Shindano la miss Tourism Tanzania limefungiwa, kwa sababu gani?


TOURISM Baraza la Sanaa la Taifa limeyafungia mashindano ya urembo ya Miss Tourism Tanzania,s ababu kuu zikiwa mbili.
1. Afisa Habari Mkuu kutoka Baraza la sanaa la Taifa Agness Kimwaga amesema ‘kwanza mashindano Miss Tourism Tanzania 2013 kushindwa kufanya tathmini ya mashindano ya miss Tourism 2012/2013 kwa muda uliokubalika baada ya maonyesho hayo kufanyika, na sababu nyingine ni kukiuka masharti, kanuni, miongozo na taratibu za uendesheaji wa mashindano ya urembo kama zilivyowekwa na serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa,  hizo ndio sababu za kulifungia shindano kwa muda usiojulikana’
2. ‘Tukiwa na ushahidi uliokamilika kutoka kwa warembo wenyewe waliohusika hatuwezi kufungia kitu pasipo ushahidi, kumbuka mashindano haya yanapokuwa yanaendelea Serikali haikai kwenye zile kambi kwa muda wote wanaokaa kwa kuwa mara nyingi tunapokwenda kutembelea warembo tunawaambia popote panapokua na tatizo watupe taarifa, tusipopata taarifa hatuwezi kumfungia mtu pasipo taarifa, tumekua na taarifa za uhakika toka kwa warembo wenyewe ndo maana tumechukua hatua’
3. ‘Tunasema kwamba unapoendesha shughuli yoyote ya sanaa usifanye vitu ambavyo vinaweza kumdhalilisha mtazamaji au muhusika anaefanya kitu kile kwa hiyo kuna vitu ukifanya vinaweza kumdhalilisha mtu kwa njia moja au nyingine umekiuka kanuni na taratibu mfano kumnyanyasa kijinsia, kwanza kabla ya kukufungia tunakwambia umekosea nini na tunakupa muda kurekebisha yale makosa yaliyofanyika’
4. ‘kama unakumbuka zamani Miss Tanzania watu walikua wanapanda na yale mavazi ya ufukweni yakiwa tupu jukwaani lakini taratibu tumewaambia hairuhusiwi kupanda hivyo hivyo yeyote anaekosea ni lazima arekebishwe, sasa kama tunatuma barua na hakuna kilichorekebishwa inakua ni kinyume na utaratibu’

0 comments: