Picha 25 baada ya moto kuteketeza soko la wamachinga Karume leo.
Kwa mujibu wa mashuhuda kadhaa waliokuwepo katika eneo la tukio tangu moto huo unatokea, Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana ingawa wana wasiwasi na hitilafu ya umeme iliyojitokeza usiku wa June 10.
Moto huo ulianza kuwaka majira ya saa 4 usiku ambapo iliwachukua zaidi ya saa moja kikoasi cha zima moto na uokoaji kufika eneo la tukio. Baadhi ya Wafanyabiashara ambao bidhaa zao zimeteketea kwa moto wamesema kuwa wamepata hasara kubwa ambayo haielezeki kwani baadhi yao wameshindwa kuokoa hata kitu kimoja.
Soko la Karume ni miongoni mwa masoko makubwa ya mitumba yanayotumiwa na wakazi wengi wa jiji la Dar es salaam na maeneo jirani kutokana na urahisi wa bei wa bidhaa zinazopatikana hapo.
Hizi ni baadhi ya picha zilizopigwa asubuhi ya leo baada ya tukio hilo ikionyesha madhara makubwa yaliyotokea baada ya ajali hiyo mbaya.
source/credit to:milard ayo.com
0 comments: