P-SQURE WAONYESHA HURUMA ZAO KWA WTOTO WALEMAVU KWA KUTOA ZAWADI
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule akipeana mkono na wasanii, Peter na Paul Okoye, maarufu kama P Square wakati walipowasili kwenda kutoa msaada katika kituo cha watoto wenye ulemavu wa usonji “Autism” (utindio wa ubongo) cha Msimbazi Mseto, jijini Dar es Salaam.
Msanii Peter Okoye akimuweka vizuri katika bembea mmoja wa wanafunzi wenye ulemavu wa usonji katika shule ya Msimbazi Mseto jijini Dar es Salaam. Wa kwa nza kutoka kushoto ni mwalimu Mkuu wa shule hiyo Reuben Gadi na Mjumbe wa bodi ya shule hiyo Mtumwa Nindi, na wa kwanza kulia ni mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Precious Hughes ambao ni wadhamini waliofanikisha wasanii hao kutua nchini
Wasanii wa kundi la P Square wakikabidhi misaada mbalimbali kwa watoto wenye ulemavu wa usonji wa kituo cha Msimbazi Mseto cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule akishuhudia makabidhiano hayo, na katikati ni walimu wa shule hiyo wakipokea kwa pamoja misaada hiyo.
Wasanii Peter na Paul Okoye Maarufu kama P square wakiwa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha huduma za jamii Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule wakicheza pamoja na watoto wenye ulemavu wa usonji wa shule ya msingi ya Msimbazi mseto, wakati waliposhiriki kutoa msaada katika shule hicho kwa watoto hao wenye mahitaji maalum.
Waviomba kuwapa ushirikiano wasanii wa muziki nchini · kufanya onesho
kwa masaa mawili mfululizo · Washiriki katika shughuli za kijamii Baada
ya kuwasili nchini usiku wa jana wanamuziki mapacha Peter na Paul Okoye
maarufu kama “P – Square” wametoa wito kwa vyombo vya habari nchini
kuwasaidia wasanii wandani na kuwa chachu ya mafanikio ya muziki kama
vilivyo vyombo vya nchi nyingine, huku wakiahidi kufanya makubwa katika
Shoo yao ya siku ya leo kwa mashabiki wao watakaojitokeza katika Viwanja
vya Leaders Club.
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika
hotel ya Hyatt jijini Dar wasanii hao wamesema wamefurahishwa na
mapokezi waliyoyapata kutoka kwa jamii ya Watanzania na waandaaji wa
Tamasha hilo na kuahidi burudani ya kipekee kwa Watanzania. Peter Okoye
ambaye ni mdogo wake na Paul alisema, vyombo vya habari vina mchango
mkubwa katika kuwajenga wasanii huku akitoa wito kwa vyombo hivyo kuwa
kichocheo cha kuwajenga wasanii na sio kuwabomoa.
“Vyombo vya nchini kwetu vimetufikisha hapa tulipo wamejitahidi
kutujenga na kutusaidia kusikika Afrika nzima., Tutaona fahari kama
vyombo vya hapa nchini pia vitajenga uwezo wa kuwasaidia wasanii wa
ndani nao waweze kufika au hata kuzidi hapa tulipo, Tutafurahi siku
tukiwaona wasanii kama kina Jay dee na Ben Pol wakija Nigeria kama sisi
tulivyokuja nchini kwao, alisema Paul.
Paul Okoye ambaye ni kaka kwa Peter amesema “Tumefurahishwa sana na
mapokezi tuliyoyapata tangu jana usiku hadi kufikia sasa, tumejisikia
faraja kuwa katika nchi hii ya Tanzania watu wake ni wakarimu sana sifa
hizi tumezisikia kwa watu mbalimbali na tumeshuhudia wenyewe tunawaahidi
Mashabiki wetu kufanya Shoo ya uhakika., alisema Paul Okoye. Kwa upande
wa wadhamini wakuu wa Tamasha hilo Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa
Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, alisema wamejisikia faraja kwa pamoja
kufanikiwa kuwaleta wasanii hao ili watoe burudani kwa Watanzania na
kuweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kutoa
msada wa vyakula katika shule ya Msingi Msimbazi Mseto kwa kupitia mfuko
wa kusaidia jamii wa Vodacom”
Vodacom Foundation”. “Kwa upande wetu sisi kama waandaaji kila kitu
kimekamilika kuanzia, masuala ya usalama na jukwaa vyote vimekamilika,
Pamoja na mambo mengine tunatoa wito kwa Watanzania kuwai kufika maana
onyesho litaanza saa 1 na kuwa sihii kuwa wastaarabu wakati wote wa Shoo
hiyo na kujiepusha na vitendo vyovyote ambavyo vinaweza kusababisha
uvunjifu wa amani. Wasanii kutoka Bongo watakao toa burudani katika
Tamasha hilo ni pamoja na wakongwe, Prof. Jay, Lady Jaydee, Jo
Makini”mwamba wa kaskazini”pamoja na Ben Pol.
Wakati huo huo wasanii hao na kitengo cha huduma za jamii cha Vodacom
Foundation wameshiriki katika kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto
wenye ulemavu wa akili cha Msimbazi Mseto kilichopo jijini Dar es
Salaam. Huku wakitoa wito kwa jamii ya Watanzania kuendelea kuwasaidia
watu wote wasio na uwezo ili kujenga jamii yenye maisha sawa kwa wote.
0 comments: