiendeleza burudani
Mashabiki wakiomba kupewa jaketi la Ommy Dimpoz
Ommy Dimpoz akiimba kwa hisia kali wimbo wake wa Nani Kama Mama.
Wadau mbalimbali wakiwa na meneja wa Kili George Kavishe
Hakuna Songea bila ngoma ya lizombe ambayo ilitangulia kumkaribisha mtoto wa nyumbani
Profesa Jay jukwaani katika uwanja wa nyumbani
Diamond platnumz akithibitisha kwa nini alipata tuzo saba katika tuzo za Kili
Na hatimaye baada ya makelele mengi ya mashabiki Diamond alimpandisha mpenzi wake Wema Sepetu
DJ Summer wa East Africa Radio kazini
Zamu ya Weusi kuifunga show
Shabiki akipeperusha kitambaa cheusi kuonyesha mapenzi yake kwa Weusi waliokuwa jukwaani
Umati
huu uliojitokeza kwa wingi uwanja wa Majimaji ulitoka ukiwa umeridhika
na bonge la show lililotolewa na wasanii wote waliopanda jukwaani
0 comments: