Mvumbuzi wa bunduki aina ya AK-47 Mikhail Kalashnikov afariki dunia

Mikhail Kalashnikov, mrusi ambaye alivumbua bunduki ya AK-47 ambayo 
imekuwa chaguo la majeshi ya mataifa mengi duniani, amefariki dunia  
jana (Dec 23) akiwa na miaka 94.
Silaha ya AK-47 ilibuniwa kwa mara ya kwanza mwaka 1942 lakini ilikuja 
kuzinduliwa na kuanza kutumika 1947 na jeshi la Urusi.
AK-47 imewahi pia kuingia katika kitabu cha rekodi za dunia ‘Guinness Book 
of World Records’ kama ‘World’s most common gun’.
Maana ya jina la AK linatokana na kifupi cha kirusi cha ‘Kalashnikov’s 
machine gun’, huku 47 inamaanisha mwaka ilipoanza kutengenezwa.

0 comments: