HIKI NDIYO KISA CHA Baby Madaha KUTEMBEA  na  Meneja wake (Mkenya)

Kama ningekuwa Soud Brown aka Gossip Cop basi ningetumia msemo wa U Head!!!Hivi sasa sio siri tena kwani Baby Madaha ameamua kukiri na kuweka wazi kuhusu uhusiano wa kimapenzi na bosi wa Candy n Candy 'Joe Kariuki'
Msanii huyo wa filamu na muziki hapa nchini Tanzania Baby Joseph Madaha,ameimbia Global Publishers kuwa mwanzo yeye na Meneja wake hawakuwa na uhusiano wa kimapenzi toka aanze kusimamiwa kazi zake,lakini kutokana na maneno ya watu kumzushia ambacho kitu akipo basi ndio kilichompelekea aingie kweli kwenye Mapenzi na Meneja wake.
' “Kusema kweli huyu kaka kanikoleza jamani japo watu watachonga mengi lakini abadani sitosikiliza maneno yao, kwa kuwa awali sikuwa na uhusiano naye ila porojo za watu zilipelekea kuchukua maamuzi hayo natamani niamie Kenya ili tuwe karibu wakati wote,”alisema Baby Madaha.

Aliongeza kuwa kikubwa kilichompelekea kuwa naye ni kutokana na upendo wake wa kweli alionao kwake siyo kutokana na suala la mkwanja kama wengi wanavyodhani.
source:djfetty

0 comments: