Unatumia internet kupitiliza? Wataalam waeleza madhara yake kiakili
Wafanyakazi wanaojituma kwa kuendelea kufanya kazi kwenye computer zao
hata baada ya masaa ya kazi ili kumalizia shughuli zao wanaweza kuwa na
mafanikio zaidi lakini wana hatari ya kujikuta wamekuwa na uraibu na internet
na kuhatarisha afya zao za akili, imebainika.
Idadi kubwa ya waajiriwa imekuwa ikifanya kazi nje ya ofisi ili kujiongeza
kipata na kuborosha career zao lakini kuhatarisha ustawi wao, utafiti mpya
umebaini. Watafiti katika vyuo viwili vya biashara nchini Uingereza wamesema
makampuni yanapuuzia matatizo ya wafanyakazi kuanzisha tabia za uraibu huo kama
vile kuamka usiku kuangalia emails, kuwa na wasiwasi wakiwa mbali na computer,
sababu walioathirika siku zote huwa waajiriwa bora.
Dr Cristina Quinones-Garcia, wa Northampton Business School, alisema dhana hiyo
mpya ya wachapakazi kutumia zaidi mtandao kunaboresha ajira zaidi lakini kuna madhara
pia. ‘Watu hao wanaotumia teknolojia kuwasaidia kufanya kazi nje ya masaa ya kazi
hufanikiwa zaidi kwenye kazi zao lakini wapo hatarini kuathirika.’
Naye Nada Kakabadse, ambaye ni profesa wa sera, utawala na maadili katika Henley School
of Business, alisema wachapakazi hujikuta wakivuka mpaka usionekana na kuanza kutumia
internet zaidi ya inavyotakiwa. Muda wa kula na kulala huharibika, uhusiano huathirika
na watu huanza kujisikia tofauti wasipotumia computer.
Watafiti hao wanasema waajiri wanatakiwa kuwa na uelewa wa madhara kwa afya ya waajiriwa
na wanatakiwa kuweka utaratibu kwao wa jinsi ya kutumia internet nje ya ofisi kwa usalama.
0 comments: