Rich Mavoko atoa machozi kwa Mama Sharo Milionea kisa hiki hapa

Hitmaker wa Roho Yangu Rich Mavoko amemtembelea mama mzazi wa marehemu Sharo Milionea huko Muheza Tanga. Mavoko amepost picha hii akiwa na mama mzazi wa msanii huyo aliyefariki Novemba mwaka jana inayoonesha akiwa kwenye simanzi zito kutokana na alichokuwa akisimuliwa na mama huyo.

 Huu ndio ujumbe wa Rich Mavoko aliyouandika baada ya kusimuliwa na mama huyo.

 "Muda mwingine wasanii tunahitaji tukumbuke wenzetu walio tangulia tena kwa kuwa enzi ata kwa kuwatembelea ndugu zake coz kuna vitu vinauma sana ukielezewa hapa alikuwa ana nielezea sharo baada ya kufa haki zake nyingi hajui zipo zinaenda wapi na mambo mengi yanayo muhusu marehem sharo kiukweli ili niuma... pole sana mama angu binadamu ndivyo walivyo,” ameandika Mavoko.

0 comments: