Smarty Ring: Pete inayounganishwa na smartphone kwa bluetooth, inauwezo wa kupokea simu, na kutumika kama remote control

Pamoja na kuwepo Smartwatches sokoni, sasa kuna pete inayoweza kuunganishwa na smartphone
 na kutoa taarifa (notification) pindi ujumbe, barua pepe, zinapoingia katika simu.

 ni pete inayounganishwa na smartphone kwa bluetooth, na kumuwezesha mtumiaji ku-control 
simu yake hata ikiwa mbali na yeye.
Ina buttons zinazoweza kutumika kupokea simu, na kuplay muziki uliopo katika smartphone ya 
mtumiaji.
LED screen ya pete hiyo huwaka pindi mtu aliyeivaa anapopokea e-mail, ujumbe mfupi, facebook 
na twitter notification, au simu inapoingia, na pete hiyo inaweza pia kutumika kama remote 
control.
Smarty Ring imebuniwa na engineer Ashok Kumar kutoka Chennai, India. 
Pete hiyo imetengenezwa na ‘Bluetooth 4.0 sensor inayoweza kuunganishwa na simu 
yoyote ya Android au  iOS kupitia application maalum ya Smarty Ring

Panapokuwa hakuna notification yoyote kwenye simu, LED screen ya pete hiyo inaonesha muda.
Simu inapoingia, aliyeivaa pete anauwezo wa kuchagua kupokea au kuikata simu kwa kutumia 
buttons ambazo ziko pembeni mwa pete hiyo.

Smarty Ring zitapatikana kwa gharama ya $275 (442,000 Tshs) pindi zitakapoingia sokoni
 April mwakani.Mwezi September wabunifu wengine wa Hungary walitambulisha pete kama hiyo  
 ambayo yenyewe inaonesha muda pekeyake. 

0 comments: