Kanye West aziponda tuzo za Grammy kwa kutajwa mara 2 tu, asema ni za ubaguzi wa rangi
 
 
Kanye West haishi kulalamika siku hizi. Awamu hii kama kawaida aliamua kuitumia 
show yake ya Arizona kupaza sauti kuwalalamikia maafisa wa ‘US Recording Academy’ 
kwa kuitosa album yake ‘Yeezus’ kwenye kipengele cha album bora ya mwaka ya tuzo za 
Grammy.

Rapper huyo aliamua kusimamisha kwa muda show yake mjini Phoenix kuelezea kuumia 
kwake kufuatia kutajwa kwa majina ya tuzo hizo yaliyotangazwa wiki iliyopita.
Alisikika akisema: Nina miaka 36 na nina Grammy 21. Hizo ni Grammy nyingi zaidi 
kwa mtu mwenye miaka  36. Katika Grammy hizo 21 sijawahi kushinda Grammy dhidi ya 
msanii mzungu. Majina yalipotoka Yeezus imepata nominations mbili tu kwenye Grammys, 
nini wanachojaribu kusema? Hivi wanadhani siwezi kugundua?
Wanafikiri kwamba, kwa namna moja kwamba nina nguvu ya kuipoteza kabisa 
heshima yao katika wasaa huu?
West amekubali kuwa hajaridhishwa na kutajwa mara mbili tu kuwania tuzo hizo 
ambazo ni album bora ya rap na wimbo bora wa rap ‘New Slaves, na kuongeza:  

0 comments: