hii ndiyo Ndege ya kijeshi ya Ukraine iliyodunguliwa
Waziri wa Ulinzi nchini Ukraine
amesema kuwa mojawapo ya ndege zake za kijeshi za kubeba mizigo
imedunguliwa na wapiganaji wanaounga mkono Urusi ilipokuwa ikitua katika
uwanja wa ndege wa Luhansk mashariki mwa taifa hilo.
Ndege hiyo ya jeshi la angani la Ukraine ilikuwa ikiwabeba wanajeshi pamoja na vifaa.Idara ya maswala ya kigeni mjini Washington ,Marekani imesema kuwa ina hakika kwamba mizinga pamoja na silaha nyengine kali zinazomilikiwa na wanamgambo wanaotaka kujitenga nchini Ukraine zilitoka nchini Urusi.
Msemaji wa Idara hiyo amesema kuwa mizinga iliokuwa katika kambi moja ya silaha za kijeshi kusini magharibi mwa Urusi iliondolewa katika kambi hiyo.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Uingereza William Hague amesema kuwa kuingia kwa vifaa hivyo nchini Ukraine hakuwezi kukubalika.
0 comments: