kama wewe ni shabiki wa Manchester United hii taarifa inakuhusu

Klabu ya Manchester United imewaonya mashabiki wake kuwa wanalazimika kununua tiketi kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kombe la FA dhidi ya Cambridge United na wakishindwa kufanya hivyo watapata adhabu .
Klabu hii imewaandikia mashabiki wake ambao bado hawajalipia tiketi za mchezo huo barua maalum ikiwataka waharakishe kununua tiketi na wakishindwa kufanya ghivyo watazuiwa kuingia uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Sunderland .
Mashabiki wa United wanaonunua tiketi za msimu wamelazimishwa kununua tiketi za mchezo wa marudiano wa kombe la FA kati ya United na Cambridge .
Mashabiki wa United wanaonunua tiketi za msimu wamelazimishwa kununua tiketi za mchezo wa marudiano wa kombe la FA kati ya United na Cambridge .
United ina mfumo ambapo mashabiki wenye tiketi za msimu wanakubali kununua tiketi za ziada kwenye michuano ya vikombe kama FA na Capitol 1 hukuwa kiwa na uhuru wa kuchagua kutonunua tiketi za hatua za awali za kombe la Capitol 1 na mechi za timu za vijana .
Uongozi wa United umesema kuwa hatua hii ya kuwatishia mashabiki kununua tiketi ni moja kati ya sheria ambazo amshabiki hukubaliana nazo kama masharti ya msingi ya kuwa mnunuzi wa tiketi za msimu .
Endapo mashabiki hao hawatanunua tiketi watazuiwa kuingia uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Sunderland kwenye ligi kuu ya England .
Endapo mashabiki hao hawatanunua tiketi watazuiwa kuingia uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Sunderland kwenye ligi kuu ya England .
Zaidi ya hapo taarifa mbaya zaidi  kwa mashabiki ni kwamba klabu hii pia imegoma  kupunguza bei ya tiketi kwa ajili ya mchezo huu dhidi ya Cambridge United utakaopigwa jumanne ya wiki ijayo kwenye uwanja wa Old Trafford .
United ilitoka sare ya 0-0 na Cambirdge hali iliyolazimu mchezo huo kurudiwa jumanne ijayo kwneye uwanja wa Old Trafford.
United ilitoka sare ya 0-0 na Cambirdge hali iliyolazimu mchezo huo kurudiwa jumanne ijayo kwneye uwanja wa Old Trafford.
source:milard ayo

0 comments: