hii ndiyo Marufuku ya Ya mtandao iliyaondolewa Uturuki
Serikali ya Uturuki imeondoa marufuku ya miezi miwili iliyowekwa dhidi ya mtandao wa kijamii wa YouTube .
Hatua hii inakuja baada ya mahakama ya juu zaidi
nchini humo kuwaamuru maafisa wakuu kurejesha huduma za mtandao huo,
ikisema kuwa marufuku hiyo ilikiuka sheria za uhuru wa kujieleza.Moja ya kanda zilizopeperushwa ilionyesha maafisa wakuu wa jeshi wakizungumzia nyenzo za kuingilia vita vya Syria na wengine wakiongea kuhusu ufisadi wakuwahusisha maafisa wakuu wa serikali ambao ni washirika wa Erdogan
Uturuki ilipitisha sheria yenye utata mapema mwaka huu ambayo iliwaruhusu wenye kutoa huduma hiyo kuikomesha bila kufuata amri ya mahakama.
Serikali pia iliweka marufuku kwa mtandao wa kijamii wa Twitter,ingawa marufuku hiyo iliondolewa mwezi jana.
Maafisa wakuu waliendelea kubana YouTube hadi Jumanne licha ya uamuzi wa mahakama ukitoa wito kwa serikali kuondoa marufuku hiyo.
Uamuzi huo wa mahakama ya juu zaidi pia unaonekana kama kupuuza serikali ya waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan, ambayo imekuwa ikikosoa vikali mitandao ya kijamii.
YouTube imewahi kubanwa tena nchini Uturuki mwaka 2007, lakini marufuku hiyo iliondolewa mwaka 2010.
0 comments: