ANGALIA PICHA MWILI WA MAMA YAKE MHE ZITTO KABWE ULIPOAGWA UWANJA WA NDEGE NA KUSAFIRISHWA KWENDA KIGOMA KWA MAZISHI

 

Zitto kabwe akiwa na Prof  Ibrahimu Lipumba wakati wa kuuaga Mwili wa mama yake kipenzi Bi Shida Salumu aliyefariki leo kabla ya kusafirishwa kwenda Kigoma kwa mazishi

Ndege Ikiandaliwa Ili kuweza Kuingiza Mwili wa Marehemu Mama yake Zitto Kabwe
Waheshimiwa Wabunge na Baadhi ya Viongozi wakibeba Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Mama Yake Zitto Kabwe Bi Shida Salum  kuingiza kwenye ndege Tayari kwa safari ya kwenda Kigoma Kwenye mazishi

Prof Ibrahimu Lipumba akijadili jambo na Mwezie baada ya kupakia mwili wa marehemu kwenye ndege kuelekea kigoma Kwenye maziko


Rais wa TASWA Juma Pinto akiwa VIP ya Terminal 1 JKN Airport alipokutana na Cardinal Pengo wakati wa kuaga mwili wa Mama yake Zitto Kabwe

 

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, (Wakwanza kushoto), baba yake mzazi Zuberi Kabwe (Wakwanza kulia) na waombolezaji wengine, wakiomba dua kwenye msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam huku picha ya chini, waombolezaji wakiingiza jeneza lenye mwilki za Saida Salum, mama mzazi wa Zitto, Jumapili Juni 1, 2014. Mama yake Zitto, alifariki mapema saa 5 asubuhi, akiwa na umri wa miaka 64, kwenye hospitali ya AMI, Msasani jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu ya kansa ya kizazi. 

Kwa mujibu wa Zitto, Saida ambaye hadi umauti unamkuta, alikuwa mwenyekiti wa Chama cah Walemavu nchini, mjumbe wa bunge maalum la katiba na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, atazikwa Jumatatu Juni 2, huko Mwanga-Kisangani baada ya sala ya mchana (Adhuhuri). Ameacha mume, na watoto 10, wanaume 6 na wakike wanne. alisema Zitto.
Picha zote kwa hisani ya Khalfan Said





0 comments: