Sheria mpya za Kiislamu Brunei zilizofanya hoteli za mfalme zisusiwe
Brunei wametangaza utumiaji wa sheria mpya kwa raia laki nne na elfu 16 wa nchi hiyo ndogo yenye utajiri mkubwa wa mafuta ambayo imekua ikiongozwa na Hassanal Bolkiah kwa takriban karibu ya nusu karne hivi sasa.
Bolkiah ameanzisha kanuni mpya ya adhabu ambazo zitafanyika kulingana na mwenendo wa dini ya kiislam akisema adhabu hizi ni njia ya kufuata maamrisho ya mwenyezi Mungu ili kulinda falme yake na ushawishi unaotoka nchi za nje ambapo mara nyingi wamekua wakishawishika kupitia mitandao ya kijamii.
Anasema “Allah ni mkarimu na kwa sababu ya ukarimu wake ametengeneza sheria kwa ajili yetu ili tuzitumie kupata haki katika nchi yetu, hatujawahi kuchukulia wengi vibaya na wala hatuwategemei wao kukubaliana na sisi lakini ni vizuri wakatuheshimu kama tunavyowaheshimu”
Adhabu zinazohusika ni pamoja na kupigwa mawe mpaka kifo, kupigwa mijeledi (floggings) na kukatwa viungo vya mwili kama miguu kwa makosa kama ya uhusiano wa jinsia moja, wizi, mimba za nje ya ndoa, unywaji pombe, kukosa kwa sala za Ijumaa, kukufuru (makosa ya lugha),ulawiti n.k na adhabu zinaweza kupungua ama kufutwa kwa wale walio chini ya miaka 18.
Kwa sheria hizi za sasa ubatizo makanisani utashindikana kufanyika kulingana na sheria hizi mpya nchini humo ambapo tayari
tume ya kimataifa ya wanasheria (ICJ) imesema sheria hizo hazitalingana na makubaliano ya sheria za kimataifa na mkuu wa tume ya haki za binaadamu UN amesema anapingana na sheria hizo.
Hoteli
hii iliyopo California Marekani ni miongoni mwa hoteli zilizosusiwa na
baadhi ya mastaa, hata wanaoandaa tuzo kubwa za dunia za Oscar wamesema
hawatofanya party hapa kama ilivyo kawaida kila mwaka wanavyofanya kabla
ya tuzo zenyewe.
Shinikizo nchini Marekani sasa hivi ni kutaka mfalme huyu azifute hizo sheria la sivyo auze hizi hoteli maana watamsusia.
0 comments: