TETESI ZA SOKA ULAYA - DIRISHA DOGO LA USAJILI
Wakala wa kipa wa Man Utd David De Gea amekataa kukanusha kuwa kipa huyo huenda akajiunga na Real Madrid (Marca), Manchester United wanajiandaa kutoa dau la dakika za mwisho kumwania beki wa Villarreal Gabriel Paulista, 24, ambaye tayari yuko katika mazungumzo na Arsenal (Daily Star), Chelsea wanashughulikia mkataba wa kumsajili kiungo wa Shakhtar Donetsk, Douglas Costa, 24 (Sun), meneja wa West Brom, Tony Pulis amethibitisha nia ya kutaka kumsajili winga wa Wigan Callum McMannaman, 23 na kiungo wa Man Utd Darren Fletcher, 30 (Times), meneja wa Swansea Garry Monk amethibitisha kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Norwich Martin Olsson, 26, na kiungo wa Stuttgart Alexandru Maxim, 24 (Wales Online), meneja wa Liverpool Brendan Rodgers anatarajia kuwa winga wa England Raheem Sterling, 20 atasaini mkataba wa muda mrefu katika klabu hiyo hivi karibuni (Sky Sports), Manchester City wametaka kupewa taarifa za upatikanaji wa mshambuliaji wa Southampton Jay Rodriguez, 25 (Manchester Evening News), Hull City wanamfuatilia winga wa Tottenham na England Aaron Lennon, 27 ambaye anajiandaa kuondoka White Hart Lane mwezi huu (Hull Daily Mail), kiungo wa zamani wa Chelsea anayechezea Wolfsburg, Kevin de Bryne, 23 anafuatiliwa na Arsenal na Manchester United, ingawa mwenyewe hataki kurejea Uingereza (Daily Star), mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez, 26, huenda asisaini mkataba wa kudumu moja Real Madrid anapocheza kwa mkopo, na huenda akarejea Old Trafford (Daily Express), nafasi ya kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny iko mashakani baada ya taarifa kupatikana kuwa washika bunduki hao wanamfuatilia kipa wa Fiorentina Noberto Neto, 25 (Daily Mail), Roma wanajaribu kuishawishi Chelsea kupokea pauni 380,000 ili kumchukua Mohamed Salah, 22 kwa mkopo hadi mwisho wa msimu (London Evening Standard). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Weekend Njema!
0 comments: