hii ndo taarifa nzuri kwa mashabiki na wapenzi wa manchester united


24AC4B1100000578-2909619-image-a-11_1421233491627
Beki wa Everton, Seamus Coleman anahusishwa kusajiliwa na  Manchester United wakati huu wanahitaji kutatua tatizo la beki wa kulia
Manchester United wanatarajia kuwa na kikao leo ijumaa kuamua kama wanahitaji kutumia fedha nyingi kuboresha safu ya ulinzi wiki mbili zijazo.
Kocha wa United, Louis van Gaal anakutana na viongozi wa klabu hiyo kuweka mipango ya usajili katika dirisha dogo na majira ya kiangazi mwaka huu.
Kununua beki wa kulia itakuwa ajenda kubwa ambapo rada zao zinaangaza kumnasa beki wa Everton mwenye miaka 26, Seamus Coleman au wa  Southampton, Nathaniel Clyne mwenye miaka 23.
Southampton defender Nathaniel Clyne (left) has also been mentioned as a possible target for the Reds
Beki wa Southampton, Nathaniel Clyne (kushoto) pia anahusishwa kusajiliwa na mashetani wekundu.
Van Gaal ambaye tayari ameshatumia paundi milioni 156 tangu majira ya kiangazi mwaka jana, anahitaji kuimarisha kikosi chake kwa lengo la kufuzu ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao.

0 comments: