DARASA AFUNGUKA NA KUDAI SASA ''NARUDI DARASANI'' PITIA KISA CHA YEYE KUFIKIRIA KURUDI DARASANI
STAA wa Sikati Tamaa, Shariff Sadick Ramadhan ‘Darasa’ yupo mbioni kurudi darasani baada ya kufanya muziki muda mrefu.
Darasa katika pozi.
Akifunguka hivi juzikati katika mahojiano na Kipindi cha Mtu Kati
kinachorushwa na Global TV Online kupitia mtandao wa Global Publishers,
Darasa alisema mpango alionao kwa sasa ni kuangalia upande wa pili ambao
ni elimu.“Kila mtu anajua picha ya mtaani jinsi ilivyo, najaribu kujipanga kwenda darasani ili nibalance kwenda sehemu nyingine, pia ni kitu ambacho nimekiweka mbele kuliko kitu kingine chochote na kwenye maisha ya mtaani naishi maisha ya kawaida ambayo mtu akipata anakula na akikosa anakomaa,” alisema.
Darasa amezungumza mengi sana kuhusiana na muziki na maisha yake kwa ujumla. Kwa mahojiano zaidi na mengine yahusuyo jamii na mastaa yanapatikana katika mtandao kupitia tovuti ya www. globalpublishers.info kisha bonyeza eneo lilioandikwa Global TV Online ujipatie uhondo kamili.
0 comments: