AZAM TV YAZINDULIWA RASMI NA MH. JANUARY MAKAMBA, CHEKI HAPA [PICHA] ZA MATUKIO MABALIMBALI YA UZINDUZI HUO
Mtangazaji wa Televisheni ya Azam TV Wasiwasi Mwabulambo akiwa kwenye Red Carpet kabla ya mahojiano na Mkurugeni wa Kajunason Blog Cathbert Angelo.
Afisa Mtendaji Mkuu na Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa Azam TV. Pichani akifanya mahojiano na Mtangazaji wa Azam TV Wasiwasi Mwambulambo.
Mtangazaji wa Azam TV Wasiwasi Mwabulambo akifanya mahojiano na Mdau William Malecela a.k.a LEMUTUZ na Mmiliki wa Blog ya Wananchi.
Yusuf Bakhresa akizungumza jambo na watoto wake kwenye uzinduzi huo.
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba (MB)
akizungumza kwenye uzinduzi wa Azam TV uliofanyika Hyatt Regency The
Kilimanjaro Hotel mwishoni mwa Juma ambapo amesema Azam TV imekujali
kuleta mapinduzi katika ulimwengu wa Digitali na kutoa fursa ya ajira
kwa Vijana wa Tanzania wenye vipaji sanjari na kuitangaza nchi yetu
katika bara la Afrika hasa kwenye upande wa Soka na Filamu.
Azam
TV itaanza kurusha matangazo yake Desemba 6 mwaka huu, Watanzania kaeni
mkao wa kula kupata King’amuzi kwa bei rahisi ambacho kitakuwa na
chaneli zisizopungua 50.
0 comments: