YANGA YAMTIMUA KOCHA WAKE ERNEST BRANDTS

MUDA mfupi uliopita klabu ya soka ya Yanga imetangaza kusitisha mkataba na kocha wake Ernest Brandts baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, mkataba wa Brandts ambaye ni raia wa Uholanzi umesitishwa rasmi leo hii asubuhi na ameshakabidhiwa barua ya kumtaarifu juu ya hali hiyo.

“Tumesitisha mkataba na kocha wetu na ameshakabidhiwa barua yake, huo ni uamuzi wa uongozi mzima wa Yanga, kila kitu kimeenda sawa katika kuachana naye,” alisema Kizuguto.

Tetesi za Brandts kutimuliwa zilizagaa jijini Dar es Salaam tangu jana muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji kwamba hata kama klabu itaamua kuachana na kocha huyo itafuata taratibu zote.

Uamuzi huo wa Yanga unaonekana pia kuchagizwa zaidi na kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Simba katika mchezo maalum wa kirafiki maarufu kama Nani Mtani Jembe uliochezwa wikiendi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

source:shafih dauda

0 comments: