PICHA MNARA WA KUPINGA MAUAJI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI WAZINDULIWA WILAYANI SENGEREMA MKOANI MWANZA.
![]() |
Rais wa Shirika linalohudumia watu wenye ulemavu wa ngozi duniani liitwalo Under the Same Sun, Peter Ash (wa pili kushoto) pamoja na mratibu wa shirika hilo nchini Vick Ntetema, wakiwa na Mkuu wa wilaya ya Sengerema (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na Katibu Tawala wa wilaya ya Sengerema Alfred Kapole (kulia) wakishikana mkono mara baada ya rais huyo kuzindua Mnara wa kwanza wa kipekee wa kumbukumbu ya watu waliouawa nchini Tanzania katika matukio mbalimbali yaliyo husisha imani potofu za kishirikina na suala la albinism. |
![]() |
Mnara huu wa kwanza wa kihistoria dunia umesimikwa katika kipita shoto kikuu kinachounganisha barabara zinazoelekea mkoa wa Geita, Kahama, Bukoba mkoani Kagera na Kamanga mkoani Mwanza, ukiwa umeorodheshwa majina takribani 72 ya watu wenye albinism waliouawa. |
![]() |
Kabla ya uzinduzi huo maandamano yalifanyika yakihusisha wageni pamoja na wananchi wa wilaya ya Sengerema walio hamasika na mpango huo ulionuia kutokomeza kabisa mauaji hayo ya kinyama. |
![]() |
Viongozi wa kada mbalimbali wilayani Sengerema wakiwa na Rais wa Under the Same Sun Bw. Peter Ash wakisoma majina ya watu wenye albinism waliouawa kwa matukio ya ushirikina. |
![]() |
Mnara uliozinduliwa unamwonyesha baba asiye na ulemavu wa ngozi akiwa amembeba mabegani mtoto wake mwenye albinism huku mama ambaye pia hana ulemavu wa ngozi akisaidia kumvika kofia mwanaye. Kumbe sasa hata baba na mama wasio na albinism katika mwonekano wa ngozi ya kawaida wanaweza kuzaa mtotomwenye albinism. |
![]() |
Pia Shirika hilo la
Kimataifa la kutetea haki za watu wenye ulemavu wa ngoziduniani kupitia Taasisi
yake ya Under the Same Sun limetoa tuzo ya kwanza duniani kwa vyombo vya habari
127 hapa nchini ikiwemo kampuni ya IPP MEDIA ambayo imejinyakulia ushindi
mkubwa wa tuzo 5. Pichani Mwakilishi wa ITV Cosmas Makongo akitoka kupokea moja kati ya tuzo.
|
![]() |
Ni tuzo ya kwanza duniani kwa vyombo habari na waandishi wake ambao wameibuka washindi kwa kuhamasika kufuatilia kwa ukaribu matukio mbalimbali yaliyojitokeza na kuyawasilisha kwa jamii. |
![]() |
Mwakilishi wa ITV Cosmas Makongo akipata mkono wa pongezi kutoka kwa Katibu Tawala wilaya ya Sengerema Alfred Kapole mara baada ya kupokea Tuzo kwa Kampuni yake ya IPP kupitia ITV kwa kutangaza bure habari na vipindi vilivyokuwa vikihamasisha kupungua kwa mauaji ya kinyama dhidi ya albinism hapa nchini. |
![]() |
Rais wa Under the Same Sun Peter Ash akitoa hotuba yake kwa jamii iliyofurika katika viwanja vya Telecenter mjini Sengerema. Huku akiwa na baadhi ya watu walioathirika na matukio ya kinyama walio nusurika kuuawa wakipoteza baadhi ya viungo vyao. Kutoka kushoto ni Bi. Mariam ambaye alipoteza mikono yake kwa kukatwa mapanga na watu waliokuwa wakihitaji viungo vya albino kwaajili ya masuala ya ushirikina, mtoto Festo aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na kukatwa kabisa mkono wake wa kushoto huku aking'olewa meno pamoja na Said Abdalah mkulima mkata mkaa aliyekatwa mkono wake wa kushoto kwa imani hizo hizo. Inasikitisha. |
![]() |
Wadau wa Taasisi ya Under the Same Sun Vick Ntetema (L) na Gamariel mboya (R). |
![]() |
Nao wazazi wenye watoto wenye albinism walifika eneo la tukio kupata elimu. Kutoka kushoto ni Daudi Nzila akiwa na mwanae Elikana na Mathayo Felician akiwa amempakata mwanae Faustin. |
![]() |
Mahudhurio yalikuwa makubwa huku huzuni ikitawala. |
![]() |
Wanahabari mstari wa mbele kunasa matukio. |
![]() |
Eneo lilifurika watu kiasi cha wengine kujikita pembezoni mwa barabara. |
![]() |
Mwanadada Mariam aliyekatwa mikono yake yote na wavamizi, aliwatoa machozi wengi kwa simulizi ya |
0 comments: