Picha: Profesa J+Diamond +P-Funk =? Watatu hao waingia studio kuandaa msosi mtamu
Unapata picha gani pale the heavyweight MC anapokutana na ‘the Bongo Flava Prince’
kwenye wimbo uliotayarishwa na ‘Godfather wa Bongo Flava’.. Kwa wengi mchanganyiko
huo unatoa mnuso mzuri wa hit ya mwaka.
Basi ndicho kilichofanyika, Profesa Jay amemshirikisha Diamond Platnumz kwenye wimbo
wake mpya unaotayarishwa na producer wa Bongo Records, P-Funk Majani.
Wimbo huu utakuwa wa kihistoria hasa kwakuwa ni kazi iliyowakutanisha Profesa na P-Funk
baada ya miaka mingi ya kutofanya kazi pamoja. Majani anabeba sifa zote za kumtengeneza
Profesa Jay huyu ambaye kwa wengi anapewa heshima ya kuwa rapper anayeheshimika zaidi
kwenye historia ya muziki wa Bongo Flava.
Majani ndiye aliyekuwa kichwa nyuma ya hit za Jay zikiwemo Jina Langu, Ndio Mzee,
Zali la Mentali, Nikusaidieje na zingine kibao kwenye album ya mwaka 2001, Machozi,
Jasho na Damu. Sina shaka kuwa ujio wao mpya utakuwa wa kishindo.
Sababu ya pili kubwa ya kwanini collabo hii itakuwa ya mwaka, ni uwepo wa Diamond
Platnumz ambaye yupo katika kilele cha mafanikio huku akiwa amejikusanyia mashabiki
wengi kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na sasa hadi nchi zingine nyingi za Afrika
kutokana na collabo yake na Davido wa Nigeria.
Profesa Jay ambaye jina lake halisi ni Joseph Haule amepost picha kwenye Instagram
akiwa na wawili hao kwenye studio mpya za Bongo Records na kuandika: Studio session
at Bongo Records with the Super dupa producer P – Funk and Diamond Platnumz
himself COOKING for all yall!! Stay Tuned.”
We can’t wait..
0 comments: