JOSE MOURINHO: WASHAMBULIAJI WANAIGHARIMU SANA CHELSEA


Mourinho ametoa ishara kwamba kikosi cha Chelsea anachofanya nacho kazi sasa hakina vifaa kama ilivyokuwa wakati ule alivyokuja Stamford Bridge mara ya kwanza, akisisitiza washambuliaji wanaigharimu timu vya kutosha. 

Kocha huyo wa The Blues pia amepinga kwamba timu yake ilikuwa ni moja ya timu zinazopewa nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu, kufuatia kipigo cha kushtusha kutoka kwa Stoke City wikiendi iliyopita.

Fernando Torres, Samuel Eto'o na Demba Ba wamekuwa wakihangaika kuwa katika fomu nzuri msimu na kwa pamoja wote wamefunga mabao manne tu katika EPL msimu huu.
Takwimu za washambuliaji wa Chelsea  2013/14 Premier League
PlayerLeague AppearancesLeague GoalsAvg. Goals Per Game
Fernando Torres1010.10
Samuel Eto'o820.25
Demba Ba610.166

PremierLeague.com
Katika kipindi kirefu cha maisha yake ya ufundishaji soka, Mourinho amekuwa na imani kubwa na washambuliaji wake kama vile Didier Drogba, Zlatan Ibrahimovic na Cristiano Ronaldo.
Torres amekuwa akionyesha afadhali, akionyesha kiwango kizuri - hasa katika mechi dhidi ya Manchester City—lakini bado hajaweza kurudisha urafiki wake na nyavu za wapinzani. 
Dhidi ya Stoke, Andre Schurrle alifunga mabao mawili huku Torress, Ba na Eto'o wote walishindwa kufnga pamoja na Chelsea kujaribu kufunga kwa mashuti 15 katika goli la wapinzani.
Kama wangeshinda dhidi ya Stoke City, Chelsea wangeweza kuisogelea Arsenal na kutengenishwa na pointi mbili baina yao, lakini ubutu wa safu yao ya ushambuliaji uliwakosesha nafasi hiyo.
source:shaffih dauda

0 comments: