Picha 8 za Mahabusu alievua nguo Mahakamani Mwanza jana
Tukio hilo limetokea May 7 2014 saa nne asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Nyamagana Mwanza walipofikishwa kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi zao lakini ghafla walipofika kwenye viwanja vya mahakama hiyo walitimua mbio kuelekea kwenye mlingoti wa Bendera hiyo ya Taifa na kuvua nguo kisha kuanza kupiga kelele kwa kupaza sauti kudai haki itendeke.
Ni Thobiasi Warioba (35) alieamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu eneo la mlingoti wa bendera ya taifa, ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji Na. 32/2012.
Watuhumiwa
wengine waliojaribu kutoroka ni Hamis Ramadani (30), Anthony Petro
(35), Marwa Mwita (38), na Chacha Wangwe (35), na mwingine ambaye
hakufahamika majina yake mara moja, wote wanakabiliwa na kesi ya Jinai
Na. 215/2013 na walikamatwa tangu mwaka 2011.
Baada
ya kudhibitiwa na askari polisi walisikika wakisema: “haiwezekani tangu
mwaka 2011 tulipokamatwa hadi sasa kesi zetu hazijasikilizwa, wengine
tumebambikiziwa kesi tunaomba haki zetu, polisi mnatuonea, vyombo vya habari tunaomba mtusaidie tumekaa
muda mrefu bila kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu 2011
tulipokamatwa, tumechoka kukaa mahabusu tunaomba kesi zetu zisikilizwe”.
Baada
ya malalamiko yao askari mmoja aitwae Inspekta Henry akiwa na wenzake
sita waliokuwa wakiwadhibiti wasikimbie aliwahoji kuhusiana na madai yao
huku askari hao wakiwataka kuondoka katika mlingoti huo na kumtaka
Warioba avae nguo ili waweze kuingia Mahakamani.
0 comments: