USHIRIKIANO WA KIBIASHARA WA MESSI, ADIDAS NA FIFA UTAKAVYOMUATHIRI RONALDO KIBIASHARA HATA KAMA AKISHINDA BALLON D'OR


Cristiano Ronaldo amekumbana na habari mbaya kuelekea utoaji wa tuzo ya Ballon d'Or wiki ijayo baada ya kutoka kwa taarifa kuhusu makubaliano ya dili baina ya adidas - wadhamini wakuu wa Lionel Messi - na FIFA.


Katika vipengele vipya vya makubaliano, Adidas wana haki zote za kipekee za promotion ya bidhaa za Fifa Ballon d'Or , wakati Nike, wadhamini wakuu wa Ronaldo na mgombea mwingine wa tuo hiyo Franck Ribery, hawana haki za kibiashara kama ilivyo kwa Adidas kwenye tuzo hiyo.

Kwama maana hiyo inamaanisha kwamba mshambuliaji huyo wa Real Madrid, ambaye anapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo, hatoweza kutengeneza fedha nyingi kutoka kwenye ushindi wa tuzo hiyo kama ambavyo Messi amekuwa akitengeneza.

"Ushirikiano huu rasmi wa kibaishara na FIFA Ballon d'or ndio sababu sisi tunaweza kutumia tuzo hii kwa ajili ya shughuli zetu za promotion na kwa maana hiyo, kupitia makubaliano hayo, Nike hawawezi kupata nafasi hiyo," Ben Goldhagen, Senior PR Manager wa Adidas UK na Ireland, alisema
     

Adidas walitengeneza toleo maalum la kiatu cha f50 katika kusindikiza ushindi wa nne wa Ballon d'or wa Messi mwezi January 2013 na wamepanga kutengeneza tena kiatu hicho kwa ajili ya Messi bila kujali matokeo ya tuzo za Ballon d'or yatakuwaje.


Ronaldo na wadhamini wake Nike, hawaruhusiwi kisheria kutengeneza na kuuza kiatu cha namna hiyo ikiwa nahodha huyo wa Ureno atashinda tuzo hiyo.

0 comments: