kombe la dunia brazili laukumbwa na balaa jingine
Maandalizi
ya mashindano ya kombe la dunia yako hatarini kuingia dosari baada ya
wafanyakazi wa viwanja kadhaa ambavyo vinaendelea kujengwa kupanga
kufanya mgomo .
Wafanyakazi hao wamepanga kufanya mgomo baada ya kutoridhishwa na mazingira ya usalama kwenye maeneo ya ujenzi .
Wafanyakazi
hao wamekuwa wakilalamikia hali ya usalama kuwa mdogo kwenye viwanja
ambavyo ujenzi wake haujakamilika baada ya kuwepo na matukio ya
wafanyakazi kufariki dunia kwenye maeneo ya kazi kutokana na ajali
katika matukio tofauti .
Endapo
mgomo huo utafanyika maandalizi ya kombe la dunia yatakuwa yamepata
pigo kutokana na baadhi ya viwanja kushindwa kukamilisha ujenzi wake
ndani ya muda uliopangwa.
0 comments: