taarifa nzuri kwa mashabiki Sunderland
Jermain Defoe akitabasamu wakati alipokuwa anaondoka kwenye akademi ya Light huko Sunderlnad baada ya kufanyiwa vipimo jana.
Jermain Defoe amewasili Sunderland tayari kujiunga na paka hao weusi, huku akisema ana hamu ya kufunga magoli.
Defoe jana alhamisi alifanyiwa vipimo vya afya katika akademi ya Light.
Mshambuliaji
huyo wa zamani wa England alijiunga na timu ya ligi ya Marekani,
Toronto majira ya kiangazi mwaka jana, lakini licha ya kufunga magoli 11
katika mechi 16 alizocheza baada ya kusaini mkataba wa miaka minne,
bado hakutulia na amekuwa akiwindwa na timu nyingi za ligi kuu England.
Defoe (kulia) anatarajia kusaini mkataba Sunderland akitokea timu kubwa ya soka ya Toronto.
Bosi
wa Sunderland, Gus Poyet ameshinda mbio za kumsaini mshambulizi huyo
mwenye miaka 32 ambaye anaamini atawasha moto na kuwaokoa paka weusi na
mkasa wa kushuka daraja.
0 comments: