mh shukuru kawambwa ajibu mapigo ya nape
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa amejibu madai yaliyotolewa hivi karibuni na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye kwamba ni mmoja wa mawaziri walioshindwa kazi hivyo kustahili kung’olewa.
Katika madai yake Nape alisema Dk Kawambwa ameshindwa kusimamia vyema
madai ya walimu na kwamba akiwa Waziri wa Miundombinu. Waziri huyo
aliingia mkataba na kampuni ya ujenzi ya Progressive iliyopewa zabuni ya
kujenga barabara ya Namtumbo hadi Tunduru wakati mkandarasi huyo hana
uwezo wa kuijenga.
Nape alikaririwa akisema kwamba umefika wakati kwa waziri huyo na
wenzake wa Fedha, Dk William Mgimwa; Kilimo, Chakula na Ushirika,
Christopher Chiza na Naibu wake Adam Malima kuhojiwa na Kamati Kuu (CC)
ya chama hicho.
Akijibu madai hayo mjini Bagamoyo jana Dk Kawambwa alisema anasubiri kwa hamu kuitwa CC kueleza tuhuma zinazomkabili huku akijigamba kuwa yeye ni mti wenye matunda ndiyo maana unapigwa mawe.
“Kuna maneno yanayoendelea hivi sasa eti na mimi mbunge wenu natajwa kuwa fisadi kwa mkataba wa ukandarasi wa barabara, siyo kweli. Wakati mkataba ule unasainiwa mimi nilishatoka kwenye Wizara ya Miundombinu, sihusiki kabisa na mkataba ule,” alisema na Dk Kawambwa
Source : Mwananchi/milard ayo

0 comments: