GATTUSO: NITAJIUA IKIWA NITAPATIKANA NA HATIA YA UPANGAJI WA MATOKEO
Gennaro Gattuso amezungumzia
skendo inayomkabili ya upangaji wa matokeo ya mechi akisisitiza, ikiwa
atagundulika ana hatia ya kosa hilo, atajiua mwenyewe.
Akizungumza na mwandishi wa Daily Mail John Greechan mchezaji huyo wa zamani wa Italia na AC Milan alikaririwa akisema:
Nimejiandaa kwenda pale town square na kujiua mbele ya kila mtu ikiwa nitapatiana na hatia ya kosa kama hilo.Maisha yangu yatakuwa hayana maana ikifikia hatua hiyo. Sitakuwa na nguvu na ujasiri wa kumuangalia mtu yoyote usoni. Naongea haya kutoka moyoni. Maishani mwangu, sijawahi kukaa na kuzungumza mtu yoyote kuhusu kupanga mbinu za kupanga matokeo na wala sijawahi kufikiria sula hilo, sijui hata wapi ningezanzia kufanya hivyo.Siwezi hata kucheza mchezo wa wachezaji watano dhid ya watano, kwa sababu sipendi kupoteza mechi, nachukia hilo suala. Hivyo upangaji wa matokeo kwangu ni upumbavu. Sijui nini wanataka kutoka kwangu, sijihusishi na upangaji wa matokeo, nimeudhika na kukerwa sana na tuhuma hizi.
Upangaji wa matokeo sio sehemu ya maisha yangu, nilikuwa nacheza kamari wakati ilipokuwa inaruhusiwa kisheria, lakini tangu ilipokatazwa kwa wanasoka, niliacha kabisa.
Ninajiamini sina hatia hata kidogo juu ya tuhuma hizi. Nimetumia maisha yangu yote kufanya kazi kwa bidii.
Juzi jumanne iliripotiwa kwamba Gattuso alivamiwa nyumbani kwake na maofisa wa kuzuia rushwa kwa uchunguzi baada ya kutolewa kwa amri ya kufanya hivyo na mwendesha mashtaka Roberto Di Martino.
0 comments: